KURUDI KWA MOZA: 7 Moza alivyoona hakuna dawa inayochemka alirudi tena chumbani,muda huu akili ikamtuma achunguze ule mfuko alioutoa kwenye maua. Akachukua ule mfuko na kuanza kuuchunguza kwa kuufunua ambapo kweli alikuta kama mpira wa makaratasi umefungwa fungwa. Moza akaanza kufungua ila kadri alivyofungua ndivyo nguvu zilivyomuisha, hadi mwishoni akaanguka kabisa na kuwa kimya hapo hapo. Kimya kilitanda sana chumbani kwa Moza hadi kesho yake asubuhi kila mtu aliamka kwenye ile nyumba na kufanya shughuli zao za hapa na pale kasoro Moza, ila Rose alijua Moza amepitiwa kama kawaida yake ila aliona kengele ya hatari ikilia kwenye kichwa chake lakini alipuuzia na kuondoka kama kawaida yake kisha akaacha ujumbe mezani ila bado nyumba ilitawaliwa na ukimya. Rose ile asubuhi alimpeleka mwanae shuleni kisha na kupanga kupitia kwenye shughuli zake, “Hivi kwanini siku hizi Ana hutaki kabisa kupelekwa shule na Moza?” “Mama, kiukweli ni kuwa Yule dada simpendi kabisa yani simpendi mfukuze bhana mama” “Namtafutia kosa la kumfukuza ila sikutaka kumfukuza kwanza mpaka nitakapomfunza adabu, unajua Yule msichana amezidi sana” “kwahiyo mama umepanga tufanyaje nae? Maana unamchekea tu Yule, jitu linachunguza kila kitu mara kutandika kitanda hadi atake kufunua godoro langu, mara anivue viatu bila ruhusa yangu. Na siku ile aliyonivua viatu kanimaliza nguvu kabisa mama” “Sawa mwanangu naelewa, ila ukitoka shule nisubirie hapo hapo shuleni twende mahali kwanza, tukitoka hapo twende nyumbani na Yule Moza atakoma. Yani Yule simfukuzi ila atajitegesha mwenyewe” Rose alimfikisha mwanae shule na kumuacha hapo, kisha yeye akaenda kwenye shughuli zake. Rose alipotoka kwenye shughuli zake kama alivyopanga alimpitia mwanae na kwenda nae mahali, “Tunaenda wapi mama?” “Kwa babu” “Babu yupi?” “Yule anayefanya tuwe na nguvu” “Mbona mimi simjui huyo?” “Utamjua tu, yeye ndio kiboko alinisaidia hata kupata mimba na kukuzaa wewe. Yeye ndiye aliyenisaidia hata kumfanya Yule mzee ndani anisikilize mimi tu. Wewe mwanangu una nguvu za ziada ila huyu babu ndio atakupa nguvu zaidi maana ndio anayejua kuhusu wewe vizuri” Walivyofika kwa Yule babu, walisikia sauti ya Yule babu ikiwaambia, “Mmeshachelewa tayari” “Tumechelewa kivipi?” “Ndani ya nyumba yenu mlikuwa mnaishi na mtu wa hatari sana” “Bado sijaelewa, hebu nieleweshe vizuri babu” “Fanyeni hima mkamzike Yule mtu” “Nani tena?” “Kwani hujui? Yule msichana wako ameshakufa” Rose na mwanae Ana walishikwa na bumbuwazi, na kujikuta wakiuliza kwa pamoja tena kwa mshangao, “Amekufa!” “Ndio amekufa, yani hakuna cha Moza tena wala mdudu wa Moza” “Ila mbona ulisema tumechelewa? Na amekufaje kufaje?” “Mngewahi tungemmaliza wenyewe mtu huyu” “Kwahiyo kamalizwa na nani?” “Kamalizwa na mpira wa maajabu” “Kheee kautoa wapi huo mpira?” “Si mliuweka kwenye bustani, sasa ameuchukua wakati wa kumwagilia” “Kheee mpira wangu, sasa itakuwaje babu” “Hakuna namna, cha msingi ameshakufa. Cha kufanya nyie muwe wa kwanza kuioana maiti yake, kisha ule mpira msiutoe mikononi mwake, hakikisheni mnamzika nao. Kisha mimi nitawatengenezea mpira mwingine, yani hakikisheni ule mpira mnamzika nao. Msiutoe kabisa mikononi mwake” “Sasa tusipotangulia sisi kumuona itakuwaje?” “Jitahidini muwe wa kwanza nyinyi sababu nitawapa dawa ya watu wengine kutokuuona ule mpira, yani mtakuwa mnauona nyinyi tu. Jitahidini kesho muuzike. Mwisho wa Moza umefika tena kautafuta mwenyewe” “Basi inabidi tufanye haraka maana watoto wangu nina mashaka nao wasije wakaenda kumtoa bure. Ngoja niwapigie simu niwaongezee majukumu ili wasirudi nyumbani” Muda ule ule Rose akaanza kuwapigia watoto wake, akampa kila mtu majukumu ambapo kwa majukumu waliyopewa ilikuwa ni vigumu sana kurudi nyumbani yani ni lazima wangerudi kesho yake ambayo hata huyo Rose ndio alipanga kesho yake hiyo ndio amzike Moza. Ana akamuuliza mama yake, “Kwani watakuja watu kwenye huo msiba?” “Watu watoke wapi? Kwanza ndugu wa Moza hatuwafahamu yani hapa tutaongea na vijana tukamzike na ikiwezekana sijui tukiwahi tumzike usiku huu” Yule mganga akawaambia, “Hapana Yule si wa kuzikwa usiku, anatakiwa kuzikwa mchana kwenye jua kali kabisa sababu ndio itakuwa uthibitisho wa kifo chake na hakika hatawasumbua tena kwani hata kumbukumbu yake haitakuwepo” “Sasa si watu wa serikali watatushtukia?” “Kuna dawa nitakupa ya kumwaga getini kwako pindi tu ukirudi kisha kila kitu kitakuwa shwari kabisa. Hakuna mtu atakayejua chochote” “Utakuwa umetusaidia sana, yani Yule msichana loh nilitokea tu kutokumpenda ila cha kushangaza kumfukuza nilikuwa siwezi ila kajiua mwenyewe bora maana hata kwa Mungu sina dhambi juu yake. Kajimaliza mwenyewe” “Nawapa na dawa ya kuoga yani baada ya maziko ya Moza mkaoge, ila baada ya wiki mje tena kuna tambiko inabidi tulifanye, Yule Moza hakuwa mtu wa kawaida Yule kama wengine” Basi Rose na Ana wakaondoka zao huku Ana akimuhoji mama yake, “Moza hakuwa mtu wa kawaida kweli mama maana tukipanga hivi yeye anafanya vile, ila kufa sijui ndio kafaje kafaje” “Tutajua huko huko nyumbani tukifika” Njiani gari yao ikapata pancha, ikabidi Rose atafute watu wa kuziba pancha ya gari yake. Leo Salome akiwa nyumbani kwao na mama yake, akamueleza kuhusu alivyokutana na Moza na jinsi alivyompeleka hadi anapoishi, “Jamani kumbe kasharudi hapa mjini” “Ndio mama” “Naomba kesho unipeleke nikaonane nae maana nina mengi ya kuzungumza nae” “Sawa mama nitakupeleka” “Unajua Yule Moza alikuwa na utambuzi wa hali ya juu yani alikuwa anatambua mambo sana, natumaini nikikaa kyzungumza nae basi tutazungumza mambo mengi sana. Halafu kuna kitu nataka anisaidie” “Kitu gani hicho mama” “Salome, wewe bado mwanangu ila ukikua utaelewa yote ambayo mwanawake yanatupata. Kuna dawa alishawahi nidokeza ipo kwa bibi yake” “Huyo bibi yake ameshakufa” “Kheee amekufa! Maskini jamani yani yeye alikuwa anasema amebakiwa na bibi yake tu, kumbe alikufa masikini dah! Ila natumai hiyo dawa atakuwa anaijua” Basi Neema na mtoto wake wakapanga kuwa kesho yake waende huko anapoishi Moza ili Neema akazungumze nae bila ya kujua kuwa huyo Moza ameshapatwa na majanga kule nyumbani. Kwa upande wa Sara nae alipopigiwa na mama yake simu na kuambiwa kuwa aende Morogoro na airudi nyumbani siku hiyo hadi kesho yake kwakweli moyo wake ulikuwa mzito sana kufanya hivyo, “kwakweli mama nae amezidi, kwanini asiniambie tangu asubuhi kuwa niende Morogoro? Yani anakuja kuniambia jioni hii hapana kwakweli, sijisikii kabisa kwenda Morogoro muda huu. Nitaenda tu kesho asubuhi, ngoja nirudi nyumbani nitamwambia tu nyumbani kuwa nimeshindwa kwenda Morogoro saa hizi” Wakati anapanga hayo akapigiwa simu na namba mpya na kuipokea, “Nani mwenzangu?” “Ommy anaongea hapa” “Kheee Ommy jamani, ulivyonifanyia sio vizuri Ommy unajua name nina moyo” “Naelewa Sara, ila nataka kuzungumza na wewe kwanza” “Sasa muda huu naenda nyumbani, labda uje nyumbani au unasemaje?” “Sawa, hata mimi nipo mitaa karibu na kwenu. Basi wewe ukifika tu nishtue nije” “Sawa” Akakata simu, yani hapo ndio wazo la kwenda Morogoro kwa wakati huo likakatika kabisa kwani mawazo yake yote alikuwa akitaka kumsikia Ommy atasema nini baada ya kutokuonana nae kwa kipindi kirefu sana. Safari yake muda huo ilikuwa ni moja kwa moja nyumbani kwao. Kwakweli lile swala la pancha liliwakosesha sana raha Rose na mtoto wake Ana, huku wakijiuliza kilichopelekea hali hiyo. Ana akamuuliza mama yake, “Hivi kwa mfano wakina kaka na dada warudi nyumbani na wao wawe wa kwanza kumuona Moza amekufa itakuwaje?” “Kwanza swala la kurudi nyumbani bila ruhusa yangu hawawezi kufanya hivyo. Wananisikiliza sana wale na nimewaambia kazi ya Morogoro ni ya le oleo sio ya kulala ile” “Sawa mama, lakini watoto wako hawajielewagi wale haswa dada Sara na kaka Kulwa” “Hata kama wakiona wao kwanza hakuharibiki kitu, najua Sara ni muoga sana kwahiyo akiona cha kwanza atanipigia simu na nitamwmbia asifanye chochote yani wale wasikutishe mwanangu yani Moza lazima tumzike na asahaulike katika dunia hii. Kwani kuna kosa tumefanya hapo? Kifo si amekitaka mwenyewe! Mwache afe” Rose bado alikuwa anashughulika na

at 2:31 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top