KIAPO CHA SIRI (Damu yangu haipotei) MTUNZI : ZAYNABTALY SEHEMU YA 08 Ilipoishia....... "Sikia stellar hiki nikiumbe changu chochote utakacho fanya ila jua hana hatia hata kidogo Usije ukamdhuru ninacho Jua masikini hana lake na mimi ni miongoni mwao najua ipo siku utaniacha mahali hapa nikitapa tapa kwenu munauwezo na hadhi yangu Wala wazazi wako hawato kibali mbali na hilo umefanya makosa makubwa mno kutoroka kwenu bila kuwaeleza wewe ni mjamzito na kuonyesha Msimamo wako ,kuja kwako kuishi kwangu utanipa shaka mimi pia ambaye sina ndugu Wala jamaa na kwavyovyote kizazi changu kinaweza kupotea. " ****** SONGA NAYO ************ Alikuwa maneno yenye ujumbe mzito mno ambao ilimbidi Stellar kuelewa vilivyo na kuufanyia kazi. "leo utalala hapa kwangu maana ni usiku Sana ila kesho itakubidi urejee kwa wazazi na kuwaonyesha Msimamo wako ". "Sawa mpenzi nimekuelewa". Walikumbatiana kisha wakajilaza kitandani usiku ulikuwa mrefu mno kwa Stellar ambaye kwa upande wake Bado hakukubaliana na yeye kurudi nyumbani ila hakuwa na jinsi zaidi ya yeye kurudi nyumbani. Asubuhi ilipofika Alijiandaa vyema na kukusanya mizigo yake na taratibu akaanza kuondoka. "Stellar..?, Sina maana ya kuwa sikupendi ama sifurahii uwepo wako nyumbani kwangu wewe ni mwanamke wa pekee Sana kuwahi kutokea umeweza nivumilia katika kila hali wakati wapo walio niacha kwa manyanyaso na matusi wasijali utu wangu ila kila linapotokea lakuniumiza napata hisia Kali Za kuchukia kwanini nilizaliwa masikini kwanini sikiwaona wazazi wangu ila nahitaji tuape Stellar Kama wanandoa wanavyoapa ila kiapo Chetu ni cha siri. " "Sam naelewa nini unamaanisha ila Sina jinsi achatuu nirudi nyumbani".Aliongea kwa huzuni huku akilipapasa tumbo lake ambalo ndani yake kulikuwa na kiumbe kichanga ambacho bado hata maungo yake hayakujitengeneza vizuri ilikujua Kama kiumbe kilichopo ni jinsia gani. "Stellar inabidi unipe Alama kupitia meno yako alama ambayo haitokaa ifutike katika maisha yangu na wewe pia nikupatie kisha kiapo Chetu kisimame kimatamshi ambayo haitokuwa rahisi kwa mmoja wetu kukikiuka kiapo Hiko." " sawa kwangu Sina kipingamizi katika hilo". kila mmoja akamuweka mwenzie alama ile ya meno katika shingo kisha kiapo cha matamshi . "Stellar naapa kukitetea kiumbe kilichopo katika tumbo lako mpaka pale mungu atakapo amua kunipoteza katika namna ambayo nitafeli kukipigania napo sio pengine nikifo. " "Sam naapa kukitetea kiumbe kilichopo katika tumbo langu mpaka pale mungu atakapo amua kunipoteza katika namna ambayo nitafeli kukipigania napo sio pengine ni kifo. " "Nanisulubiwe katika namna yoyote huku nikiwa radhi iwapo nitakiuka kiapo hiki" "Nanisulubiwe katika namna yoyote huku nikiwa radhi iwapo nitakiuka kiapo hiki ". Naam wakawa ni wenye kujifunga ndani ya kiapo kile huku kila mmoja wao akiwa na tumaini la kutoenda kinyume na kiapo kile. Stellar alifunga safari tena mpaka nyumbani kwao ambako alijitahidi asiweze kuonekana na yoyote wakati anaingia . *********************************************** "Baba stellar unajua alichokiongea stellar jana kinaukweli ndani yake ". "Kipi..? " aliuliza mzee SUDDEIS baada yakuinuka kitandani na kutaka kuingia maliwatoni ilikuweza kujiandaa kwenda kazini. "Hatuwezi muuza mtoto hivyo na yeye anahaki yakusikilizwa juu ya chaguo lake ".Alimtetea binti yake ambaye kwa Kiasi flani alihisi kumkosea. " hivi mama stellar huyo mwanaume anaye sema yuko naye wewe amekwisha wahi kukuletea hata siku moja hapa ukamuona..? "alimuuliza. "Hapana " "Sasa mnataka niwasikilize nini kama kweli huyo mwanaume angekuwa anampenda binti yangu basi angeshakuja kujitambulisha ". Akamaliza kwa ukali kisha akaingia maliwatoni kujiandaa na baada ya muda alielekea panapo mahali pakumuingizia kipato chake cha kila siku. Huzuni na majonzi yalitawala upande wa Stellar ambaye ujauzito alio nao ulizidi kumnyima raha na kiapo cha kumsulubu iwapo atakiuka walichokubaliana yeye na Sam. Akiwa katika hali ile ambayo ilikuwa ikimtesa na kumsulubu nafsi ghafra mlango wa chumbani kwake ulifunguliwa, na mama yake akaingia haraka akajifuta machozi na kumtazama mama yake kwa macho makamu na yaukaka mavu. "Kulia sio suluhisho binti yangu, nimejaribu kuongea na baba yako kuhusu swala hili imekuwa ngumu kunielewa hasa alipo nihoji kama niliwahi kumuona huyo mwanaume ambaye wewe unataka akuoe." "mama kama kumuona tuu mimi nitamleta hapa nyumbani mumuone ilo sio tatizo atakuja hata mkitaka leo. " "sasa sikiliza subiri baba yako arudi tuongee naye akikubali sawa utamwambia kesho aje kujitambulisha ". Yalikuwa maneno yaliyompa tena furaha stellar akajifuta machozi na kuendelea na shughuri zake za Kawaida. Jioni ilipofika mama Stellar alifanya hima na kutenga muda wakuongea na mume wake. Huku stellar akisali kwa maombi baba yake akubaliane na kile atakachoelezwa na mama yake. "Umeshinda je mume wangu..? " "Namshukuru mungu sijui nyie hapa nyumbani? ". "Tunashukuru mungu ila bado hali ya mwanao niyakujiliza tuu siku nzima ameshinda hana raha, mume wangu tungemsikiliza tuu stellar yupo radhi kesho kumleta hapa nyumbani. " "Mimi Sina neno ila ahakikishe ananiletea mtu wa maana asije kututia aibu na kwakuwa wewe ndo umemtetea mimi Sina chakuongeza " Wakakubaliana vyema na hatimaye Stellar akaambiwa amuite mpenzi wake nyumbani kwao ili aweze kuonana na wazazi wa stellar. Itaendelea......... Acha tuone sehemu ya tisa kama Sam ataenda kwa mzee SUDDEIS na je nini kitafata baada ya yeye kufika katika familia ile kwa ajili ya utambulisho....... Ilikuwa nami mwanadada ZAYNABTALY hapa hapa mkono wangu....

at 4:21 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top