KIAPO CHA SIRI (Damu yangu haipotei) MTUNZI : ZAYNAB TALY SEHEMU YA 11. ILIPOISHIA...... Aliongea maneno ya kulaumu na kukufuru huku machozi yakimtoka, tegemeo la pekee kwake alikuwa stellar hakuwa na budi zaidi ya kurejea kwake na kujipanga ilikupambana na maisha aliyonayo. ******* SONGA NAYO ******* "Sam una nini kaka angu mbona umeondoka na furaha na hata ulivyorudi umekuwa kama mtu aliyefikwa na Jambo zito..? ". "Acha tuu dada Anna muda mwingine unaweza ukajuta kuja duniani kwa yanayokufika ". "kwani vipi embu nieleze imekuwaje kwani? "Alimuliza Anna aliyekuwa mpangaji mwenzie wa chumba cha jirani. Bila kusita Sam alimuelezea Anna kila kilicho mfika juu ya mwanamke yule ambaye aliwaza kuwa ndiye ndugu na msaada pekee kwake. "Usijali kila kitu kinacho sababu ya kutokea kwake usimlaumu mungu kwa kukuumba analo kusudio madhubuti muhimu kumshukuru na kupigana ili kujua ni ipi hatima yako. "Zilikuwa jitihada za Anna juu ya kumpa moyo na kumfanya atulie. Hatimaye siku ilipita Salama japo moyoni mwake Sam hakutaka kuamini kilichitokea. "sawa binti yao wamuozeshe ila kiumbe changu nakihitajia kikiwa hai ".Alijisemea mwenyewe wakati amejilaza kwenye kitanda chake cha kavu ambacho kukicha kilikuwa kikimkumbusha liwazo alilokawa akilipata kutoka kwa mwanadada yule kutoka katika familia ile ya kitajiri. Uzoefu wake katika kuishi na wasichana mbali mbali katika mahusiano ya kimapenzi hukuwahi kumpata msichana aliyekuwa Tayari kubeba ujauzito wake ,hivyo Stellar alikuwa na nafasi ya kipekee mno kwake . Mara mlango ulifunguliwa kwa ghazabu na binti aliyeonekana kuwa katika majonzi na hofu ya kukimbizwa huku akitweta kwa Kasi akaingia. "Stellar.. ?".Aliita Sam baada ya kumgundua aliyekuwa ameingia ndani ya chumba chake. "Umefata nini hapa..? ".Alihoji huku akiinuka na kumsogelea pale alipo kawa Stellar. "Sam siwezi siwezi kuishi bila wewe mwanangu pia awezi kuishi bila baba ". "Ila baba yako awezi kuwa radhi na mimi uoni utakuwa umenipa janga Mimi nimekuruhusu kuolewa huko wanako taka wazazi wako ila nakuomba ukumbuke kiapo ambacho tulipa." Akafunua Kola ya sharti lake ambayo ilifunika sehemu ya alama Zile za meno walizowekeana kama ahadi wengine wanaita love bite. "nakuomba umtunze mwanangu ukishajifungua nakuomba uniletee nimtunze ndiye ndugu pekee nitakaye ishi naye na ndiye nitakaye mtarajia anizike". "Sam siwezi kuishi na Elly mwanaume ambaye ni chaguo la wazazi wangu sio pendekezo langu naomba uniruhusu niishi hapa kwako". Baadae wakaridhiana kuishi pamoja kwani hakuwepo Kati yao aliyetamani kuwa mbali na mwenzie kwa namna yoyote ile japo hali Zao za maisha ziliwapa changamoto. "Nakupenda Sana Sam sitarajii kuwa mbali na wewe kwa lolote ". "nakupenda pia Stellar wewe ndo mwanamke wakunifanya tajiri kwa fikra ila nimasikini wakutupwa kiuhalisia ". Wanatabasamu wote kisha wakakumbatiana na mwisho usingizi ukawa wa Chukua. Tabasamu lilidumu katika sura ya Sam kana kwamba alikuwa akifungua kurasa mpya katika maisha yake. Mwili ulianza kuongezeka uzito akawa mwenye kunawili Kiasi kitambi kikaanza kutokea. Jioni moja akiwa katika shughuri za kila siku nyumbani kwake mara walikuja vijana wawili walio shiba kweli kweli huku wakivalia mashati meupe na suluari Za kitambaa. "karibuni ".Ndio kauli pekee aliyoweza kuwaambia baada ya kuwaona wakielekea pale alipo kawa . "Asante Sana, sisi ni afisa wa polisi Kutoka kituo cha Kati unatuhumiwa kwa kuishi na binti wa watu bila ridhaa ya wazazi wake. " "Binti yupi jamani Mbona Mimi na ishi na mpenzi wangu tuu hapa naye kazidi miaka kumi na nane na anaakili timamu Mbona. "Yalikuwa maelezo ya Sam huku akikokotwa asijue hatima yake na mwingine miongoni mwa wale afisa wa polisi aliingia kunakochumba cha Sam na Kutoka na Stellar ambaye pia alichanganyikiwa juu ya tukio lile. ******************************** "Stellar usije ukanisumbua tena tafadhali kila kitu kimeshakaa sawa utake usitake utaolewa na Elly na huyu mpuuzi wako ataozea jela. "yalikuwa maneno makali aliyekuwa akiongea mzee SUDDEIS kwa binti yake wapekee ambaye ulipita Mwezi sasa hakumuona nyumbani baada ya tukio la utambulisho kufeli. ITAENDELEA.... USISAHAU KULIKE NA KUDONDOSHA COMMENT YAKO YA NGUVU MUAMBIE NA MWENZIO AJISOGEZE KARIBU NA KURASA HII MARIDHAWA YA MKONO WANGU.... ULIKUWA NAMI MWANADADA YULE KUTOKA KATIKA FAMILIA YA KUWAELIMISHA NA KUBURUDISHA JAMII YA HADITH APP ZAYNAB TALY.....

at 4:22 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top