Home → simulizi
→ KIAPO CHA SIRI
(Damu yangu haipotei)
MTUNZI : ZAYNABTALY
SEHEMU YA 09
ILIPOISHIA..................
"Tunashukuru mungu ila bado hali ya mwanao niyakujiliza tuu siku nzima ameshinda hana raha, mume wangu tungemsikiliza tuu stellar yupo radhi kesho kumleta hapa nyumbani. "
"Mimi Sina neno ila ahakikishe ananiletea mtu wa maana asije kututia aibu na kwakuwa wewe ndo umemtetea mimi Sina chakuongeza "
Wakakubaliana vyema na hatimaye Stellar akaambiwa amuite mpenzi wake nyumbani kwao ili aweze kuonana na wazazi wa stellar.
******SONGA NAYO ************
"Hallo Sam..? "
"Naam upo Salama...? " Aliuliza Sam ambaye alionekana kuwa na hofu zaidi huku asijue hatima ya kiumbe kilichopo ndani ya tumbo la Stellar.
"Ndio nipo Salama lakini nina habari njema kwako ".
"Habari Njema? "
"Ndio ".
"Eeh now Zipi hizo? ". Aliuliza huku akijiweka sawa kupokea Habari ambazo zilisemekana Ni nzuri kwake.
"Baba na mama wanahitajia kukuona ".
"Mmh wanataka kuniona..? "
"Ndio ".
"kwa wema lakini? ".Aliuliza Sam ambaye shaka yake ilikuwa kubwa mara dufu juu ya wito ule.
"je umewaeleza kama wewe ni mjamzito? ".
"Ndio kwa wema , ila kuhusu ujauzito awafahamu chochote ".
Moyo wake ukatulia hofu ikaanza kumpotea ghafra akajiona kama aliyemwagiwa maji kwa uwoga jasho lilimtoka, Umasikini alio nao ulimpa maswali mengi na kumpotezea tumaini la yeye kukubalika kuwa mkwe wa familia ile ya kitajiri.
"Sawa nitakuja ".Ndo likawa jibu lake na simu ikakatwa huku stellar akitawaliwa na furaha usiku kucha na kwa upande Sam nafsi yake kutawaliwa na unyonge huku akiwaza namna atakavyopokelewa na familia ile siku hiyo.
**********************************************
Wageni mbali mbali wenye hadhi na nyazifa za juu selikarini waliwasili eneo la tukio ilikuweza kushuhudia Hafla ile fupi ya utambulisho juu ya mtoto wa pekee wa mfanyabiashara yule maharufu Tanzania nzima.
"Stellar..? Siku hii nimuhimu mno kwako uwenda ukawa autambui hilo ila ni moja ya hatua muhimu Za kuyaendea maisha yako hasa katika Kipengele cha kuwa mama wa familia ".
yalikuwa maneno mazuri aliyokuwa akiambiwa na mama yake.
"Shika gauni hii ndo inayostahiki uivae siku ya leo ". Alimkabidhi kisha akaondoka zake. Lilikuwa gauni zuri la kifahari lililo tengenezwa vyema na material yenye thamani mno.
baada ya muda alikwisha valia gauni lile zuri na Kutoka nje ambapo kila aliyekuwepo mahali pale alikiri hakukuwa na mrembo miongoni mwao zaidi ya Stellar ambaye alikuwa akivutia katika kila jicho la wageni wale.
"Umependeza mno hivi ndivyo ambavyo mimi na baba yako tunapenda uyaishi maisha yako". Kisha akamshika mkono na kumuongoza mpaka alipo stahiki Kuwepo kimwana yule.
Kwa upande wa Sam alivalia T-shirt nyeusi na suluari ya kitambaa nyeusi pamoja na sendo zilizochoka kupita Kiasi. Akajijumuisha pamoja na wageni waalikwa asiwepo hata mmoja aliyegundua kuwa ndiye aliyekuwa mlengwa ndani ya Hafla ile.
Naye alikuwa miongoni mwa walioshuhudia uzuri wa msichana yule ambaye kwake uzuri wake ulizidi kuunyima moyo wake furaha mara mia zaidi .
