NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 40 ELECTRIC SYMBOL Baada ya hiyo nikaona alama ya umeme ambayo hutumika sana kuonesha hatari ya shoti. (ipo hapo juu) Alama hii akasema huficha maana halisi ya neno ‘Shetani’ na uwezo wake, kutokana na kubeba herufi ‘s’ iyochezeshwa mfano wa zigzag. Akasema alama hii huchochea kuungua kwa nyumba kutokana na shoti na kupigwa radi au shoti ya umeme. DRAGON Alama nyingine niliyoiona ni hii ya joka maarufu kama Dragon ambalo linatajwa kutumika sana kama alama muhimu ya dini za kichina. Joka hili huwa na miguu huku likitema moto. Lusifa aliniambia kuwa watu hawafahamu kuwa joka hilo ndilo lilikuwa umbile lake lilivyokuwa alipomtokea Adam na Eva kule bustanini. Akasema yoyote atakayevaa alama hiyo atajikuta akishikwa na kiu kikali au kukaukiwa na damu kusikokuwa na sababu tena akaongeza kuwa hii husababisha mafuriko na vimbunga visivyoisha kwa mtu au sehemu ambayo mvaaji wa ile nguo huwa. Baada ya hapo nikatazama kulikuwa bado na alama nyingine mbili zilizokuwa zimebaki tena zikiwa zimefungiwa ndani ya vitambaa vikubwa. Akaniambia alama hizo mbili sipaswi kuziona kwa kuwa nikizijua nitawasaidia wengi watoke mikononi mwake. Akadai kuwa kwa alama hizo amewakamata wanatumbuizaji wakiwemo wanamuziki, wacheza filamu na wanamichezo na alama nyingine akidai huwa ndiyo inayoamsha mashetani yawaingie vijana na kuwafanya wapende ngono kuliko ibada na hata kupelekea ushawishi wa mapenzi ya jinsia moja. Kazi ni kwako kuzijua alama hizo. Itaendelea..

at 4:16 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top