Home → simulizi
→ SHANGAZI ANATAKA
STORY NA 🅱
SEHEMU YA ISHIRINI 2B
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TISA :“inamaana wewe siyo dada wa baba Jayden?” aliuliza mama
Jayden akiwaangalia kwazamu, Dr Stella na baba Jayden “nazani nimesha kuambia kila kitu”
alijibu Dr Stella au mama Jada “na amkuwai kukutana kimwili?” aliuliza tena mama Jaydeni au
bibi Jada “aswaaa, hakuna aliewai kuingiza ata kidole cha mkono” alijibu tena shangazi ambae
alikuwa anaamini kuwa yupo sahii kabisa kwajambo alilolifanya, endelea....
“Eti mume wangu nikweli anacho ongea wifi?” mama jayden alimwuliza mume wake ambae muda wote
alikuwa amekaa kimya kajiinamia, “baba mkwe mweleze mama nayeye ajuwe kama nikweli niliyo
yasema?” aliongea mama jada au Dr Stellah akimwambia baba Jayden, huku Dr Stellah akuwa na ata
chembe ya utani, “nikweli mke wangu, huo ndio ukweli halisi, lakini siku juwa kama Stella
angefanya aliyo yafanya, yani ni haibu kubwa sana kwenye familia zetu, na wale waliotufahamu
toka zamani” aliongea baba Jayden kwa sauti tulivu na nzito iliyo jawa na mfadhaiko, “
samahani baba si,vyema ukiniita kwa jina, ni bora ukiniita kwa jina la mwanangu yani mama Jada
au mkwe, alafu mimi ni mke wa mwanao, ahibu ya nini?” aliongea Dr stellah kwa sauti ya upole
iliyojaa adabu na heshima, kanakwamba anaongea na wakwe, hapo mama Jaden akatulia kidogo,
kisha akamtazama Jayden akiwa amempakata mwanae Jada, "mwanangu nawewe ulianzaje anzaje ku…
yani haa! watoto hawa jamani, yani ata kuogopa kidogo mwanangu?, we mmama kama huyu...
uliwezaje mwanangu?...” ukweli mama Jayden alishindwa kuongea “mama samahani, hapo unamkosea
mumewangu, uwezi kumwuliza hivyo mbele yangu, na hiyo ni siri yetu, kama mmesha elewa
kilichotokea, naomba mume wangu akaoge, ili ajiandae kwa chakula” aliongea tena Dr Stellah
kwasauti ya upole yenye hesima na adabu, wote wakakubali Jayden aende kuoga,
Kumbe ujio wa wazazi wa Jayden, shangazi aliufahamu mwzi mmoja kabla,akaamua kumficha
Jayden maana angekosa amani kusikia wazaziwake wanakuja, wazazi wa Jayden walipo fika na
kumwona mtoto waligundua amefanana sana na Jayden, kwa mama Jayden haikuwa tatizo maana Jayden
amefanana baba yake, pia alikuwa anajuwa kuwa wifi yake ni dada wa mume wake, mtoto kufanana
na Jayden nisawa maana ni ndugu, tatizo likawa kwa baba Jayden au Joseph, alipo mwona mtoto
kengere ya hatari ikagonga kichwani kwake, ndipo alipo jikuta ameuliza juu ya baba wa mtoto,
na Stella akuficha akawa chana live kwamba mtoto ni wa Jayden,*******
Muda wakulala Jayden na mpenzi wake, wakihapo cha kurithi Dr Stella akiwa chumbani
kwao, waliongea mengi sana ikiwa ni pamoja na mipango yao yakimaisha, huku chumba kingine mama
na baba Jayden walikuwa wajadiliana juu ya mausiano ya Jayden na Dr Stellah, kweli ni alali
kwa Jayden kuishi na shangazi wa hiyari kama mke wake?, atimae asubuhi ikawadia, siku ile
jayden akwenda chuo, baada ya kunywa chai baba Jayden akaomba wote wakae bale sebuleni waongee
jambo, dakika chache baadae maongezi yakaanza, baba Jayden alisema kwamba kiukweli yeye na mke
wake wame kubari kwa moyo mmoja Jayden kuishi na Dr Stella,lakini walicho itaji nikwamba Dr
Stella amchukulie Jayden kama walianza kukutana wao na asichukulie kama ni kisasi cha
kuthalitiwa na baba yake Jayden, Dr stelah aliwaahidi kwa kusema kuwa yeye ameamua kuolewa na
Jayden kwasababu ya mapenzi yake toka moyoninasiyo kisasi,
Mahisha yaliendelea vizuri pale nyumbani, wakiishi kwa amani huku Dr Stellah
akiwaheshimu wazazi wa Jay den kama wakwe zake japo mama Jayden, wakati mwingine alikuwa
anakosea na kumwita Stellah wifi, atimae likizo ikaisha na wazazi wa Jayden waka rudi songea
nakumwacha Jayden na mke wake, nao Jayden na Dr Stellah waliishi vizuri na kwa upendo na
amani, mpaka mwisho wa story hii, nikwamba Jayden naye Doctor anafanya kazi hospitary ya
muhimbili, licha ya kuwa yeye na mke wake walifungua hospital kubwa mbili nyingine, pia
walijenga nyumba nyingine mbili na kufungua shule, primaly and secondaly academy school, na
tayari wameshapata watoto wengine wawili, siku zote waliishi maisha ya furaha na amani, kwani
ata wakina Dr Suzie walisha fahamu ukweli kuwa Dr Stellah na Jayden ni wapenzi, japo mwzo wali
ashangaa sana lakinibaadae walijuwa siyo ndugu na kuwazowea, wakawaona wakaida, mwanzo ikuwa
ngumusana kwa Dr Suzie kukatisha mausiano na Jayden, lakini mpenzi wake alipo maliza chuo
ikamlazimu kufanya hivyo, ingawa mechi za mpenzi wake azikumfikia Jayden...
MPAKA HAPO TUMEFIKIA MWISHO WASTORY HII JIANDAE NA STORY YA NYINGINE AMU SANA YA: 🅱
KAMA UNAMAONI AU USHAURI KARIBU IN BOX MAONI NA USHAURI WAKO VITATAFANYIWA KAZI ASANTENI KWA KUFWATILIA NAKUSOMA STORY HII MWANZO MPAKA MWISHO ASANTENI MLIO LIKE, MLIO COMMENT NA KUTOA MAONI YENU, ASANTENI SANA MLIO SHARE....MWISHOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: