NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 34 Nilibaki mdomo wazi nikishindwa kuzungumza neno lolote, yeye mwenyewe alionekana kujua hilo akanishtua; “Swali la pili!” Huku machozi yakinitoka nikamwambia; “Nimeona watu wengi wakiingia kuzimu na hiyo inaonekana wazi kabisa utashinda kuthibitisha kuwa wanadamu hatumpendi Mungu kwa kuwa hatufati amri zake, lakini, unaweza ukanitajia dini gani inataja amri sahihi za Mungu na ambazo tunatakiwa haswa tuzifuate?” Kwa swali hili akacheka kisha akasema; “Miaka zaidi ya elfu mbili nyuma, nimewagawa kiimani, nimehakikisha wa dini hii atamchukia wa dini ile, na hata ndani ya dini moja nimewagawa na viongozi wenu na wengi ni wa kwangu. Kwa sasa nadhani umeshajua kuwa sipambani na dini bali na yeyote anayehimiza na kufuata amri za Mungu.” Alijibu kisha akaandika tena hewani namba mbili, nikamuuliza swali la tatu; kuwa ni mbinu zipi huzitumia kutunasa wanadamu tuingie motoni kwa kiasi kingi vile, akajibu: “Ooh ninazo nyingi sana, ya kwanza ni kutumia mashetani wangu wazuri mno kama ulivyowaona njiani wakati unakuja huku ambao hawa nimewatuma kuwaingiza kwenye uasherati na zinaa viongozi wa dini na watu wanaojifanya kumtumaini Mungu kupindukia, tangu kuanza kwa mwaka huu hawajawahi kushindwa kwa mtu yoyote zaidi ya yule unayemuona anaingia kule Mbinguni, nikatamani kumuuliza anitajie jina lake yule mtu lakini nilihofia atalifanya hilo kuwa swali la nne na nikapoteza bure maswali saba yaliyobakia. Akaongeza kuwa mbali na mashetani hao, amewatuma wengine wengi kwa kila mtu ambapo alidai kwa mtu mmoja amezungukwa wastani wa mashetani ishirini wakimzonga siku nzima amkufuru Mungu kwa kila aina ya dhambi.” Kisha akaongeza kuwa ameingiza teknolojia na starehe za kila aina zinazofanya watu wasipate muda hata wa kumuabudu Mungu, akiwa anazungumza hayo akaonesha mkono wake juu kukawa wazi, nikaona mfano wa televisheni kubwa ikanionesha watu mbalimbali wakiwa wanachati makanisani, wengine wakipiga picha za uchi na kutumiana, mwenyewe Lusifa akacheka kisha akasema “Smart phone, hiki kifaa kitawatumbukiza wengi huku na ndiyo kifaa pekee ninachokitegemea kwa sasa,” aliposema hivyo nikastaajabu na kumuuliza jinsi gani smart phone zinahusika na yeye?

at 4:14 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top