KIAPO CHA SIRI (damu yangu haipotei) mtunzi :ZAYNABTALY 0625756953 SEHEMU YA 03 Ilipoishia....... Alikuwa kijana Mpole, mnyenyekevu na mtanashati ambaye mvuto wasura yake ulifichwa na ugumu wa maisha aliyokuwa akipitia kwa kipindi kile.stellar alibaki kumsindikiza kwa macho mpaka alipo potelea gizani naye akawasha gari na kurejea nyumbani. **********SONGA NAYO *********** Ugumu wa maisha ndio uliokuwa ukimfanya kuwa dhaifu kila kukicha mbali na upole wake sasa aliendea kuwa zoba kwa kuikosa nafsi ya utetezi kwake. Uhuni ndio ikawa stara yake kwa kuwaridhisha wake za watu kimwili kisha wakamzawadia Kiasi kadhaa cha pesa na kumfanya arudi katika hadhi yake ya ubinadamu. Moyo wake uliwahi kupenda mara moja na mara Zingine zote ukawa niwenye kutamani na kujichomeka vilivyo ilikupoza machungu ya maumivu aliyokawa akiyapata awali. Yote hayakuwa na sababu maalum zaidi ya umasikini pekee ndio uliosimama Kama chachu na chanzo cha kila kilichomtesa. " Hivi Sam kila siku nikuambie Jambo moja mwanamke Matunzo wewe ulitaka nani anihudumie wewe uje unitumie tuu? ". "Sio maana yangu nasra nielewe basi na hali yangu napambana nakupa utakacho mwenyewe nashinda njaa napo unaniona sikujali..? Tazama na hali yangu basi ningalikuwa na uwezo ningekupa chochote utakacho ila kwasasa Sina mapenzi Nivumilie baada ya wiki mbili nitakuwa Nishapata hiyo pesa. " " Khaaa wiki mbili tena wakati mimi nimekuambia kesho kutwa ndo shughuri yenyewe Sam Unajua usinitanie ". Aliongea kwa jaziba kisha Akakusanya vilago vyake na kuanza kuondoka kwa hasira." sasa mama unaenda wapi mpenzi Njoo tuongee basi" "sitaki naomba uniache ". Ilikuwa kumbukumbu ya maumivu iliyomjia akiwa kajilaza kitandani baada ya kunusurika kufa katika purukushani Zile za kimbiza mwizi. "Nasra nakukumbuka wewe ndo ulikuwa mfariji wangu kwenye joto ukawa upepo wangu mzuri na kwenye baridi ukawa nguo nzito ya kunipa joto na hata pale nilipo tingwa na mambo dunia ilipo nipa kisogo na kila mtu kunichukia wewe ndo ukawa mtu pekee uliyelijali chozi langu sasa nini kime kukumba nasra wangu nini kimekupata au ndo ulichoka kuivumilia hali yangu, ukachoka kutukanwa kwa ajili yangu nasra umepatwa na nini mama..? ". Aliendelea kutoa maneno ya ulalamishi huku akigaragara kitandani peke yake asijue wapi pakushika.Kweli ulipita wakati tangu alipoondoka nasra kwa ghazabu na kumuacha Sam akiishi katika maumivu na kumfanya kutumia mwili wake kama sehemu ya kupata chochote kitu kwa ajili ya maisha yake. *************************************** Hisia za ajabu ndizo zilizokawa zikiutafuna moyo wa stellar Kama panya alavyo mabaki ya chakula shambani. Alitaabika huku na kule kupata usingizi wake wakila siku ambao alitumia gharama kubwa za kufumba macho na kufumbua kisha kujigeuza mara kadhaa bila matokeo yenye usahihi. "Daaah nini hiki mbona nakosa usingizi Kiasi hiki..? "alijiuliza baada ya kushika simu yake na kugundua muda haukuwa rafiki kwake. "saa saba hii bado naangaika kitandani ?." Mara akakumbuka kitu ambacho kilikuwakina mtesa nafsi wakati huo na kumfanya asilale. Ilikuwa sura yakijana Mpole ambaye aliwahi kumuona mara moja kwa dharura na Wala asilijue jina lake,mwili ulimsisimka na meno ghafra yakafa ganzi baada ya taswira ya yule kijana kumjia vilivyo. "Mmmh nini hiki ?".akainuka na kukaa kitako kitandani kisha akashuka na kwenda mpaka dirishani akiwaza na kuwazua. "Stellar wanaume wanaumiza mno kwanini usikae mbali nao ".Alijikuta akijionya bila sababu."Tena uliwahi kulia kwa kwikwi kisa wao na Wala asitokee mmoja wao kukufuta machozi stellar embu shindana na adui wa nafsi yako japo kuwa ndiye shujaa wa moyo." Akajikuta akishusha pumzi na kujitupa kitandani baada ya muda usingizi ulimpitia na kujikuta kumeshakucha. Taratibu akajivuta kutoka juu ya kitanda chenye hadhi yake na kuelekea palipo maliwatoni ilikuweza kujiandaa na pilika za siku nzima. Masiku yalikimbia na kila kukicha mambo yalibadilika walikuwa na furaha basi iliongezeka mara dufu na walio fikwa na madhila basi kila kukicha ilikuwa hivyo na wakati mwingine iliongezeka. Asubuhi moja zilisikika kerere za kugongwa mlango katika hali ambayo haikuwa ya kawaida, aliyekuwa amejilaza ndani ya chumba kile alijivuta taratibu na kuusogelea mlango ilikutazama kulikoni. " Eeeh bora nimekukuta wewe mkaa bure unafikir hii ni nyumba ya baba yako ya urithi..?"aliongea kwa ghazabu baada tu kukutanisha macho yake na muhusika wachumba kile. "Mama kwani nini tatizo asubuhi yote hii?" "unajifanya hujui hivi wewe kuwaonga hao wake za watu pesa kisha ukalala nao sio tatizo ila kulipa pango ya nyumba yangu mpaka tuvaliane njuga , nimefata changu baba ". "Samahani mama angu kweli niliahidi ile Juzi ningekulipa pesa yako ila nikapata matatizo kidogo nimeshindwa kukulipa pesa yako nisaidie mama angu baada ya muda kidogo nitakupa pesa yako. " " We Koma wewe mimi sio mama yako nataka changu ". Yalikuwa maneno yaukali ambayo yalimchoma moyo na kumfanya akose cha kukiongea mbele ya mama yule ambaye jaziba zake aliamini zingetulia kwa pesa tuu na sio vinginevyo. Itaendelea ..... .usiache kuitembelea kurasa hii maridhawa kwa simulizi murua KIAPO CHA SIRI... sehemu ya nne inakuja ulikuwa nami mwanadada machachari Zaynabtaly ndani ya kurasa hii ya mkono wangu Karibu tuungane tujue ni nani mwenye kiapo hiki na huyu Sam ni nani hasa....?

at 4:20 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top