NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 28 Ile sauti ikaniambia niendelee kusonga mbele, nikaendelea kupiga hatua taratibu nikijitahidi kufuata njia moja iliyokuwa ikielekea sehemu nisipopajua. Mbele zaidi nikaanza kuona majumba mazuri ya kila aina, maghorofa ya ajabu ambayo ukubwa na miundo yake kamwe sijawahi kuiona hata kwenye televisheni za huko duniani. Ndani yake kulionekana watu wengi wakifurahia jambo, wengine wakinywa na kuponda raha wakiwa hawana hofu ya kitu chochote. Nilikuwa hata siwezi kujifananisha na wao kwa jinsi walivyokuwa wasafi na maridadi kupindukia. Nilijisikia mshamba nashukuru na wao hawakuniangalia wala kuonekana kunijali. Baada ya kutoka sehemu hiyo sasa nilitokea sehemu ambayo ule mchanga niliokuwa nikiukanyaga ulibadilika na kuwa almasi nyingi kiasi kwamba nilistaajabu. Nikashindwa kujizuia kunyoosha mkono wangu nikachota na kuzijaza mkononi. Cha ajabu upande wangu wa mashariki hadi magharibi sikuweza kuona kitu chochote zaidi ya mng’ao wa vito hivyo adimu. Sehemu hii nilitamani kubaki lakini mbele nilishangaa kuona kukiwa kuzuri zaidi ya hapa, ilikuwa ni kila kitu cha dhahabu, nilishangaa kuona hadi majumba makubwa yakiwa ya dhahabu tupu, hapa sikuona kitu chochote cha aina nyingine zaidi ya dhahabu, hadi mchanga ulikuwa dhahabu tupu. Nikachota nakuweka mkono mzima mfukoni. Nikaendelea na safari nikiifata ile sauti iliyoendelea kuniita kwa ushawishi mkubwa.

at 12:48 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top