KIAPO CHA SIRI (Damu yangu haipotei) Mtunzi: ZAYNABTALY Whatsapp. : 0712272972 SEHEMU YA 01. Alfajiri tulivu iliyosindikizwa vyema na milio ya ndege na wanyama mbali mbali walio karibu kuizunguka nyumba ile zilisikika.Ikiwa ni siku mpya kwa upande wake siku ambayo hakuwaza kama ingewahi kutokea na kumkuta yeye akiwa bado yuko hai. “Tarehe 5/5/2015 juma nne ya kihistoria kwangu”. Alijisemea mwenyewe baada ya kukurupuka kutoka kitandani na kufungua dirisha la chumba alichokawa amelala na kuruhusu mwanga wajua kupenya. “Ooh umekwisha amka?”. Ilikuwa sauti ya kijana mdogo wa makamo aliyeingia ndani ya chumba kile. “Naam nashukuru nimemka salama”. “Okay pole na uchovu”. “Asante nilikwisha poa tangu jana uliponikaribisha nyumbani kwako na kushukuru mno.” “Usijali binadamu tumeubwa kusaidiana katika kila lililo ndani ya uwezo wetu japo kuna wachache hawataki kukubali uhalisia wa jambo”. “Ni kweli lakini tukiyaacha hayo nafikiri niwakati wangu sasa nawaza maisha yangu mapya natafakari wapi pakushika ili niishi kama zamani”. “Hilo sio tatizo kubwa sana tuta kaa tutaongea namna yakufanya ilikila kitu kiende sawa sasa sikia acha niwahi ofisini nikitoka nitakutafuta tupate chochote kitu kisha tujadili kuhusu maisha sawa…?”. “Amna neno”. Huo ukawamwisho wa maongezi ya vijana wale wawili huku mmoja wao akionekana mwenye dhiki na wakuhitaji msaada huku akiwa na jambo zito kichwani linalo pambana na ubongo wake ili kupata jibu kamili. ******************************* Purukushani za hapa na pale ziliendelea katika kila kona ya nyumba za jiji la Dar Es Salaam.Wanafunzi ndani ya sare zao zenye kupendeza za kila namnakulingana na shule walizokawa wakisoma walionekana kupendeza huku wakiwa na haraka yakuwahi shuleni.Wafanya kazi maofisini pia walikuwa hai hai ilikuweza kuwahi majumu yao yasiku ile. “Mume wangu wasaa unazidi kwenda na mtoto anapaswa awahi kwenda shule au nimuitie gari ije imchukue tuu?”. “Mke wangu afya yangu sio njema sana muache mtoto awahi shuleni nikipata nguvu nitamfata wakati wakurudi”. “Kwahiyo hutoweza kwenda kazini kwasiku ya leo mume wangu?” “Sito weza achanifanye taratibu za kwenda hospitali kwanza”. “Sawa acha nifanye taratibu za kumpeleka mtoto shuleni kwanza kisha tuone tunafanya je kuhusu matibabu”. Haraka akawasiliana na aliyekuwa dereva wake wa mara kwa mara na punde aliwasili na kumchukua mtoto kisha kumpeleka shuleni.Kisha akarejea ndani ilikuweza kumuandaa mumewe kisha kumpeleka hospitali kwa ajili ya vipimo na kupatiwa dawa. “Vipimo vinaonyesha hali ya mumeo sio salama sana presha yake imeshuka mno ndiyo hali iliyopelekea akawa anapata homa na kupoteza nguvu, muhimu ajitahidi kufanya mazoezi na kula kwa wakati wakati mwingine ataweza kurejewa na hali hii akiwa mwenye mawazo na kutokula kwa wasaa lakini pia ana malaria wawili hivyo tumemuandikia dawana fikiri zita msaidia muhimu ajitahidi sana kunywa maji”. “Asante daktari nashukuru”.Haraka akamkongoja mume wake mpaka kwenye gari na kumpeleka mpaka nyumbani. “Pole sana mume wangu Daktari amesema utaendelea vizuri baada ya kutumia dawa acha tufike tuone inavyokuwa.” Safari ya kurejea nyumbani ilianza huku kimya kikitawala ndani ya gari huku mume akilalama kwa maumivu makali kila dakika.Hatimaye waliwasili nyumbani na kikaandaliwa vyema chakula na kuwekwa mezani wakala kisha mgonjwa akapatiwa dawa na kupumzika. Jioni ilipotimu kila mtu alitamani kuihitimisha siku yake ikiwa vyema kabisa wanafunzi walikuwa tayari kurejea ma kwao na wafanyakazi walikuwa mbioni kufunga ofisi zao ili waweze kupata wasaa wakutulia na familia zao. “Hallo..?, Sam minilikwisha toka kazi njoo basi pale nilipokuelekeza jana tupate msosi”. “Sawa bro acha nitoke nakuja”.Alifunga safari na kuelekea ambapo alihitajika wakapata chakula huku wakipiga soga za hapa na pale wakati wakiwa bado wanaendelea kupata chakula kulikuwa kuna taharifa ya habari mbaya ambayo ilikuwa ikirusha kupitia kituo cha habari clouds kupitia taharifa ya habari ya saa moja jioni. “Ajari mbaya ya gari imetokea barabara ya shekilango na watu watatu wamepoteza uhai hapo hapo wakiwemo watu wazima wawili mke na mume Mr na Mrs SUDDEIS pamoja na mtoto mdogo aliyenaumri usio zidi miaka mitano kutoka katika gari ya upande wa pili ikisemekana alikuwa akirejea kutoka shule dereva aliyesababisha ajali ile alikimbia baada ya tukio.” Mara simu ya Sam iliitaakainuka na kwenda kuipokea pembeni. “ Naam kazi yako imekwisha kamilika nachohitaji ni changu”. “kuwa mpole kila kitu kinaenda kikiwa na mikakati maalumu kazi bado haijaisha”. Kisha akakata simu na kwenda kuketi. “Sam umesikia msiba huu wa Mzee SUDDEIS ?”. “nimeusikia ila sidhani kama unamashiko yoyote kwangu”. “Achana na hizo habari ngoja tufatilie taratibu zote kisha tuende kwenye mazishi”.Sam hakuwa na neno zaidi ya kumsikiliza mwenyeji wake pasi na kujua ni jambo gani hasa alilifikiria. ******************************* Taharifa ziliwafikia Mr na Mrs Elly yakuondokewa na mtoto wao kipenzi sara lakini haikuwa hiyo tuu machungu yalizidi mara mbili baada ya Mrs Elly( Stellah) kuondokewa na wazazi wake pia ndani ya siku moja kwa pamoja. Hatimaye taratibu za mazishi zikapangwa na marehemu kufikishwa katika nyumba Zao za milele. Wakati shughuri za mazishi zikiendelea punde Stellar akakutanisha macho yake na kijana ambaye sura yake haikuwa ngeni mbele ya macho yake alikumbuka aliwahi kumuona mahali ila hakuwa ni Uhakika wapi. Mazishi yalimalizika Salama na baadhi ya ndugu na jamaa Walio wasili kwa ajili ya kuifariji na kuipa pole wanafamilia walianza kurejea makwao.Asubuhi moja stellar akiwa anafanya usafi ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi wazazi wake enzi za uhai wake mara katika kupekua pekua akakutana na picha ya mtu. Picha ambayo ilimkumbusha mtu ambaye alikwisha msahau kwa muda mrefu Sana lakini akakumbuka aliwahi kumuona siku za karibuni. "Mmh nani huyu..? " akajiuliza pasi na Kumpata mtu wakumsaidia kumpatia jawabu la swali lake. "na nambona kama nilimuona msibani...? "swali jingine likaubeba ubongo wake pia likiwa halina jibu kamili. " Vipi mke wangu Kuna tatizo?". Ilikuwa sauti ya mume wake Elly ambayo ilimshtua na kumsahaulisha yote kuhusu ile picha. "Hapana Sina tatizo ". Huku akijaribu kuificha ile picha ambayo alikuwa ameishikiria mkononi mwake. " unauhakika..? " "Ndio, ningekuwa na tatizo ningelisha kuambia ". "Basi sawa, ila najua upo katika wakati ngumu Sana mke wangu japo nami pia nipo katika wakati ngumu ila tujikaze kila kitu kina sababu ya kutokea, lakini vipi aliwahi kuja yule dereva aliyekimbia tangu msiba utokee? ". "Hapana sijawahi muona ila ungemuacha tuu sioni umuhimu wakudeal naye ". "Mmh sawa kama niivyo acha miniwahi ofisini basi ". "sawa kazi Njema". Akamuaga mkewe kisha akafunga safari kuelekea pahali alipo kawa anafanyia kazi na kumuacha mkewe nyumbani. "Hivi huyu ni nani ". Aliitoa tena ile picha na kuitazama mara taswira yazamani ikaanza kumjia ulikuwa miaka kadhaa iliyopita ndipo alipo kutana na yule aliyekawepo katika picha ile. "Sam.. , Ndio ni Sam yule alikuwa wapi siku zote hizo ". Alikwisha pata picha juu ya mtu yule aliyekawa akimuangalia kwenye picha ile ambayo alionekana ni mtu ambaye alipoteana naye kwa muda sasa. "sasa nitampata wapi tena Sam iliniweze kuongea naye nitampata wapi ".akajikuta akiongea mwenyewe asijue chakufanya, moyo wake ulionekana kuhitajia Sana kuonana na Sam lakini ilikuwa ngumu kujua wapi angeweza kumuona. Masaa yalipita siku ikayoyoma huku kichwani akiwa na mawazo juu ya Kumpata Sam. Je Sam ni nani ....? Na nini kilitokea usikae mbali na kurasa hii maridhawa ilikupata uhondo halisi wa simulizi zenye kukonga nyoyo ni yule yule mwanadada machachari ZAYNABTALY ndani ya KIAPO CHA SIRI ....... usikose sehemu ya pili......

at 4:19 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top