NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 43 Nilishtuka na kujiona nikiwa mwepesi kuliko kawaida, nilisimama na kutoka pale kitandani na kuanza kujiuliza mwenyewe; ilikuwa saa ngapi na siku gani! maana tangu nikae kule kuzimu nilijihisi nimetumia hata mwezi mzima nikiwa nimekaa huko. Cha kushangaza nilipotazama saa ya ukutani iliandika kuwa ilikuwa ni saa 10 usiku ili kuhakikisha nilikuwa sahihi nikaifungua na simu yangu na kuona kweli ilikuwa hivyo tena ilionesha ni tarehe 12 mwezi wa nne mwaka 2014, nikagundua kumbe kule kuzimu sikutumia hata siku moja bali ni masaa manne tu kwa sababu mpaka mara ya mwisho nilikuwa kitandani na Rabia akiwa amesinzia ilikuwa ni saa sita usiku. Nikajikuta nikiwaonea huruma watu waliokufa na kuingia motoni maana kama mimi masaa mawili nimeona mwezi, je kwa wao watakuwa wakijisikiaje? Nilisimama haraka na kujongea mezani kwangu ili niyaandike majibu yote ya Interview niliyofanya na Lusifa ili nisije nikasahau kwa kuwa yalikuwa muhimu kwa binadamu wenzangu. Lakini nilishangaa nilipofika pale mezani na kukuta kile kitabu nilichoandika maswali nikiwa kule kuzimu, kikiwa kimewekwa vizuri, hapa ndiyo nikaanza kupata hofu kuwa huenda wale mashetani wa Lusifa watakuwa wameifanya kazi hiyo kwa kuniletea kitabu hadi pale. Nilikifungua na kuona kila swali na jibu limekaa vizuri kama nilivyoandika mwenyewe. Moyo wangu ukapoa lakini shauku ya kutaka kumueleza Shehe kilichonitokea ilinishika kupindukia, nikampigia simu, alipopokea nilistaajabu kusikia sauti yake ikiwa kama ameelemewa na kilevi.

at 4:17 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top