Home → simulizi
→ KIAPO CHA SIRI
(Damu yangu haipotei)
MTUNZI : ZAYNABTALY
SEHEMU YA 10.
ILIPOISHIA.......
hatimaye Asubuhi iliwasili na purukushani za hapa na pale zilianza. Sam alikuwa bize kutafuta nguo itakayo mkaa vyema na kumfanya aonekane ni miongoni mwa watu wenye hadhi sawa na stellar ambaye bila shaka moyo wake ulijua siku hii ilikuwa ni siku adhimu mno kwake nasiku ambaye ingempa jibu moja Kati ya mawili kama ndio au hapana.
***********SONGA NAYO **********
Dakika zilisogea na hatimaye Lisaa mpaka Masaa akiwa anachagua nguo ya kuvaa na asijue ipi itampa hadhi sawa na msichana yule mrembo Kutoka katika familia ya kitajiri.Hatimaye alibahatika kuiyona nguo ambayo itampa thamani mbele za macho ya watu.
Ilikwa miongoni mwa nguo nzuri alizowahi kununuliwa na stellar kutahamiki ilikuwa saa Tatu Asubuhi ambapo alihitajika kufika kwa kina stellar saa nne kamili haraka akawahi palipo na pasi ya Umeme ili aweze kuziweka sawa nguo alizohitajia kuzivaa na kufanya aonekane nadhifu.
"mungu wangu Umeme umekatika!".Alimaka baada ya kugundua hatoweza Kunyoosha nguo zake,haraka akaiwahi simu yake ambayo mara ya mwisho kuiweka kwenye chaji ilikuwa Juzi yake kuishika tuu na kuiwasha kabla ya kufanya chochote simu ilizima chaji.
"Daaah kweli kufa kwa nyani miti yote uteleza ".Haraka akatoka nje kwa jirani ambaye alimzoea na kuazima pasi ya mkaa kisha akaziweka sawa nguo zake na kuingia bafuni na baada ya dakika chache alikwisha vaa na akawa Tayari kwa kutoka.
"Dada Anna? ".Alimuita yule jirani ambaye alimsaidia pasi ile ya mkaa.
"Abee kaka angu ".Mara Anna alitoka ndani ya chumba chake ambapo alikutana na Sam akiwa smart kabisa katika mavazi yake.
"Looh umependeza Sana Leo sijui safari ya wapi hiyo au ndo...? "Aliuliza Anna ambaye kukicha ndio mpangaji pekee aliyekawa akiyaamini maisha ya Sam bila kuyapa dosari yoyote.
"Ndo nini Jamani Sista ushaanza hivyo, sasa Sikia asante Sana kwa msaada wako ila bado nilikuwa ninaombi jingine ".aliongea huku akimkabidhi pasi ile ya mkaa.
"Ombi gani hilo..? "Aliuliza Anna ambaye alikuwa makini kumsikiliza.
"Nidogo Sana naomba unisaidie kujua wakati ni saa ngapi saizi maana simu yangu haina chaji kabisa. ".
"Ooh hilo dogo mno "Aliingia ndani na Kutoka na simu yake ya mkononi ambayo nayo pia chaji ilikuwa ikififia.
"saa nne na robo saizi ".
"Eeh..? Saa nne? ".Aliuliza bila hata kusubiri jibu kisha akaanza kuondoka kwa haraka ilikuweza kuwahi palipo natukio. Muda watukio ulikwisha pita na umbali kutoka vingunguti mpaka mbezi uliongezwa kutokana na foleni ya njiani kutokana na msongamano wa watu jijini Dar es salaam.
"Mungu wangu , nimechelewa mno. "Aliongea mwenyewe huku akiwa naharaka kuelekea palipo kituo cha mabasi.
***********************************************
"Nimemsubiri mno huyo unayesema ndo Mchumba wako Unataka kumtambulisha nimechoka utaolewa na Elly utake usitake ".Aliongea kisha akainuka na kuelekea lilipo paki gari lake kisha akaondoka zake.
Lilikuwa pigo kwa upande wa Stellar ambaye alikwisha pata tumaini jipya juu ya hatima yake yeye na Sam. "Sam.. Sam sijui kapatwa na nini."
"Stellar mwanangu hivi unafikiri Sam anakupenda kweli..? "aliuliza mama stellar.
"Ndio mama Sam ananipenda ananipenda Sana."
"sasa imekuwaje Mbona anaipoteza siku hii muhimu kwenu ila ulimwambia kilichokawa kimejili kwa baba ako lakini ..?"
"mama Sam nimemwambia kila kitu ".
"sasa..? "
"mama misielewi na simu na mpigia hapatikani mama ".Aliongea huku kwikwi ya kilio ikichukua nafasi. Haukupita muda mara mlango uligongwa kufungua hakuwa mwingine.
"Sam ushapoteza nafasi muhimu ambayo ulikuwa umepewa na baba yangu Sam mimi na wewe hatuwezi kuwa mke na mume ".
Yalikuwa maneno ya stellar baada ya kufungua mlango na kukutanisha macho yake na Sam.
"Nisamehe mpenzi halikuwa kusudio langu kufanya hivyo niwieradhi ?".
"Hata nikikusamehe Sam sijui Kama tunaweza kuwa Kama tulivyodhani Sam kiwapi kiapo Chetu cha siri? ".
Huzuni ilitawala baina yao hakukuwa na mwenye kulipokea Jambo lile katika hali ya kawaida. Kila mmoja aliwaza kuitetea nafsi ya kiumbe hai kilichopo tumboni mwa stellar ila ni kivipi wakati walikwisha feli katika jaribio lao muhimu ambalo walipaswa kulifanikisha.
Baada ya kuipoteza bahati ile hakuwa na jinsi zaidi ya kujongea taratibu akirejea kwake. "Kweli ng'ombe wa masikini azai ".Alijisemea mwenyewe asijue ni wapi anaweza kuanza iliwalau na yeye maisha yake ya jengwe vyema na nguzo ya furaha.
"umasikini..? Usinifanye nikufuru unanipa mitihani kwa kila ninachokihitajia umasikini utamani nipate walau furaha ya muda hivi wewe umasikini ni nani hasa maana kama kupambana na pambana haswa ilituu nisiwe na urafiki na wewe ajabu unakuwa rafiki nisiye kutarajia mara zote unapigana na furaha yangu Aaah mungu ni kwanini ulinifanya masikini kiasi najiuliza hivi ni lipi hasa jukumu langu hapa duniani.. Eeh mungu umenileta ili niteseke? Nitaabike? Nidharirike? Na Kama sio yawaje sasa kila ninapo taka kupiga hatua unanirudisha nyuma yawaje kila ninapo pata tumaini jipya unaniziba macho nisione chochote. "
Aliongea maneno ya kulaumu na kukufuru huku machozi yakimtoka, tegemeo la pekee kwake alikuwa stellar hakuwa na budi zaidi ya kurejea kwake na kujipanga ilikupambana na maisha aliyonayo.
ITAENDELEA.........
USIKOSE SEHEMU YA 11 ....kiapo cha siri ulikuwa nami mwanadada ZAYNAB TALY Karibu tena katika kurasa yangu ya MKONO WANGU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: