Home → simulizi
→ NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 29
Nilipitia sehemu kulikuwa na mahela mengi sana ya kila nchi na thamani zake, na kila sehemu kama nilivyokwambia ilinifanya nisitake kurudi nyuma kwa uzuri wake.
Sehemu ambayo sitaisahau kabisa ni ile iliyofuata hapa. Niliona wanawake wanawake wazuri mno, siyo malaika wala majini wanaoweza kuwazidi uzuri wao.
Nilistaajabu kwani walikuwa hawajavaa chochote na walikuwa wakitembea huko na huku wakijiachia katika kila aina ya pozi wanalotaka. Miondoko yao na hata walivyozungumza kulinifanya nibaki mdomo wazi, kwa hao niliweza hata kumsahau mke wangu Rabia, kwa sekunde moja tu ya kuwaona.
Vichwani walikuwa wamevalia taji kama vile malkia, ukichia hicho hawakuwa wamevaa chochote cha kuwastiri. Cha kushangaza nao wala hawakuonekana kunijali kwa chochote nilichokuwa nikikifanya.
Nikubali tu kwamba nilishindwa kujizuia nikamshika mkono mmoja naye akageuka na kunifuata, njiani akaniumiza kwa ngozi yake laini na sauti yake nyororo.
Alikuwa akionekana kufanya kila ninachotaka, na sijui ile hamu ya kufanya naye mapenzi ilitokea wapi, nilishawishika mno kiasi ambacho haikuwahi kutokea hapo kabla nikamgusa akagusika.
Nikiwa sekunde chache kuelekea dhambini nikashtuka, nikamsukuma kasimama na kuzidi kusonga mbele nikiifuata ile sauti bila kutazama nyuma ili nisivutwe na yule mwanamke. Nikamuacha na kuingia sehemu nyingine.
Tofauti na ile ya kwanza hii ilikuwa ni ya kawaida, mfano wake ni kama maisha ya duniani, niliona watu wakiwa wamekaa kwa makundi na wengine wakizungumza lakini sura zao zilionesha hawaoni ladha yoyote ya maisha.
Nilipotazama mbele nilishangaa kuona kukiwa kubaya zaidi ya hapo. Nikatamani nisimame lakini ile sauti ilizidi kuniita nisonge mbele na kwa sasa haikuwa ya upole tena nilishangaa ikizungumza kwa ukali na kuwa nzito kidogo. “Denis Endelea!”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: