Home → simulizi
→ NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 33
Nilifikiria jinsi ya kumtwanga maswali ambayo nilikuwa na uhakika kila mtu duniani alikuwa akitaka kupata majibu yake kwa kuwa hiyo ilikuwa ni nafasi adimu sana kupatikana kwa kiumbe chochote duniani. Hivyo sikuwa na budi kuitumia vyema.
Niliinua midomo yangu na kuanza na swali la kwanza, “Umekuwa na uadui mkubwa na mwanadamu, tangu Mungu akufukuze mbinguni na mara zote umekuwa ukienda tofauti na Mungu, lakini mwishoni umekuwa ukishindwa je, huoni sasa ni muda muafaka wa wewe kumuomba Mungu msamaha na urudie utukufu wako?”
Kabla hajajibu chochote alinyanyua mkono wake na kuchora namba moja angani, nikatambua alikuwa akiweka kumbukumbu ya swali langu la kwanza.
“Kwanza Mungu hakunifukuza mbinguni bali kwa uonevu, hakutaka kabisa nimuombe msamaha, akanitupa duniani. Kisasi changu nikakihamishia kwa nyinyi wanadamu maana anawapenda sana. Nikajiapiza kuwa nitamuonesha Mungu kuwa nyinyi hamna upendo kwake kama yeye anavyowapenda. “Tukaweka agano na yeye akaniambia niutumie muda huu kabla sijatupwa motoni kumuonesha kwa vitendo kuwa wanadamu hawampendi, na hiyo ndiyo kazi yangu. Kila siku naweka hesabu ya maelfu ya watu ninaowaingiza motoni na ninauhakika hata Mungu mwenyewe anapoteza imani yake kwenu.”
Nilistaajabu baada ya kusikia hivyo nikamuomba anioneshe japo kidogo jinsi watu wanavyoingia motoni akanibeba kwa spidi na kuniweka kilele cha kuzimu nikaona watu wengi mfano wa mchanga wa bahari wakimiminika motoni. Akanionesha njia kuu ielekeayo peponi akaniambia tazama watu wanaoingia kule, maskini nikamuona mtu mmoja tu akitembea barabara nzima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: