NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 42 Nikiwa ninafikiria hayo nikamuuliza Lusifa; “Watu wengi wanakuogopa na kukuchukulia kama kiumbe unayetisha zaidi kuliko kiumbe chochote kutokana na matendo yako, je, kuna mwingine ambaye anatisha kuliko wewe? Akaweka kuwa hilo ni swali la nane akacheka na kunijibu kupitia wimbo huu aliouimba palepale; “Tabasamu lako limeniteka. Siku zinavyozidi kusonga unazidi kuniingia Silikinai penzi lako tamu Niliumizwa sana lakini wewe umeniponya Umekuja kama malaika kumbe Lusifa Umzuri mtesaji wangu, Nakupenda.” Alipomaliza wimbo ule mzuri ajabu nisiowahi kuusikia duniani tangu nizaliwe, akaniuliza; “kwa wimbo huo, nani mbaya?” Nikashindwa kujibu akaniambia kwa ukali; Ubaya ni mtazamo dhaifu wa binadamu, ewe mpumbavu, mimi ni mzuri kwa anayenipenda na hata yule anayefanya matendo kinyume na Mungu!” “Maliza maswali yako haraka uondoke! Nina mengi ya kufanya!” akaniambia kwa ukali. Nikashusha hofu kisha nikauliza swali ambalo lilikuwa likinitatiza kila Lusifa aliposhika kinanda na kuimba; “Nimeshangazwa na uzuri wa nyimbo zako na sauti yako, kamwe sijawahi kuisikia duniani kote, je, wewe unapenda muziki?” Kwa swali hili akafurahi na kuniambia; “Mwanadamu mjinga, haukusoma maandiko kuwa mimi ndiyo nilikuwa malaika mkuu, nikiimba nyimbo za kumtukuza Mungu? mimi ndiye nimegundua muziki!” akaongeza; “Nimeweka watumwa wengi duniani wakiniletea watu kupitia muziki. Muziki ni miujiza na njia ya kuja kuzimu. Tazama watu wanavyonitumikia kupitia muziki. (hapa nikaona watu wakicheza hadi kuvua nguo, wengine wakitukana kupitia muziki hata baadhi ya waimba injili na kaswida nikawaona humo) Akaniambia swali la mwisho, Kwa wakati huo sikuweza kuuliza swali lolote zaidi ya linalonihusu mwenyewe; “Je, mimi nimezungukwa na mashetani wako?” Akacheka na kuniambia, “nimekuongezea zaidi, nakungojea kwa hamu”. akacheka kisha akapiga mguu wake chini nikaona giza zito nilipokuja kuzinduka nilikuwa kitandani kwangu, nikiwa na Rabia.

at 4:16 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top