Home → simulizi
→ NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 30
Baada ya kusikia sauti hiyo niliamua nisimame na kurudi kule nyuma ambako ni kuzuri zaidi maana nilianza kuhisi dalili mbaya kwenye ile sehemu niliyodhani ni mbinguni.
Lakini cha ajabu nilishangaa kuona miguu yangu ikigoma kufanya hivyo ilizidi kusonga mbele yenyewe, na hata nilipojaribu kukaa kiuno kilikataa.
Nikiwa sina cha kufanya nilisonga mbele ambapo nilishangaa kutokea sehemu ambayo niliona hakuna chochote zaidi ya jangwa lenye joto mno, hapa niliona watu wakiteseka na njaa na kiu.
Ile sauti ikabadilika na kuwa ya kuogofya kama vile siyo ya mtu ikaniita tena na kunitaka nikaze mwendo.
Nilijua fika ninapoelekea hakuna jema kwangu zaidi ya baya lakini sikuwa na jinsi miguu yangu ikanisongesha nikipitia sehemu mbaya nyingi na hatimaye nikashuhudia vyumba vidogo mno kama makabati ambapo nilishuhudia watu mbalimbali wakiwa ndani yake uchi wa mnyama.
Kwenye mapaji yao ya uso wameandikwa namba ambazo zilikuwa zikifuatana moja baada ya nyingine. Ilitisha sana. Na hapa sasa ndiyo nilipata picha kuwa kumbe kila anayekufa hupitia ile njia ninayoipitia mimi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: