NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 36 Niliziona alama zile kumi zikiwa zimechorwa ukutani kwa ufundi mno na kila jitu la kule kuzimu lilionekana kuzipa heshima kubwa. Siyo siri baadhi nilikuwa nikizijua kwa kuwaona watu wakiwa wamezivaa, nyingine hata mimi mwenyewe nilishawahi kuzivaa. Akaniambia kuwa kazi ya alama hizo ni kuharibu akili zetu, hasa akili ya ndani kwa ndani ambazo ndiyo hasa huendesha matendo yetu ya kila siku ambayo mara nyingi tunayafanya bila kufikiria. Mbali na hayo, Lusifa alisema kuwa alama hizo zina kitu kingine spesho ambapo pindi mtu anapozivaa huwavuta mashetani ili wamdhuru kutokana na jinsi alama hiyo inavyomaanisha. MONARCHY BUTTERFLY Hapa akanionesha alama ya kipepeo ‘Monarchy butterfly’ (nimeiweka hapo juu), akasema kuwa anayevaa nguo au cheni ya alama hii hujikuta akili zake zikiwa kama vile ni za kushikiwa na mwishowe hujikuta akifanya kitu kibaya bila kujua anachokifanya mpaka pale matokeo mabaya yanapowakuta. Mfano ukivaa nguo hiyo mtu akikuchokoza kidogo unaweza ukajikuta unamchoma kisu bila kujijua, ukija kushtuka ndiyo unagundua kosa lako na kuanza kujutia. Akasema kuwa amehakikisha watu wengi wananunua nguo za kipepeo yule kupitia viwanda vya nguo alivyovifungua kila sehemu duniani. 666 BAR CODE Alama hii (nimeiweka hapo juu) ilikuwa ni ya pili kuiona akasema Biblia ilikuwa imeandika siku za mwisho atakuja shetani na alama ya 666 ambayo bila hiyo mtu hataruhusiwa kuuza wala kununua, tena ikafafanua kuwa Mungu alionya kuwa kama mtu ataitumia alama hiyo basi hataingia peponi tena. Akacheka na kuniambia alama hii tayari ipo duniani na kila mtu huitumia bila kuijua na tayari tumeishamuasi Mungu hivyo tusitegemee kuingia peponi tena. Nikajiuliza nimewahi kuitumia wapi akanionesha mfano wa bidhaa ambayo mimi binafsi nilinunua ikiwa na chata hilo la 666. Nguvu zikaniishia nikadondoka chini nikiwa nimepoteza fahamu kwa sababu nilijua sina matumaini kabisa ya kuingia Peponi. Je, Denis aligundua nini kwenye 666 bar code? usikose kufuatilia kesho.

at 4:15 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top