KIAPO CHA SIRI (Damu yangu haipotei) Mtunzi : ZAYNABTALY 0625756953 SEHEMU YA 4....... Ilipoishia...... " We Koma wewe mimi sio mama yako nataka changu ". Yalikuwa maneno yaukali ambayo yalimchoma moyo na kumfanya akose cha kukiongea mbele ya mama yule ambaye jaziba zake aliamini zingetulia kwa pesa tuu na sio vinginevyo. *******SONGA NAYO******** Wakati akiwa anahaha asijue chakumpa yule mama mara alisikia sauti ambayo aliwahi kuisikia siku zilizo pita. "Habari zenu..? " ilikuwa nisauti nzuri yenye kupendeza Kutoka kwa Stellar. "Salama ". Aliitikia huku akiwa hamkumbuki mwanadada yule aliwahi kumuona wapi Wala kuisikia sauti yake. "vipi Mbona hapa Kuna tatizo? ".aliuliza ilikuona namna atakavyoweza kusolve tatizo lile. "yaani Dada angu acha tuu ". Kabla ya yule kijana kutia neno lolote mara yule bibi akadakia. "Kama wewe ndo Hawala yake haya msaidie kulipa pango sasa sio kukitumia tuu chumba changu na kukiacha hata gest wanalipa pango eeeh... ". Maneno ambayo yalimfanya stellar staajabu kwa yale maneno yaliyomshukia ila hakuwa na jinsi akaingiza mkono wake katika pochi yake kisha akatoa noti za elfu kumi na kuanza kuhesabu. Kisha akampatia yule mama "nimekulipia na miezi miwili ijayo ". "Ooh asante Sana Dada angu nashukuru Sana kwa msaada wako ". "Usijali ". "naushukuru huyu malaya wako Kaja kukupa msaada leo saa sivyo pangechimbika hapa leo maana habari zako zote ninazo mpuuzi wewe kukicha kuleta wasichana wa ajabu ajabu nyumbani kwangu na sijui hata utakuwa lini maana hela yenyewe huna hae hohe tuu kama mimi ila msumbufu mtaa mzima huu wanakujua wewe kwa jinsi ulivyokicheche na mwizi na sikia hata juzi ukitoka kuuliwa tandika lakini Mi hata sijali hayo muhimu umenipa pesa yangu " Yalikuwa maneno ya mama mwenye nyumba huku taratibu akikanyaga hatua kuondoka eneo lile. "Daah niwie radhi tafadhali maana bila mimi yote haya Sidhani kama yangekusulubu. "Aliongea yule kijana mwenye sauti ya upole ambayo ilienda sambamba na sura yake. Macho yake ya aibu yasiyo na hata chembe ya ukaidi ndio yaliyokuwa yakitalii kwa kuibia juu ya mwanadada yule aliyemsaidia kutoka katika sakata lile huku machozi yakimlenga katika macho yake juu ya lile tukio la muda mfupi lililotokea. "usijali ila nilikuwa naomba wasaa wakuongea na wewe kwa uchache? ". "Aah usijali Karibu ndani ". "Naitwa Stellar "alijitambulisha baada ya kuingia ndani ya chumba cha kijana yule kilicho pambwa na kitanda kimoja kikubwa cha Ukubwa wa tano kwa sita, kiti cha plastiki, meza ndogo iliyopangwa vyombo vichache chini yake. kwa chini kulikuwa na jiko la mafuta pamoja na sufuria mbili chafu. Baada ya kukamilisha kutembeza macho yake ndani ya chumba kile sasa macho yake yalikutana na macho ya yule mvulana. "Mi naitwa Sam Karibu kwangu". "Asante, sijui unanikumbuka..? "aliuliza ilikuweza kutambua uhai wakumbukumbu juu ya tukio lile la kukutwa ndani ya gari la watu na kuhitajia msaada. "Hapana Labda unikumbushe tulionana wapi ". "any way kunasiku nilikukuta katika gari yangu ukaniomba msaada Nikulete mpaka mitaa hii. "Ooh Nimekukumbuka ila Samahani Sana kwa lile tukio sikuwa na jinsi ". Aliongea huku akipiga goti kwa nidhamu kumshukuru mwanadada yule ambaye kwa mara ya pili sasa alikuwa msaada mkubwa mno kwake. Baada ya muda wakautengeza urafiki ambao chanzo chake ilikuwa ngumu mno kwa watu kutambua. Uwepo wa Sam Ulifanya furaha ya stellar kuongezeka mara dufu kila leo na hasa pale alipokawa akiona mipango yake ya kila siku ikiwa na director katika kila hatua aliyokawa akiipiga. Jioni moja walipanga Kutoka ilikuweza kutalii manzari ya jiji kwa Masaa kadhaa kisha kila mtu angerejea kujipumzisha. Muda wa miadi ukifika na kila mmoja aliwasili kwa wakati huku nafsi ya stellar ikiwa na furaha zaidi kuwa Karibu na Sam kila pale anapohitaji. "Sam...? ".Alimuita jina lake ilikumpa utayari wakumsikiliza juu ya nini ambacho stellar alikuwa akihitaji kukiongea ,Ilikuwa ni baada ya kimya cha muda mrefu ambacho kilitawala baina ya watu wale wawili huku kila mtu akiwa busy kutazama mazingira ya sehemu ile. "Naam... ". "Tumejuana kwa bahati mbaya Sana uwenda bila mimi Kuwepo eneo lile la tukio siku ile basi ingekuwa bahati mbaya zaidi kwa wako lakini pia sitamani iwe bahati mbaya zaidi kuishi na rafiki nisiyejua hata historia yake kwa ufupi ya hapo awali mpaka sasa, Kwetu mimi ndo mtoto wapekee wakike baba angu mzee SUDDEIS anao uwezo wakifedha Kiasi Fulani ameunga ubia na baadhi ya makampuni makubwa hapa nchini mbali na hivyo yeye sio mtu wakutulia Sana nyumbani na mama yangu ni mama tuu wanyumbani tunaishi Mbezi siku moja nitakuchukua na kukupeleka kwetu ukapaone". Alimaliza kumueleza kuhusu yeye na familia yake huku akijiweka sawa kuyasikiliza kwa upande wa Sam. Itaendelea...... Naam hiyo nisehemu ya nne usikae mbali na sehemu ya tano inakuja hivi punde huyu ni Stellar usikose sehemu ijayo iliuweze kumjua Sam ni nani hasa na hiki kiapo ni cha Nani na iweje Damu yangu haipotei.... Ulikuwa nami mwanadada ZAYNABTALY usisahau kulike na kushusha comments ya nguvu katika page hii iliniweze kuendelea kukuletea simulizi maridhawa kupitia mkono wangu page........

at 4:20 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top