KIAPO CHA SIRI (Damu yangu haipotei) MTUNZI : ZAYNABTALY 0712272972 /0625756953 SEHEMU YA 05. Ilipoishia...... Alimaliza kumueleza kuhusu yeye na familia yake huku akijiweka sawa kuyasikiliza kwa upande wa Sam. ********SONGA NAYO ******** "Stellar unajua hata nikisema nieleze kama nilikuwa au niliwahi kuwa na ndugu sijui kama nitakuwa napatia sana katika hilo mimi nilijikuta nikiishi mwenyewe tangu utoto wangu. Sija bahatika kumjua baba,mama wala ndugu yoyote wa karibu yangu wa kunishika mkono kwa ufupi historia kuihusu familia yangu bado sijaipata na hata nikisema niitafute sina pakuanzia kusema naweza nikaijua walau robo kuwa mimi ni nani, wakati na kuwa niliwasikia watu wakiniita Sam sikujua lilitokea wapi ilijina ila ndo likawa jina langu na mpaka leo ndo jina langu. Hapo awalinilikuwa nikiishi tuu mitaani kama hawa watoto wengine wa mitaani wanavyoishi kwa kuokota chakula majalalani na kulala maeneo ya wazi unajua sisi tukiwa katika hali kama ile ndipo jamii inayotuzunguka inapopoteza tumani la kutuona sisi ni watu kama wao, wengi hututoa utu wetu wote na kutuvisha vazi la unyama kama ni vibaka watu wasio faa na wengine ni majambazi wanaozuga tuu mitaani”. Aliweka nukta kushushapumzi huku akijiandaa kujikazakiume kuelezeamaisha ambayo yalimkabili katika kipindi chote mpaka pale alipofikia, Ilionyesha haikuwa kazi rahisi na hata maisha aliyokawa anaishi hayakuwa yakimpa haata tone la furaha, akaendelea. “Jioni moja nikiwa nimejilaza pembezoni mwa magari yaliyowekwa parking nilimuona kijana mmoja mtanashati akipita karibu yangu huku akiongea na simu siku pata kufahamu hasa kitu gani alikuwa akikiongelea ila ghafra likatoka kundi la vibaka na kumvamia kisha wakampola simu na kutaka kupekua mifuko yake ya suluari, tukio lile liliniumiza siku taka kabisa kuliona likifanyika nikainuka na kujitolea kupambana nao iliwasiendelee kumzuru yule kijana na hatimaye nilifanikiwa. “Daah asante sana”.Alinishukuru baada ya kumrejeshea baadhi ya vitu vyake ambavyo viliachwa pale chini baada ya purukushani zile.Siku mjibu kitu nikarudi balipo maboxi yangu ambayo niliyapanga vizuri sakafuni iliyasiweze kupitisha baridi kisha nikajilaza. “Samahani bro tunaweza kuongea?”Aliongea yule kijana ambaye alionekana kupata maumivu mkali baada ya kukabwa na wale vibaka. “Ongea nakusikiliza”. Namimi nikajiweka tayari kumsikiliza. “samahani najisikia vibaya sana na nina mumivu mkali mno kwenye mguu wangu siwezi kufika popote naomba unipe msaada wa kunifikisha kwangu”. Lilikuwa jambo jipya na geni kwangu eti ni mpeleke kwake mi nitapajua vipi na hata hivyo maskani yangu nitaiyacha na nani?hivi nikiondoka tuu sindo huku nyuma wahuni watakuja kufanya yao… Nikajikuta moyo wa kutoa msaada ukiwa na nguvu zaidi kuliko nafsi ile yenye maswali mengi na kujali sana upande wangu. Nilimuinua yule kijana pale alipoketi na kumsaidia kumkongoja mpaka kufika sehemu aliyonielekeza ndo alipokawa akiishi.Tulipofika nilimuhakikisha alikuwa na salama na mimi sikuwana muda tena wakupoteza nikapanga kuondoka kurudi katika maskani yangu. “Nafikiri upo salama nilikuwa naomba niende?”