NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 31 Sehemu ya mwisho ambapo ile sauti ilisikika kwa ukaribu mno ni ile ambayo tangu nikiwa duniani nilifundishwa nayo si nyingine ni moto wa milele ‘Jehanam’. Nilichokiona hakielezeki, hapa ujasiri ulinishinda, nikajisikia mpweke kuliko maelezo, kile kiburi nilichokuwa nacho sikuwa nacho tena wakati huo. Nikadondoka chini nikitetemeka kwa hofu kuu, lakini hata nilipoanguka nilishangaa kusikia maumivu makubwa yaliyonifanya nilie kwa sauti kali. Hata niliposimama na kukanyaga mguu wangu chini nilihisi maumivu makubwa mno, hata nilipojishika mwili wangu bado niliumia kama vile vidole vyangu vilikuwa sindano, kote kulikuwa maumivu. Nikiwa katika hali hiyo nilishangaa kusikia ile sauti ya ukali iliyokuwa ikiniita ikiwa karibu sana na mimi nilipogeuka nikutana na msichana mmoja mzuri zaidi hata ya wale wa mwanzoni. Macho yangu yalipotua mwilini pake niliganda kwa mshangao kama nimepigwa na bumbuwazi. Alikuwa amekamilika kila eneo lakini tofauti na wale wa kule njiani huyu alikuwa na sauti kali ya mnyama, akazungumza tena na mimi, “Denis! Unajua upo wapi na unazumgumza na nani?” Nikajibu; “Kuzimu, Shetani,” Akaniambia huku anacheka; “Umekuja kuzimu, hivyo ni lazima niwe Shetani, lakini unajua unaongea na nani!” Nikiwa natafuta kujua ni nani hasa nikaropoka, “Ibilisi” Nikashangaa akificha uso wake kama vile maneno yangu yalimchoma, akasimama kwa ghadhabu akasema kwa lisauti lake la ajabu; “Usitamke tena jina hilo!,” kisha akanyosha mkono wake mara kinanda kikatokea mkononi mwake akaimba wimbo ambao kwa hakika uzuri wake sijawahi kuusikia duniani. BAADHI YA MASHAIRI YAKE YALISEMA: Dunia yako imeumbwa na aliyejuu, “Lakini umeamua kumsaliti na kuchagua njia ya muovu badala ya upendo wake tuu, Ukanifanya mimi niwe muumba wako kwenye ulimwengu wako, Na wala Roho uliyotolewa haikumbukwi kwako.” Alipomaliza nilishangaa nikamuuliza jina lake; hakujibu mara moja badala yake alisimama na kujigeuza kiumbe wa ajabu na kutisha zaidi kuliko hata michoro ninayoitumia hapa na kwenye hali hiyo akanijibu; “MIMI NI LUSIFA” Je, nini kitaendelea usikose kesho

at 12:49 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top