Home → simulizi
→ KIAPO CHA SIRI
(Damu yangu haipotei)
MTUNZI : ZAYNABTALY
SEHEMU YA 07.
ILIPOISHIA......
.Aliongea kwa uchungu huku machozi yakimiminika Kama mvua itokavyo angani huku akiinuka kwa hasira kuelekea alipo kawa baba yake ambapo alikuta Tayari wageni wale walikwisha ondoka.
"Baba kwanini unataka kuniuza Kama gunia la viazi kwani mimi sio mwanao..?".Lilikuwa ni swali zito ambalo lilimtoka stellar bila kukusudia ila haikuwa na namna zaidi ya kulijibu tuu.
********* SONGA NAYO *******
"Sikiliza binti yangu Elly nikijana mzuri na mwenye uwezo mkubwa wa kifedha msomi Kama wewe mimi sikuona aja ya kuanza kukuuliza chochote kuhusu hilo. "Lilikuwa Nijibu ambalo bado halikukidhi haja ya moyo wake Kiasi aweze kuelewa lengo na nia yao hasa.
"Baba angu kipenzi mapenzi sio pesa zake alizonazo ni moyo wa mtu hata kama yeye ananipenda lakini mimi simpendi naombeni mumrejeshee kila alichokitoa kwa ajili yangu mimi ninaye ambaye nina mpenda na yeye ananipenda na ndo atakaye nioa ".
Alijitoa kwa maneno ya kiburi mbele ya wazazi wake akiipinga ndoa yake yeye na Elly mwanaume ambaye hajawahi hata kumuona kwa sura.
Kwa usiku ule hakuweza kulala kwa amani ulipo fika saa tisa na usiku ikiwa watu wote wamelala akapatwa na wazo haraka aliamka Kutoka kitandani na kukusanya baadhi ya nguo na vitu vyake muhimu na kuviweka katika begi lake dogo ambalo alihakikisha awezi kupata tabu wakati wakulikokota kwenda nalo popote.
Kisha akajiandaa na yeye mpaka kutimia saa saba na nusu alikuwa tayari kwa safari aliyokawa ameikusudia.
Taratibu alijikongonja kwa kunyata ili asiweze kuonekana na yeyote mpaka Alipofika baranarani na kuosubiri usafiri baada ya dakika kadhaa aliziona taa zikiwaka huku zikiwa katika Kati ya barabara kwa mwendo wa kasi akapunga mkono na hatimaye aliyekuwa na usafiri ule alisimama alikuwa dereva boda boda na boda boda yake akirudi nyumbani kujipumzisha.
"Samahani kaka angu unaweza kunipeleka vingunguti..? "
"Usiku huu? ".Alihoji yule dereva huku akiangalia saa yake ya mkononi ambaye kwa sasa ilionyesha saa nane kamili japo kwa jiji la Dar ilikuwa bado ni kama mchana maana watu walipita na wengine walionekana bize na shughuri Zao za hapa na pale.
"Unajua vingunguti ni mbali Sana na mimi hapa nilikuwa naelekea kwangu kupumzika? ".
"Nalijua hilo kaka angu ila nisaidie nimesimama Sana hapa nitakupa Kiasi chochote cha pesa unachotaka ".
Hatimaye yule kijana alikubali na safari ya kwenda vingunguti ikaanza na baada ya muda kidogo walikwisha fika sehemu husika stellar alishuka kwenye piki piki na kuelekea palipo mahali husika alipo pategemea.
"Saa tisa saizi nafikiri nitakuwa namsumbua sana ilanitafanyaje"Alijisemea mwenyewe huku akiukabili mlango kisha akagonga iliaweze kufunguliwa akagonga mpaka alipo itikiwa kwa sauti Kutoka usingizini.
"Na kuja... "Baada ya muda kidogo mlango ulifunguliwa hakuwa mwingine Sam ndiye aliyefungua mlango.
"Kulikoni Stellar...?"Ndio swali pekee kabla ya salamu alilo weza kumuuliza.
"Sam achatuu ".
"Niache nini wakati unakuja kwangu na mabegi pia inaonyesha hauko sawa? "Aliuliza Sam huku akijisogeza karibu na mwanadada yule ilikujua ni kwanamna na jinsi gani angeweza kumsaidia.
"Sam mpenzi nimetoroka nyumbani "
"Umetoroka...? ".
"Ndio nimetoroka Sam siwezi kuishi na watu wanaotaka kuidhurumu nafsi yangu Sam ".
"Embu nieleze vizuri una nini Stellar ckuelewi ni nani anataka kuidhurumu nafsi yako....? ".
"Sam baba na mama wamenitafutia Mchumba na wanataka kuniozesha na kila kitu kipotayari bado ndoa tuu.. ".
"Nini..?" aliuliza kwa hamaki na kusimama huku akionekana kutafakari jambo.
"yawaje utolewe mahari na posa leo ndo uniambie ulikuwa wapi kunishirikisha siku zote hizo leo ndo uje kwangu na mabegi..?"
"Uwezi kuamini Sam mimi mwenyew nilikuwa sijui chochote kile kama Juzi tulivyokubaliana nikapanga leo nimeambiwa mama kuhusu wewe ili uje ujitambulishe nyumbani na harakati Za harusi zifate lakini nashangaa jana mama ananifata chumbani akinieleza juu ya posa na mahali ambayo baba aliiipokea Kutoka kwa kijana ambaye inasemekana ni mtoto wa mfanyabiashara mwenzie ila mimi sikuwa nikifahamu chochote ".
Likazuka zogo huku kukiwa hakuna maelewano baina yao hatimaye walifikia muafaka.
"Sam nakupenda Sana na ndio maana nipo hapa leo nina kiumbe chako tumboni ni vipi kitaishi na mtu ambaye sie baba yake naomba hifadhi yako mahali hapa kama ulivyonipa hifadhi ndani ya moyo wako."
"Sawa ila Stellar lazima tule kiapo cha siri Damu yangu aiwezi kupotea " .
"Najua sama ila nikiapo gani hiko cha siri Sam ?".
"Sikia stellar hiki nikiumbe changu chochote utakacho fanya ila jua hana hatia hata kidogo Usije ukamdhuru ninacho Jua masikini hana lake na mimi ni miongoni mwao najua ipo siku utaniacha mahali hapa nikitapa tapa kwenu munauwezo na hadhi yangu Wala wazazi wako hawato kibali mbali na hilo umefanya makosa makubwa mno kutoroka kwenu bila kuwaeleza wewe ni mjamzito na kuonyesha Msimamo wako ,kuja kwako kuishi kwangu utanipa shaka mimi pia ambaye sina ndugu Wala jamaa na kwavyovyote kizazi changu kinaweza kupotea. "
ITAENDELEA.....
KIAPO CHA SIRI Ulikuwa nami mwanadada ZAYNABTALY katika sehemu hii ya saba Tukutane Tena katika sehemu ya nane ambapo taratibu tunaenda kujua kwa undani zaidi juu ya kiapo hiki cha siri... LIKE & COMMENT unipe nguvu katika hili...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: