NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 32 Nikiwa na hofu kubwa kiasi hicho ndipo sasa nilikumbuka kuwa LUSIFA lilikuwa ni jina lake la awali alipokuwa mbinguni akiwa kama malaika mkuu. Baada ya kukaidi na kumuasi Mungu ndipo alipotupwa duniani na kupewa kila jina baya likiwemo Ibilisi na mengine kwa kila lugha ambayo mimi na wewe tunaifahamu. Nilistaajabu kuwa kumbe hata yeye mwenyewe huchukia kuitwa Ibilisi na bado anapenda kuitwa Lusifa jina la malaika mkuu. Wakati nikifikiria hayo ghafla alirudi katika umbo lake la awali sura yake ilionekana kuwa kama vile mwanamke mzuri lakini sasa niligundua kifuani alikuwa hana matiti bado nikawa nimechanganywa na umbile lake. Nilishangaa kwa nini Lusifa alikuwa akinikawiza kwa kuniachia muda huo wote; maana kama nilitakiwa kuchomwa moto basi kwa nini hakunionesha sehemu yangu niungulie mbali? Japo niliombea kutopelekwa huko. Nahisi alinisikia nikiwaza hivyo akaniambia; “Wewe si mwandishi! chukua karatasi na peni na uandike haya kisha wafikishie wenzio huko duniani,” “Je hii ni Interview? Kwa hiyo utanirudisha duniani?” nilijikuta nikiropoka. “Muda wako wa kuja huku bado, fanya kama nilivyokwambia, nitajibu maswali kumi tu!” alisema kwa amri, alipomaliza tu nikashangaa kuona peni na notibuku vikitokea mbele yangu. Nikakishika na kuanza kuwaza maswali ya muhimu kabisa ya kuuliza ili mradi nisije nikauliza maswali kumi ambayo hayana faida kabisa kwa walimwengu. Je, kama wewe ungetakiwa ungekuwa Denis ungemuuliza nini Lusifa?

at 4:13 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top