Hatimaye ulifika wakati ambao Stellar alipewa kipaza sauti na kuombwa kumtambulisha mwanaume ambaye ndiye aliyehitajia awe mume wake.Ilikuwa ajabu kwa Muonekano wake na mwanaume aliyekawa akipanda jukwaani kwa ajili ya utambulisho ule.
Kila aliyekuwepo ndani ya ukumbi ule alipatwa na mshangao juu ya kile kilichokawa kinatokea. Hasira na ghazabu zikamfika MR SUDDEIS akajikuta akipanda jukwaani na kumvuta Sam ambaye alikuwa akijongea kwa uwoga akimkaribia Stellar iliaweze kumkumbatia kisha utambulisho ufate.
"Samahani kijana Sijaelewa vizuri wewe ndo Sam...? "
Aliuliza Mr SUDDEIS ambaye alionekana kuwa na hasira kupita Kiasi.
"Ndi...ndi.. Ndio mimi mzee ".Alijibu kwa kubaba ika huku akiwa ajiamini, akavutwa pembeni kisha akateremshwa katika jukwaa huku Kila aliyekuwepo mahali pale asielewe juu ya kile kilichokawa kinaendelea wakati ule.
"Niitie Stellar haraka ".Aliongea kwa ghazabu baada ya kufika katika chumba alichokikusudia Kiasi mama Stellar akafanya kama alivyoagizwa. Na Baada ya muda stellar pia alifika ndani ya chumba kile huku nyuma wakiwaachia maswali kibao wageni waalikwa ambao hawakuwa wakielewa juu ya kile kilichokawa kinatokea.
"Stellar huyu ndo mpuuzi ambaye umeamua kunitia aibu na kunidharirisha mbele ya umati ule kisa yeye sio..? "Aliuliza Mzee SUDDEIS.
"Hapana baba lakini huyu ndio mwanaume ambaye ananipenda na Kunijali na mimi Nina mpenda pia. "
"kweli mzee anachokiongea stellar nisahihi kabisa. "kabla hajamaliza alichokikusudia mkono wa mzee SUDDEIS ulikwisha tua katika shavu lake.
Mara akashituka ilikuwa ni ndoto kutahamiki ilikuwa saa nane usiku na simu yake ya mkononi iliita kutazama hakuwa Mwingne ni Stellar.
"Hallo upo sawa mpenzi? ".Aliuliza stellar baada tu yakuhakikisha simu yake ilikwisha pokelewa.
"Ndio Niko sawa Kuna tatizo? "Aliuliza Sam ambaye naye alikuwa ndani ya taharuki kubwa juu ya ndoto aliyo iota.
"Hapana ila nimeota ndoto mbaya mno sijui inamaanisha nini ".
ilikuwa ndoto yenye kufanana na ile ya Sam na zote ziliishia sehemu ile ya kupigwa kofi na mzee SUDDEIS.
"Mmh inamaana hii ndoto ".Alisema Sam kwa sauti ya chini ,ila stellar aliweza kumsikia.
"Maana gani? ".
"Sijajua bado ila achatulale kesho ndo itatueleza kila kitu."
Simu ilikatwa na kila mmoja akavuta Shuka na kujiegesha ilikusubiri kupambazuke. Hofu ilikuwa zaidi upande wa Sam huku akijiuliza maswali mengi ambayo aliyakosea majibu sahihi.
hatimaye Asubuhi iliwasili na purukushani za hapa na pale zilianza. Sam alikuwa bize kutafuta nguo itakayo mkaa vyema na kumfanya aonekane ni miongoni mwa watu wenye hadhi sawa na stellar ambaye bila shaka moyo wake ulijua siku hii ilikuwa ni siku adhimu mno kwake nasiku ambaye ingempa jibu moja Kati ya mawili kama ndio au hapana.
ITAENDELEA.....
COMMENT NA LIKE zenu ni vitu muhimu Sana kwangu Msisahau kunikosoa ninapo kosea mimi pia binadamu karibuni Sana Tukutane sehemu ijayo wapendwa wangu mlikuwa nami ZAYNABTALY katika kurasa hii ya simulizi......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: