NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 39 EYE OF HORUS Inatajwa kuwa Horus alikuwa mmoja ya miungu ya Misri ambaye alipoteza jicho moja katika vita na miungu mingine hivyo akawa na jicho moja. Jicho hili mara nyingi hufanywa ishara za watu maarufu duniani kwa kuziba jicho moja ili kumtukuza Horus (baadhi ya picha nimeziweka hapo juu). Lusifa alisema kuwa kwa ishara hiyo huwavuta mashetani kutoka kila kona ya dunia kumuandama mtu anayeoneshewa ishara ile ili kumdhuru. Baada ya alama hiyo Lusifa akanionesha alama nyingine hii ilikuwa na alama ya Jua na chini yake yaliandikwa maneno OBEY. OBEY Akasema kuwa alama hii inapotazamwa na mtu humfanya awe mtiifu kwa dhamira mbaya ambazo humpelekea kufanya maasi. Neno hili ‘Obey’ humaanisha ‘fuata amri’ au ‘tii’. (nimeiweka mfano wa nguo hapo) ANARCHY Alama hii humaanisha fujo na ghasia kutokana na kutokuwepo kwa utawala. Alama hii huvaliwa kwenye mashati nchini Marekani, uzuri wake Bongo bado hayajaingia hivyo kuwa makini. Lusifa alisema mtu anayevaa nguo yenye alama hii ataingiliwa na mashetani yatakayomfanya asababishe ghasia au vurugu na kufanya amani iwe kitu adimu kwenye familia yake au jamii kwa ujumla.

at 4:16 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top