NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 35 Akaandika hewani kama hilo ni swali la nne kisha akanichukua na kunipeleka sehemu yenye chemba nyingi zisizo na idadi, ndani yake nikakutana na mijitu ya ajabu ikiwa bize na kutengeneza vitu mbalimbali, nikaona vifaa vingi vya umeme na walionekana wazi kuwa ni wanasayansi kama vile wa duniani. Akaniambia kuwa hicho ni kiwanda kinachotoa kila aina ya teknolojia, na ndiyo kinachowatumia wataalamu wa duniani vitu vipya kila siku, akataja viwanda vikubwa vya teknolojia kuwa vyote vinatoa teknolojia huko. Akanionesha sehemu zinazotengenezwa hizo smart phone, akaliita jitu moja lililoonekana kama kiongozi wao, akaliambia linioneshe vitu vinavyowekwa kwenye simu zao, akaniambia angalia; nikatazama lile jitu likifungua Smart phone likatoa kifaa mfano wa kidonge kidogo cheusi (picha yake nimeiambatanisha hapo juu) likasema; “hiki tumekiweka kiwe kinanyonya na kuhifadhi damu ya kila mtumiaji wa Smart phone,” nikamuuliza inawezekanaje! akasema; “tazama hiki kioo ‘touch screen’ kina mirija maalumu ambayo huvuta damu na kuingiza kwenye hiki kifaa, ndiyo maana tunataka mtu aguse na kidole chake na si kitu kingine. Kidude hiki kikijaa damu ndiyo huja kwetu kwenye mapipa haya (akanionesha kwa kidole ni mapipa mengi sana ya damu hata idadi yake pengine yangeweza kujaza bwawa la kuogelea watu) akaongeza kuwa kile kidonge kikijaa husubiri mpaka pale utakapozima simu yako kisha ndiyo kipeleke damu, lakini kwa wale ambao hawazimi simu watashangaa simu zao zikianza matatizo ya kugandaganda na kisha kujizima yenyewe na ndiyo hapo kumbe hupeleka damu kuzimu na kuwalisha mashetani wa huko. Baada ya ufafanuzi huo Lusifa alicheka na kunitazama, akasema nimekwambia siri hizi makusudi kwa sababu hata ukawapelekea ujumbe huu wenzako huko duniani hawatakuamini watakuona chizi. Kisha akanionesha alama kumi za hatari ambazo mwanadamu akizitazama na kuzitumia hataweza tena kuepuka moto wake kwa kuwa atakuwa kama vile amenaswa kwenye mtego wa buibui, je unataka kuzifahamu ni alama gani? Itaendelea..

at 4:14 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top