Home → simulizi
→ NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 37
Sikujua dakika ngapi zilipita hadi fahamu zangu ziliponirudia, lakini nilishtuka na kuona kila kitu kikiendelea kama kawaida na Lusifa alikuwa mbele yangu akinitazama. Akanikebehi; “mwanadamu ni dhaifu sana, ila wewe umefikia hadi hapa ni jasiri sana ilibidi uzimie tangu mwanzoni.
Nikwambie tu kilichonifanya nizimie ni baada ya kujua kuwa kumbe ile 666barcode kuwa ipo katika kila bidhaa tunayonunua kutoka viwandani, hapo ndiyo lile neno la Mungu kuwa hatutanunua wala kuuza isipokuwa tukiwa na alama hiyo ambayo itatuzuia kuingia peponi linapotimia.
Nikashangaa kuona ikiwa ni mistari tu, nikamuuliza Lusifa inakuwaje hii mistari ikawa ndiyo 666 yake? Akaweka hiyo kuwa swali langu la tano akajibu kuwa ameweka muundo kwenye kampuni za Barcode duniani kutumia mfumo wa mistari kwa faida ya kuhifadhi jina la kampuni ya bidhaa ilipotengenezwa; siku ilipotengenezwa kuelekea kuexpire na gharama yake.
Akasema kuwa wakati viwanda vikizitumia faida hiyo kurahisisha uuzwaji wake supamarket ambapo kama umeingia utaona Cashier na kimashine Fulani akiscani hii alama na ndiyo anakuandikia bei.
Mwenyewe akasema hawajui kuwa kisirisiri yeye ameingiza 666 kwenye mfumo wa mistari hiyo ambayo ufafanuzi wake ni kuwa kila mstari una jina lake kinamba.
Kuna ule mnene wa rangi nyeusi huu hupewa jina la namba 3, ule mwembamba huitwa namba 4, lakini mistari hii yote hupangwa kwenye misingi ya mistari mitatu mikuu ambayo huwa ni miwilimiwili ambayo hupewa jina la 6. Mistari hii mitatu ambayo hujulikana kwa urefu wake huwa mwanzoni mwa barcode, katikati na mwishoni.
Hapo ndiyo hupatikana ile 6- 6- 6. (ufafanuzi pichani)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: