KIAPO CHA SIRI (damu yangu haipotei) MTUNZI : ZAYNABTALY SEHEMU YA 06. ilipoishia......... Ikawa kawaida yao kutoka out mara kwa mara kwa ajili kutalii jiji huku akijitahidi kuongeza furaha ya Sam kwa asilimia kadhaa huku kwa upande wake na yeye akifuta kumbukumbu ya maumivu ambayo ilimtesa kwa muda sasa. **********SONGA NAYO************** "Sam...?".Alimuita siku moja wakiwa pembezoni mwa fukwe za bahari wakiangalia uwezo wa mungu juu ya mapambo na vioja alivyotuumbia walimwengu kwani kwani lilikuwa pendekezo pekee na lenye kumpa stellar furaha. "Naam... ". "Unajua maisha ni safari ndefu Sana tena ni safari yenye kuleta maajabu na vioja vya kila namna utajikuta leo ukicheka na kesho ukiumia kulingana na safari hiyo hiyo ambayo uwenda kwako leo ikawa msiba lakini nyumba ya jirani ikawa sherehe, nafikiri tumepitia mengi mno sio wewe peke yako hata mimi pia na tumepata wasaa wakuirejesha furaha yetu kupitia mambo mbali mbali ".Akasimama kidogo akiangalia umakini wa Sam juu ya kile alichokawa akimueleza kisha akamsogelea karibu na kuhakikisha macho yake na Sam yalikuwa yakitazamana bara bara. "Nimesafiri safari zaidi ya mia za furaha na majonzi katika maisha yangu lakini natamani hii iwe safari yangu ya mwisho nikiwa na wewe nimeteswa Sana na hisia hizi pasi na kuzifikisha kwa muhusika nikihofia haukuwa wakati sahihi kufanya hivyo". Akajikongoja na kuushika mkono wa Sam wakulia na kuuweka katikati ya mikono yake miwili. "wewe ni rafiki mwema ambaye umeweza kuirejesha furaha yangu ambayo hukuwahi kutokea wa kuipigania kwa muda sasa, sio familia ndugu hata marafiki zangu wanaamani kujua chimbuko la furaha yangu nalo sio lingine ni wewe Sam., Nimehitajia nikupe zawadi itakayo simama na wewe milele ikiwa kama kumbukumbu ya asante kwa kuirejesha tena furaha yangu lakini nimeikosa naomba nikukabidhi moyo wangu, nahitaji kuwa mama bora wa familia yako na mke bora WA ndoto zako nimevumilia nimeshindwa Sam nakupenda".. Ndio maneno yaliyo zikutanisha nyoyo mbili baina ya stellar na Sam na wote wakajikuta wakiingia katika upofu wa mapenzi huku kila mmoja wao akijitoa kubadilisha maisha ya mwenzie kila siku iliyoitwa leo. Stellar alizidi kuwa hasikii Wala kuona chochote kile kuhusu Sam na kuona maisha yake yalibadilika na kuwa mwenye furaha siku zote na hatimaye Stellar akapata ujauzito ukawa wakati sahihi mno kwake ilikuweza kuijuza familia kama ulikuwa ni muda wake muafaka wa yeye kuitwa mke kisha mama wa familia. Jioni moja baada ya kujigundua Kama alikua mjamzito Stellar alitoka kwa furaha akielekea nyumbani . Ajabu wakati yeye anamikakati kamilifu juu ya mipango yake ya kuingia katika ndoa kwani ilikuwa nikitambo sasa tangu kumaliza elimu yake ya chuo kikuu na kuajiliwa. Alipofika maeneo ya nyumbani alipokelewa na ugeni ,ugeni ambao haukuwa wa Kawaida nyumbani kwao. Msururu wa magari ya kifahari nyumbani kwao na wazee watatu pamoja na vijana wanne walio kawa wameketi sebuleni wakiongea na baba yake mzee SUDDEIS ulimuonyesha haukuwa ugeni wa kawaida. "Stellar..?". "Abee..?"alisikia sauti ya mama yake ikimuita na yeye kuitika baada tuu ya yeye Kufunga mlango wake wa chumbani. Baada ya muda mama stellar alikwisha ingia katika chumba cha binti yake na kumkaribia pale alipo keti. "Binti yangu Sidhani kama Kuna ambacho haujakielewa mpaka sasa? ". "Unamaana gani mama ?".Akauliza stellar ilikupata maana halisi ya maneno yale ya mama yake ambaye siku ile alionyesha kujawa na busara kuliko siku zote. "Huu ugeni ni wako binti yangu. ". "Wangu kivipi mama Mbona Bado sielewi?". "Yaani wamekuja kuleta barua ya posa tuu pamoja na mahali maana kila kitu baba ako alikwisha ongea nao kabla japo hatuku kushirikisha ila Ni kwasababu hatuku taka watu wajue kuhusu hili hata wewe ilibidi iwe suprize kwako." "mama hakuna suprise ya hivi mama yaani mnapokea barua ya posa mpaka mahali bila hata kunishirikisha Mama mnaniozesha au kuniuza Kama bidhaa...? Maana bidhaa iwapo dukani hata iwe imezoea vipi mandhari ya pale itaondoka hata kama isipo ridhia mama mimi nimewakosea nini lakini? ". .Aliongea kwa uchungu huku machozi yakimiminika Kama mvua itokavyo angani huku akiinuka kwa hasira kuelekea alipo kawa baba yake ambapo alikuta Tayari wageni wale walikwisha ondoka. "Baba kwanini unataka kuniuza Kama gunia la viazi kwani mimi sio mwanao..?".Lilikuwa ni swali zito ambalo lilimtoka stellar bila kukusudia ila haikuwa na namna zaidi ya kulijibu tuu. ITAENDELEA....... karibu tena tuone nikipi kinachojiri ndani ya kurasa hii maridhawa ilikupata uhondo halisi wa simulizi zenye kukonga nyoyo ulikuwa nami mwanadada mchakalikaji ZAYNABTALY karibu tena sehemu ijayo. COMMENT & LIKE umuhimu Sana ilikunipa nguvu....

at 4:21 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top