Home → simulizi
→ NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 44
Nikakata na kupiga tena, safari hii nikasikia sauti ya mwanamke akizungumza kilevilevi tena saa nyingine wakazungumza na shehe, wote wakionesha kama vile wamelala pamoja.
Nilichofahamu ni kwamba mke wa Shehe alikuwa amesafiri na sauti yake siyo ile niliyoisikia, kama akili yangu inaweka kumbukumbu vizuri nilikumbuka kuwa mke huyo wa shehe pia hanywi pombe na ana staha kwenye mazungumzo.
Akili ikanituma kuwa shehe amechepuka maana kwa alfajiri hiyo atasingizia nini, kazi?
Nikarudi kitandani nikiwaza jinsi gani shetani anavyowaandama watu wa Mungu, nilikosa kabisa imani naye, pengine alikuwa ni mtu niliyemuamini sana na kuona mfano wa kuigwa lakini nini hasa kilichomkuta!
Hapa ndiyo nikawaza wale wanawake wazuri wa kuzimu, huenda walimfuata shehe na kumvunja misimamo wake katika dini. Hata hivyo nilimuombea Mungu ajue kosa lake mapema na kutubu haraka mara tu baada ya kurudia akili zake.
Dakika chache baadaye nilisikia sauti ya jogoo akiwika ikiwa na maana ni mapambazuko. Shauku ya kutaka nielekee kanisani kutubu dhambi zangu ikanijaa, maana niliogopa mashetani wa Lusifa huenda watanizonga na kunifanya nife muda wowote na kunivutia kuzimu mahali ambapo sikutaka kurudi hata kidogo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: