NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 41 Nikiwa na kiu ya kufahamu alama hizo mbili nilijikuta nikishindwa kujizuia kuuliza japo anitajie mfano wake, Lusifa aliyeonekana makini na maswali yangu akaniambia hilo ni swali la sita na akashikilia msimamo wake wa kukataa kuzungumzia chochote. “Kuwa makini una maswali manne tu ambayo umebakiwa uniulize, yatumie vizuri, mwanadamu,” alisema huku akinitoa pale tulipokuwa tukizungumzia. Nikamuuliza; “Inaonekana wazi kabisa kuwa hatuwezi kuepuka mtego wako katika dunia ya sasa, lakini angalau unaweza ukanitajia nini alichokifanya hadi ukamshindwa mtu yule aliyeingia peponi?” Akahesabu hilo kama swali la saba kisha akaniambia; “mtu yule mara tu alipozaliwa nilimpa mashetani saba yamsimamie na kumvuta kwenye uasi, kama ambavyo nilikufanyia wewe na wanadamu wengine wote wanaozaliwa. “Mtu yule alinifurahisha sana kwani alikua na kuwa mchawi mkubwa, akizunguka kila sehemu kuniletea roho za watu wengi wa Mungu waliodondokea kwenye mitego yake. Nilimpa nguvu akawa mkubwa sana mbele ya wachawi wengi duniani,” “Jana ndiyo nilishangaa kuona mashetani wale niowatuma wamlinde wakirudi kwangu mbio, nilipowauliza kulikoni wakaniambia mara ya mwisho walimuacha akiwa anauumwa lakini ghafla wakawa hawamuoni. “Nilimtazama kote duniani na kweli hata mimi sikumuona, nilijua kwa vyovyote atakuwa kabla ya kufa alitubu kwa dhati dhambi zake na badala yake malaika wa mbinguni wanamlinda ili kukamilisha safari yake duniani. Tangu siku hiyo sikuwahi kumuona tena hadi sasa hivi ninapomuona akiingia Peponi. Kwa maneno hayo nikagundua kuna matumaini bado ya kila mmoja kutubu kwa dhati na hatimaye kuingia peponi. “Asante Mungu kwa bahati hiyo iliyokuwa kwetu sisi binadamu tu na si kwa Lusifa na mashetani wake” nilijikuta nikizungumza kimoyomoyo. itaendelea kesho.

at 4:16 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top