. “Hapana uwezi kwenda kule saizi ni usiku sana nakuomba upumzike hapa kesho asubuhi utaenda”. Aliongea yule kijana ambaye hali yake haikuwa nzuri sana kutokana na kipigo alichokiambulia usiku ule.Sikuwa mbishi nilifanya kama alivyoniomba nifanye tulilala na kisha asubuhi niliamka vyema nikisikilizia hali yake iliniweze kuondoka. “Oii mi nilikuwa na wahi zangu maskani?”nilimuamsha baada ya kumsubiri muda mrefu pasi na matumaini yoyote ya yeye kuamka nilipo mgusa mwili wake ulikuwa na joto kali mno,hakuwa akiweza kuongea chochote kila alipokawa amepigwa palivimba kupita kiasi kwa nafsi yangu haikuwa rahisi kunifanya nimuache niondoke nikamkongoja na kutafuta usafiri kisha mpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu. Hatimaye nilifanikiwa kufanya hivyo na kwa muda wasiku mbili afya yake ilikuwa imara kisha tukaruhusiwa kurudi nyumbani. Hapo ndipo maisha yangu mapya yalipo anza nikawa nikiishi naye pale nyumbani kwake historia za maisha yetu haziku tofautiana sana hata yeye alikuwa akiishi pasi na kujua wazazi wake. Hakuchukua muda alifariki dunia kwani ilisemekana aliumia ndani kwa ndani kiasi kusababisha damu kuvilia ndani pasi na sisi kujua. Nilimzika salama rafiki yangu kipenzi aliyeniamini katika kipindi ambacho binadamu walikuwa hawana thamani kulingana na hadhi au mavazi watakayo ya vaa akanipa hifadhi na tukaishi kama ndugu tukicheka na kufurahi pamoja. Vitimbi vya majirani na watu wakaribu vikaanza wapo walio kaniita mwizi kunitukana na kunizihaki pesa ziliponiishia nikawa sina egemeo madhubuti nikaanza kutanga tanga tena mitaani nikitafuta pesa. Tuhuma nyingi za wizi zikawa tandiko la mwili wangu huku nikijitahidi kupambana na maisha nipate walau kodi ya nyumba na chakula, nikajikuta nikiingia katika mchezo mbaya wakuwalizisha wake za watu huku wakinilipia kodi ya nyumba na kunipa pesaya matumizi na hivyo ndivyo ambavyo maisha yangu yalikuwa yakiendeshwa mpaka siku ile tulipokutana na kukuamuru unipeleke vingunguti na kunikuta tena nikigombana na mama mwenye nyumba kuhusu pango yake ndio maisha halisi ambayo napambana nayo kila leo iliniweze kuiyona kesho yangu.” Chozi lilimtoka kwa uchungu stellar kwani siku zote akiishi pasi na kujua kama walikuwepo watu wenye shida Kiasi kile akaingiwa na roho ya huruma juu ya Sam na kutamani angelikuwa na ufutio na kufuta kumbukumbu ile ambayo alikuwa ikimtesa Sam kila kukicha lakini haikuwa rahisi. Akajikuta akijitahidi kuwa rafiki mwema na kuhakikisha anaipoteza kumbukumbu yote yenye kumuumiza moyo rafiki yake yule na kumfanya mwenye furaha siku zote. Ikawa kawaida yao kutoka out mara kwa mara kwa ajili kutalii jiji huku akijitahidi kuongeza furaha ya Sam kwa asilimia kadhaa huku kwa upande wake na yeye akifuta kumbukumbu ya maumivu ambayo ilimtesa kwa muda sasa. ITAENDELEA....... Usisahau LIKE na COMMENT yako inanipa nguvu nizidi kuleta uhondo ndani ya group hii KIAPO CHA SIRI Bado story ni ndefu usikae mbali na page hii ulikuwa nami mwanadada ZAYNABTALY wataalifu na wengine wakaribie ndani ya MKONO WANGU PAGE.......

at 4:21 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top