NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 47 Nikiwa nakaribia kumaliza mapumziko yangu, nilisafiri pamoja mke wangu Rabia na kuelekea kijijini kwetu kwa sababu zilikuwa zimetimia siku za kufanya tambiko. Tukaonana na wazee wakatubariki na kurudi tena jijini. Maisha yangu yalibadilika na sasa nikaweza kurudi kazini na kupanda cheo na kuweza kumiliki magari, mashamba na nyumba tatu, kamwe sikusahau kuwasaidia watu wote wenye matatizo na Mungu akanibariki kwa mtoto mzuri wa kike nikamuitwa Catherine. Kwa muda wote huo sikusahau kuhakikisha nazungumza na watu mbalimbali kuhusu niliyoyaona na wengi walinisikiliza mara moja na kuogopa, siku ya pili walisahau na kuendelea na maisha yao ya dhambi. Pamoja na hayo nimeandika vitabu vingi vyenye kuwaonya binadamu wenzangu kwa yale yatakayotukuta huko ahera, nimeanza kutumia pia mitandao ya kijamii ili ujumbe wangu ueleweke na uwafikie wengi. Siku nyingine huwa ninatoka na kuzunguka jiji zima hasa nyakati za usiku, nikijaribu kutazama mipango mipya ya shetani na jinsi anavyowateketeza binadamu. Nimeona mengi, naufahamu uwezo mkubwa wa Lusifa kwenye hii dunia na kamwe sisi kama binadamu hatuwezi kumshinda bila msaada wa Mungu na malaika zake. Tafadhali kama umeisoma hadithi hii jitahidi kumfikishia ujumbe huu na mwenziyo ili achukue hatua. Ni mimi Denis. Mbarikiwe wote mliosoma hadithi hii na kujilinda na hila za shetani. Mungu atulinde.. Ameen. *****mwisho***

at 4:18 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top