NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 27 Fahamu zilinirudia na kukumbuka kuwa sikuwa chumbani nilipolala jana na mke wangu Rabia na kwa kuwa ilinipasa nife asubuhi ya siku hiyo hivyo nilijua wazi kuwa nimekufa na sehemu ile si nyingine bali ni kuzimu nilipotakiwa kuwepo kwa laana ya Jay Love. Nilijihisi kuchanganyikiwa nikamuomba Mungu aniepushie na adhabu zozote nitakazozikuta huko maana nilifundishwa kuwa mtu akifa basi atakutana na vipigo palepale kaburini kutoka kwa viumbe wa ajabu kabla ya kuingia kwenye moto usioisha. Wakati nimekaa pale nisijue cha kufanya nikasikia sauti nzuri ya kike ikaniambia kwa unyenyekevu; “ Denis .. njoo huku.” Nikageuka ile sauti ilipotokea, nilishangaa kuona mwanga mkubwa ukitokea kwenye tundu kubwa lililotokea mle ndani nilipokaa. Nilisimama na kutambaa kwenye lile tundu kuelekea kwenye ule mwanga, nikastaajabu baada ya kuona nimetokea sehemu kubwa yenye bustani yenye maua mazuri na kila aina ya matunda ambayo kamwe macho yangu hayajawahi kuyaona. Kiasi kwamba nikajiuliza mara mbili “huku ni kuzimu au peponi?”

at 12:47 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top