Home → simulizi
→ NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 46
Niliondoka kwa hasira kwa sababu nilitambua kiongozi kama huyo lazima angenielewa kwa sababu suala langu ni la kiimani moja kwa moja na si la kidunia lakini kwa kuwa amelitazama kidunia nikaachana naye nikayakumbuka ya Shehe.
揕azima elimu hii niifikishe kwa watu wenzangu,� nilijisemea mwenyewe kimoyomoyo.
Nilikaa nyumbani nikiendelea kupoza misukosuko ya kimaisha iliyonikuta huku ya Lusifa yakiwa ni siri yangu maana hata Rabia hakujua nini kilichoendelea.
Afya yangu ya akili na mwili ilirudi vizuri na penzi langu na Rabia likazidi kuchanua na wakati huo nilikuwa makini kuwahi kurudi na kumtoa out mke wangu ili mradi asiwe na mawazo, kila mtu aliyetuona alituonea wivu na tukawa mfano wa kuigwa kwa kila anayetufahamu.
Nakumbuka rafiki yangu Shehe mara ya mwisho kusikia chochote kutoka kwake, nilisikia alifumaniwa na mke wa mtu na akakimbia kabisa mjini jina lake likiharibiwa kabisa.
Hii inatufundisha kuwa chochote unachokifanya kwenye giza huja juu kwenye mwanga, ni vyema usiigize kama mtu wa Mungu wakati siyo au pengine ni wa uvuguuvugu kama shehe maana shetani atakuumbua tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: