KURUDI KWA MOZA: 8 Rose na Ana wakaelekea sebleni ila walipofika tu waliona jambo la kushangaza sana. Walikuta watu wamejaa sebleni tayari kwa maombolezo, kwakweli hiki kilikuwa ni kitu cha kuwashangaza sana kuwa watu wote wale wametoka wapi kwa muda mfupi ule. Lakini kabla hajajiweka sawa kuwauliza maswali, wakafika wengine yani Rose alizidi kuchukia, nao wakawa wanamsogelea na kumpa pole kwa msiba. Ikabidi Rose akae chini sasa na kuzungumza na waliokuwa karibu yake, “Mmmh watu wa huku mna ushirikiano, hivi mmejuaje kama kuna msiba ikiwa hata sisi wenyewe tumejua muda huu” “Kuna Yule dereva Juma, amepita mtaani na kutuambia wote nyumba baada ya nyumba kuwa huyu msichana wa hapa amekufa. Kwakweli tumesikitika sana, alikuwa mtu wa watu sana huyu msichana” Rose akashangaa kuwa mtu wa watu kivipi wakati hata mwezi hana kwenye nyumba yake, ikabidi aulize tena, “Kwani mlikuwa mnamfahamu?” “Ndio, Moza tena tusimfahamu! Siku ya kwanza tu alikuja kujitambulisha kila nyumba kuwa anaitwa Moza na anaishi hapa. Tena mara zote alipokuwa akienda gengeni alikuja kutusalimia, kwakweli tumemfahamu kwa kipindi kifupi halafu amekufa. Inasikitisha sana, ndiomana unaona watu wote hawa wamekuja msibani, ni muda mfupi tumemfahamu Moza ila alikuwa ni mtu wa watu” Rose akainuka na kwenda chumbani kwake akawaza kuwa Moza alikuwa anapata wapi muda wa kwenda kuwatembelea majirani na kuzungumza nao, “Yani kuna wengine pale hadi mimi mwenyewe siwajui ila Moza wanamfahamu loh kweli huyu msichana kwa umbea alishindikana jamani” Ana nae akafika chumbani kwa mama yake na kumuuliza, “Sasa mama tutafanyaje?” “Yani hapa nachanganyikiwa kabisa, yote haya kayasababisha Sara na kiburi chake, lile toto sijui nilibadilishiwa hospitali! Kwakweli sio toto langu lile” “Sasa mama huu sio wakati wa kulumbana, unajua watu ni wengi na bado wanaendelea kuja huku kila mmoja akiulizia chanzo cha kifo cha marehemu. Sijui tufanyeje kuwatoa hapa nyumbani” “Hebu kaniitie kwanza huyo Sara” Ana akatoka na kwenda kumuita Sara. Alifika sebleni na kukuta watu wameongezeka kushinda wale wa mwanzo tena wengine walijaa nje, yani ilionyesha wazi majirani wa hapo walitaka siku tu wapate nafasi ya kwenda kwenye nyumba hiyo maana ni kitu cha kushangaza kuwa watu wamesikia msiba muda sio mrefu na washajaa nyumba yenye msiba, ni kwamba hawakuwa na majukumu mengine walikuwa wanasubiri tu msiba utokee au ni nini, ila Ana alihisi kuwa watu hao walikuwa wakitamani sana kuingia kwenye nyumba ile. Kwahiyo siku hiyo ilikuwa imetokea kama bahati hivi. Ana alienda kumuita Rose ambaye alikuwa katikati ya watu wakimuuliza chanzo cha kifo cha marehemu, “Kwakweli hata hatujui ni nini labda aliumwa gafla maana tumerudi tu tumemkuta amekufa” “Dada unaitwa na mama” Sara alimwangalia mdogo wake kwa makini sana maana siku hiyo alimuita kwa heshima zote, kisha akainuka na kwenda chumbani alikoitwa na mama yake. Kufika kule Rose akaanza kumwambia mwanae, “Fanya ufanyavyo hao watu waondoke kwenye nyumba yangu” “Kheee mama wataondokaje na wamekuja msibani” “Sara sitaki ujinga, msiba msiba, msiba huo vipi? Kwani hapa ni nyumbani kwakina Moza? Hapa ni kwao hadi waje hapa? Waambie waende kwakina Moza huko kijijini ndio wakafanye msiba, nyumbani kwangu siwataki, kwanza nataka kulala saa hizi” “Kwakweli mama siwezi, labda uje kuwaambia mwenyewe ila mimi siwezi” Sara alitoka chumbani kwa mama yake na kumfanya mama yake azidi kupatwa na hasira huku watu kwenye sebule yake wakizidi kumkera. “Sikiliza mwanagu Ana, kachukue nguo zako kisha uje tulale huku wote. Naenda kuzima umeme wakae na giza hapo sebleni” Ana akaenda kuchukua nguo na kwenda chumbani kwa mama yake ambapo mama yake akawasha taa ya kuchaji mule chumbani na kuzima umeme wa nyumba nzima kisha wao wakajifungia chumbani. Sebule ilitawaliwa na giza totoro na kufanya ndani kutishe kiasi ila sababu watu walikuwa wengi na wengine wakawasha tochi za simu zao ikasaidia kufanya ndani kusitishe sana. Ila kulikuwa na matukio yaliyofanya watu wasipatwe na usingizi pale kwani kulikuwa kama kuna vitu vinawapitia kichwani, sema kwavile watu walikuwa wengi kwahiyo wasiwasi ukawa sio mkubwa. Kulipokucha, Rose alijua watu wameondoka. Akaoga na kuvaa vizuri kisha kumuandaa mtoto wake ila walipotoka sebleni walishangaa kuona watu wamejaa, huku wamama wawili wa makamo wakimfuata Rose na kumuuliza, “Sasa asubuhi hii tutapika nini kuwapa watu hawa? Na je upo tayari tulete kuni tuanze mapishi?” Rose akawaangalia kisha akawauliza, “Kwani watu hawa hawana makwao?” “Wanapo ila wamekuja msibani” “Kwani msibani ndio sehemu ya kumaliza njaa zao? Wakale makwao” “Makwao kupo, hata kulala hapa msibani ni heshima tu halafu ni utaratibu wetu waafrika mpaka pale tutakapozika” “Sikia nikwambie, sina hela ya kulisha watu hao halafu nyumbani kwangu sitaki mpikie makuni. Waambieni wakale makwao” “Dada jamani usiseme hivyo, watakususia msiba mwenyewe” “Usitake kunichekesha na wewe, kwani wakisusa ndio nini, sitaweza kuzika au nini? Nitoleeni balaa mie” Rose alikuwa na hasira sana na watu hawa, kisha akatoka na mwane Ana bila hata ya kumwambia Sara. Wale wamama ikabidi waende kumueleza Sara walichojibiwa na mama yake, “Jamani Yule ndio mwenye nyumba, sina usemi mimi.” “Mmmh makubwa ya leo, nimehudhuria misiba mingi tu lakini hakuna msiba wenye vimbwanga kama huu mara tuzimiwe taa usiku,mara tutembelewa na wadudu popo si popo sijui wadudu gani wale, haya kumekucha eti kila mtu akale nyumbani kwake mmmh sijawahi kusikia mie. Hata kuturuhusu tupike uji jamani!” Ikabidi hawa wamama wafikishe ujumbe kwa wengine, lakini watu walisema wataondoka kidogo kidogo kwenda kula ili tu washuhudie mwisho wa msiba huo utaishia wapi. Sara akaona vyema ampigie simu na baba mwenye nyumba ili ampe hizo taarifa maana wanadhalilika mtaani halafu akawapigia simu na wale mapacha ambao walikuwa tayari Morogoro, “Kuna msiba huku?” “Msiba? Wa nani tena? Au baba kafa?” “Hapana sio baba, ni Moza amekufa” “Kheee Moza amekufa jamani masikini, loh tunageuza tunakuja huko msibani” “Sasa mama anavyofanya vihoja huku msibani yani anatudhalilisha mtaani haswaaa. Njooni kaka zangu bhana tusaidiane” Halafu na Mr.Patrick nae akampa habari hizo ambaye alibaki anashangaa tu ila akakumbuka kuwa mkewe amemwambia jana yake kuwa asirudi kabisa nyumbani, “Mmmh Sara kwakweli hiyo habari imenishtua sana, nakuja nyumbani muda sio mrefu” Sara akapumua sasa baada ya kupiga simu hizo na kushukuru kwa kupiga kwani kidogo zimempa amani baada ya kuambiwa na ndugu zake kuwa wanakuja. Mr.Patrick akiwa na harakati za kuwahi nyumbani kwake, njiani akamuona mtu amesimama barabarani. Alikuwa ni mwanamke amejitanda khanga, ikabidi Patrick ashuke ili ajue huyo mwanamke amekumbwa na nini, alipotaka kumtazama Yule mwanamke aligeuka na kumwambia Patrick, “Usinitazame” Patrick akashtuka sana kwani sauti ilikuwa kama sauti ya Moza, Patrick alijikuta akimuuliza Yule mwanamke kwa wasiwasi sana, “Mbona sauti kama ya Moza” “Ndio, mimi ni Moza” Kwakweli Patrick alipatwa na uoga zaidi na kuuliza kwa wasiwasi zaidi, “Ila nimeambiwa kuwa Moza amekufa” “Umeambiwa hivyo ila kiukweli mimi sijafa” “Kwahiyo wewe ni Moza?” “Ndio mimi ni Moza, unatakiwa kunisaidia kwani msaada wangu kwasasa ni wewe” “Kheee sasa mimi nitafanya nini?” “Nitakupa maelekezo ya kufanya ukifika nyumbani, halafu jitahidi nisiende kuzikwa saa saba kama alivyopanga mama bali nizikwe saa tisa” Yani Patrick alikuwa anamsikiliza huku akitetemeka sana, Yule mtu alimpa malekezo mzee Patrick ila hakumuangalia usoni kabisa na wala mzee Patrick hakumuona kwahiyo alimuamini sababu tu ya sauti ilikuwa ni ya Moza. Mzee Patrick aliondoka mahali pale huku akili yake ikiwa haipo kabisa kwenye muelekeo wa kawaida kwani jambo aliloliona halikuwa la kawaida kabisa kwake. Nyumbani kwa Rose, kwenye mida ya saa tano, Rose alirudi na mtoto wake Ana ila bado watu walikuwa wamejaa pale nyumbani kwake kwani wote walikuja kwa nia ya msiba, Rose akawaambia watu wale, “Nishaongea na wachimba kaburi, kwahiyo saa saba tutaenda kuzika” Wale wamama wa asubuhi wakauliza, “Kwahiyo na ndugu wa Moza watakuwa wamefika muda huo?” “Hivi nyie watu mnafikiria kwa akili gani, yani nitunze maiti kwenye nyumba yangu nikisubiria ndugu zake!” “Si ungempeleka hospitali” “Halafu hiyo hela ya kuhifadhia maiti mtatoa nyie?” Wakawa kimya, ila wakaongezea lingine “Basi turuhusu tukamsafishe marehemu kabla ya maziko. Na tuwaite watu wa dini kwaajili ya mazishi” “Hivi nyie ndio mnamfahamu sana Moza kushinda mie, mnaijua dini ya Moza nyie? Kipindi hiki nilichoishi naye, sijawahi kumuona akienda kanisani wala msikitini. Hakuna siku aliyoongelea kanisa wala msikiti, sasa nyie mnataka kuita watu wa dini wafanye nini wakati mtu huyu alikuwa mpagani. Hebu niondoleeni ujinga mie” “Basi tukamsafishe” “Hivi mbona mnakazania sana au nyie wachawi? Maana sio kwa kukazania huko. Nitamsafisha mwenyewe” Ikabidi wawe kimya na wangoje huo muda ambao amesema wa kuzika ufike, Rose na mwanae wakaingia ndani ila watu pale msibani yani kila mtu alikuwa akiongea lake kuhusu ule msiba na mwenendo wa pale msibani. Kwenye saa sita na nusu, mzee Patrick nae alifika nyumbani kwake, ila muda huu mkewe alikuwa ndani kumbe alikuwa akijiandaa kwa maziko. Moja kwa moja alionana na Sara kwanza ambapo alimuuliza, “Maiti ya Moza iko wapi?” “Chumbani kwake baba” “Nahitaji kuiona” Patrick aliongozana na Sara hadi chumbani kwa moza, ambapo Patrick alimuomba Sara akamletee maji, wakati Sara ameondoka Patrick akatumia muda huo kuipulizia ile maiti dawa aliyoambiwa na mtu aliyekutana nae huku akisema kama itafanya kazi sawa na hata isipofanya kazi hakuwa na namna zaidi kwani alifanya vile alivyoelekezwa. Kisha alienda kuifunua ile maiti na kumpaka ile dawa puani, Sara alikuwa amerudi na kumshangaa baba yake, “Baba, unafanya nini tena?” “Unajua nilikuwa siamini kabisa kama Moza amekufa kweli, ndio nikawa namuangalia hapa” Wakasimama, muda kidogo akaja Rose ambapo alishangaa kumuona mume wake hapo, “Mchezo gani huo umeanza wa kurudi bila kusema?” “Nisamehe mke wangu, ila niliambiwa kuna msiba ndiomana nikarudi” “Haya sasa mtoke nataka kuita vijana wambebe tukazike maana wachimba kaburi washanipigia simu kuwa tayari” “Mmh mke wangu kwahiyo tunamzika kama hivyo tu?” “Ndio, tunamviringisha nguo zake tunamzika” “Mmmh mke wangu jamani, kwanini tusimwagizie jeneza!” “Sina hela za mchezo, huyu msichana hana hata mwezi halafu nianze kumgharamikia hivyo. Siwezi kwakweli wanakuja kumchukua tukazike. Kwanza nimechoka kukaa na maiti yake humu ndani kwangu” Patrick akawa anawaza ni njia gani atumie ili waweze kidogo kupeleka mbele muda wa kuzika kama alivyoombwa na Yule mtu, basi akajifanya amemuitikia pale mke wake kisha akawa anatoka akaanguka chini na kumfanya Rose aache kuwapigia simu vijana wa kuja kumbeba moza ili kuzika na kuanza kushughulika na mumewe, “Vipi tena?” "Mguu wang" “Mguu wako! Umeteguka au?” Ikabidi amshike na kumkongoja hadi chumbani kwao ambapo Patrick alionekana kulalamika kweli kuhusu mguu, ikabidi Rose amchue kwanza. Mapacha wa Rose nao walifika kwenye saa saba kwahiyo Sara alikuwa akiwapokea ndugu zake na kuwaeleza kinagaubaga kuhusu kifo cha Moza kwa uelewa wake, “Kwahiyo ulimkuta tu ndani ameshakufa?” “Ndio, ila mama kafanya vituko sana” “Ila mama yetu tunamfahamu, na watu hawa walivyojaa hapa najua ndio amechefukwa balaa” “Na amesema tunaenda kuzika muda sio mrefu” “Ila hicho kifo nina mashaka nacho hata sio cha kawaida ila wengine tukisema midomo michafu, ngoja nikae kimya tu.” Wakamsubiria mama yao pale, mzee Patrick nae alimpotezea muda Rose hadi alihakikisha saa nane inamfikia pale ndio akamuacha achukue vijana aende kuzika ila yeye alisema haendi sababu bado alikuwa na maagizo mengine aliyopewa na yule mtu kwahiyo alitaka kuyatekeleza wakienda makaburini na kubaki mwenyewe nyumbani. Rose alitoka na kutaka watu waharakishe huku akiwaelekeza maeneo ya makaburi ili waanzage kwenda, basi alichukua na vijana wakumtoa Moza mule ndani ila hata wale vijana walimshangaa Moza kwakweli alikuwa mwepesi kabisa kama hawajabeba mtu vile ingawa aliviringishwa mashuka ila bado alikuwa mwepesi sana. Wakati watu wanatoka ndio njiani wakakutana na Salome na mama yake ambao walikuwa wanaenda kwa Moza, walipoona watu wengi wengi wanatembea ikabidi waulize, “Kuna nini kwani?” “Kuna msiba, Yule msichana muongeaji. Mpenda watu amekufa” “Nani huyo?” “Anaitwa Moza” Kwakweli nguvu ziliwaisha kabisa ila ilibidi waongozane na hao watu makaburini, lakini Salome alikuwa haamini kabisa. Walifika makaburini, na wale waliobeba maiti nao walifika makaburini. Wakataka kuzika sasa, ila Salome aliwafata na kuwaomba “Naombeni hata mnionyeshe tu dada Moza nimuone kama kweli amekufa” Wale vijana wakamuangalia Rose na kumuuliza, “Eti tumruhusu amuone?” “Ametoka wapi huyo, aone nini na yeye embu atutolee balaa huko. Hakuna cha kuona, zikeni na nyie tumalize watu waende zao maana wanataka tu kushuhudia moza anavyozikwa” Kwa wakati huo Rose hakumtambua Salome kabisa kwani alikuwa na mawazo yake, kwanza kashachelewa muda wa kuzika. Wale watu walimtumbukiza Moza kwenye shimo, ila bila kutegemea Salome nae aliingia kwenye lile shimo. Ndani ya muda huo kila mmoja akistaajabu tukio la Salome, walipoenda kumchungulia Salome kwenye kaburi la Moza alionekana amekauka kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Itaendelea Jumatatu usiku……!!!!1 Kesho kuna majukumu ninayo kwahiyo kesho kutwa tutaendelea. By, Atuganile Mwakalile. Mapenzi na Maisha iko kwenye Facebook. Ili kuunganisha kwa Mapenzi na Maisha, jiunge kwenye Facebook leo. Jiunge au Ingia Mapenzi na Maisha KURUDI KWA MOZA: 8 Rose na Ana wakaelekea sebleni ila walipofika tu waliona jambo la kushangaza sana. Walikuta watu wamejaa sebleni tayari kwa maombolezo, kwakweli hiki kilikuwa ni kitu cha kuwashangaza sana kuwa watu wote wale wametoka wapi kwa muda mfupi ule. Lakini kabla hajajiweka sawa kuwauliza maswali, wakafika wengine yani Rose alizidi kuchukia, nao wakawa wanamsogelea na kumpa pole kwa msiba. Ikabidi Rose akae chini sasa na kuzungumza na waliokuwa karibu yake, “Mmmh watu wa huku mna ushirikiano, hivi mmejuaje kama kuna msiba ikiwa hata sisi wenyewe tumejua muda huu” “Kuna Yule dereva Juma, amepita mtaani na kutuambia wote nyumba baada ya nyumba kuwa huyu msichana wa hapa amekufa. Kwakweli tumesikitika sana, alikuwa mtu wa watu sana huyu msichana” Rose akashangaa kuwa mtu wa watu kivipi wakati hata mwezi hana kwenye nyumba yake, ikabidi aulize tena, “Kwani mlikuwa mnamfahamu?” “Ndio, Moza tena tusimfahamu! Siku ya kwanza tu alikuja kujitambulisha kila nyumba kuwa anaitwa Moza na anaishi hapa. Tena mara zote alipokuwa akienda gengeni alikuja kutusalimia, kwakweli tumemfahamu kwa kipindi kifupi halafu amekufa. Inasikitisha sana, ndiomana unaona watu wote hawa wamekuja msibani, ni muda mfupi tumemfahamu Moza ila alikuwa ni mtu wa watu” Rose akainuka na kwenda chumbani kwake akawaza kuwa Moza alikuwa anapata wapi muda wa kwenda kuwatembelea majirani na kuzungumza nao, “Yani kuna wengine pale hadi mimi mwenyewe siwajui ila Moza wanamfahamu loh kweli huyu msichana kwa umbea alishindikana jamani” Ana nae akafika chumbani kwa mama yake na kumuuliza, “Sasa mama tutafanyaje?” “Yani hapa nachanganyikiwa kabisa, yote haya kayasababisha Sara na kiburi chake, lile toto sijui nilibadilishiwa hospitali! Kwakweli sio toto langu lile” “Sasa mama huu sio wakati wa kulumbana, unajua watu ni wengi na bado wanaendelea kuja huku kila mmoja akiulizia chanzo cha kifo cha marehemu. Sijui tufanyeje kuwatoa hapa nyumbani” “Hebu kaniitie kwanza huyo Sara” Ana akatoka na kwenda kumuita Sara. Alifika sebleni na kukuta watu wameongezeka kushinda wale wa mwanzo tena wengine walijaa nje, yani ilionyesha wazi majirani wa hapo walitaka siku tu wapate nafasi ya kwenda kwenye nyumba hiyo maana ni kitu cha kushangaza kuwa watu wamesikia msiba muda sio mrefu na washajaa nyumba yenye msiba, ni kwamba hawakuwa na majukumu mengine walikuwa wanasubiri tu msiba utokee au ni nini, ila Ana alihisi kuwa watu hao walikuwa wakitamani sana kuingia kwenye nyumba ile. Kwahiyo siku hiyo ilikuwa imetokea kama bahati hivi. Ana alienda kumuita Rose ambaye alikuwa katikati ya watu wakimuuliza chanzo cha kifo cha marehemu, “Kwakweli hata hatujui ni nini labda aliumwa gafla maana tumerudi tu tumemkuta amekufa” “Dada unaitwa na mama” Sara alimwangalia mdogo wake kwa makini sana maana siku hiyo alimuita kwa heshima zote, kisha akainuka na kwenda chumbani alikoitwa na mama yake. Kufika kule Rose akaanza kumwambia mwanae, “Fanya ufanyavyo hao watu waondoke kwenye nyumba yangu” “Kheee mama wataondokaje na wamekuja msibani” “Sara sitaki ujinga, msiba msiba, msiba huo vipi? Kwani hapa ni nyumbani kwakina Moza? Hapa ni kwao hadi waje hapa? Waambie waende kwakina Moza huko kijijini ndio wakafanye msiba, nyumbani kwangu siwataki, kwanza nataka kulala saa hizi” “Kwakweli mama siwezi, labda uje kuwaambia mwenyewe ila mimi siwezi” Sara alitoka chumbani kwa mama yake na kumfanya mama yake azidi kupatwa na hasira huku watu kwenye sebule yake wakizidi kumkera. “Sikiliza mwanagu Ana, kachukue nguo zako kisha uje tulale huku wote. Naenda kuzima umeme wakae na giza hapo sebleni” Ana akaenda kuchukua nguo na kwenda chumbani kwa mama yake ambapo mama yake akawasha taa ya kuchaji mule chumbani na kuzima umeme wa nyumba nzima kisha wao wakajifungia chumbani. Sebule ilitawaliwa na giza totoro na kufanya ndani kutishe kiasi ila sababu watu walikuwa wengi na wengine wakawasha tochi za simu zao ikasaidia kufanya ndani kusitishe sana. Ila kulikuwa na matukio yaliyofanya watu wasipatwe na usingizi pale kwani kulikuwa kama kuna vitu vinawapitia kichwani, sema kwavile watu walikuwa wengi kwahiyo wasiwasi ukawa sio mkubwa. Kulipokucha, Rose alijua watu wameondoka. Akaoga na kuvaa vizuri kisha kumuandaa mtoto wake ila walipotoka sebleni walishangaa kuona watu wamejaa, huku wamama wawili wa makamo wakimfuata Rose na kumuuliza, “Sasa asubuhi hii tutapika nini kuwapa watu hawa? Na je upo tayari tulete kuni tuanze mapishi?” Rose akawaangalia kisha akawauliza, “Kwani watu hawa hawana makwao?” “Wanapo ila wamekuja msibani” “Kwani msibani ndio sehemu ya kumaliza njaa zao? Wakale makwao” “Makwao kupo, hata kulala hapa msibani ni heshima tu halafu ni utaratibu wetu waafrika mpaka pale tutakapozika” “Sikia nikwambie, sina hela ya kulisha watu hao halafu nyumbani kwangu sitaki mpikie makuni. Waambieni wakale makwao” “Dada jamani usiseme hivyo, watakususia msiba mwenyewe” “Usitake kunichekesha na wewe, kwani wakisusa ndio nini, sitaweza kuzika au nini? Nitoleeni balaa mie” Rose alikuwa na hasira sana na watu hawa, kisha akatoka na mwane Ana bila hata ya kumwambia Sara. Wale wamama ikabidi waende kumueleza Sara walichojibiwa na mama yake, “Jamani Yule ndio mwenye nyumba, sina usemi mimi.” “Mmmh makubwa ya leo, nimehudhuria misiba mingi tu lakini hakuna msiba wenye vimbwanga kama huu mara tuzimiwe taa usiku,mara tutembelewa na wadudu popo si popo sijui wadudu gani wale, haya kumekucha eti kila mtu akale nyumbani kwake mmmh sijawahi kusikia mie. Hata kuturuhusu tupike uji jamani!” Ikabidi hawa wamama wafikishe ujumbe kwa wengine, lakini watu walisema wataondoka kidogo kidogo kwenda kula ili tu washuhudie mwisho wa msiba huo utaishia wapi. Sara akaona vyema ampigie simu na baba mwenye nyumba ili ampe hizo taarifa maana wanadhalilika mtaani halafu akawapigia simu na wale mapacha ambao walikuwa tayari Morogoro, “Kuna msiba huku?” “Msiba? Wa nani tena? Au baba kafa?” “Hapana sio baba, ni Moza amekufa” “Kheee Moza amekufa jamani masikini, loh tunageuza tunakuja huko msibani” “Sasa mama anavyofanya vihoja huku msibani yani anatudhalilisha mtaani haswaaa. Njooni kaka zangu bhana tusaidiane” Halafu na Mr.Patrick nae akampa habari hizo ambaye alibaki anashangaa tu ila akakumbuka kuwa mkewe amemwambia jana yake kuwa asirudi kabisa nyumbani, “Mmmh Sara kwakweli hiyo habari imenishtua sana, nakuja nyumbani muda sio mrefu” Sara akapumua sasa baada ya kupiga simu hizo na kushukuru kwa kupiga kwani kidogo zimempa amani baada ya kuambiwa na ndugu zake kuwa wanakuja. Mr.Patrick akiwa na harakati za kuwahi nyumbani kwake, njiani akamuona mtu amesimama barabarani. Alikuwa ni mwanamke amejitanda khanga, ikabidi Patrick ashuke ili ajue huyo mwanamke amekumbwa na nini, alipotaka kumtazama Yule mwanamke aligeuka na kumwambia Patrick, “Usinitazame” Patrick akashtuka sana kwani sauti ilikuwa kama sauti ya Moza, Patrick alijikuta akimuuliza Yule mwanamke kwa wasiwasi sana, “Mbona sauti kama ya Moza” “Ndio, mimi ni Moza” Kwakweli Patrick alipatwa na uoga zaidi na kuuliza kwa wasiwasi zaidi, “Ila nimeambiwa kuwa Moza amekufa” “Umeambiwa hivyo ila kiukweli mimi sijafa” “Kwahiyo wewe ni Moza?” “Ndio mimi ni Moza, unatakiwa kunisaidia kwani msaada wangu kwasasa ni wewe” “Kheee sasa mimi nitafanya nini?” “Nitakupa maelekezo ya kufanya ukifika nyumbani, halafu jitahidi nisiende kuzikwa saa saba kama alivyopanga mama bali nizikwe saa tisa” Yani Patrick alikuwa anamsikiliza huku akitetemeka sana, Yule mtu alimpa malekezo mzee Patrick ila hakumuangalia usoni kabisa na wala mzee Patrick hakumuona kwahiyo alimuamini sababu tu ya sauti ilikuwa ni ya Moza. Mzee Patrick aliondoka mahali pale huku akili yake ikiwa haipo kabisa kwenye muelekeo wa kawaida kwani jambo aliloliona halikuwa la kawaida kabisa kwake. Nyumbani kwa Rose, kwenye mida ya saa tano, Rose alirudi na mtoto wake Ana ila bado watu walikuwa wamejaa pale nyumbani kwake kwani wote walikuja kwa nia ya msiba, Rose akawaambia watu wale, “Nishaongea na wachimba kaburi, kwahiyo saa saba tutaenda kuzika” Wale wamama wa asubuhi wakauliza, “Kwahiyo na ndugu wa Moza watakuwa wamefika muda huo?” “Hivi nyie watu mnafikiria kwa akili gani, yani nitunze maiti kwenye nyumba yangu nikisubiria ndugu zake!” “Si ungempeleka hospitali” “Halafu hiyo hela ya kuhifadhia maiti mtatoa nyie?” Wakawa kimya, ila wakaongezea lingine “Basi turuhusu tukamsafishe marehemu kabla ya maziko. Na tuwaite watu wa dini kwaajili ya mazishi” “Hivi nyie ndio mnamfahamu sana Moza kushinda mie, mnaijua dini ya Moza nyie? Kipindi hiki nilichoishi naye, sijawahi kumuona akienda kanisani wala msikitini. Hakuna siku aliyoongelea kanisa wala msikiti, sasa nyie mnataka kuita watu wa dini wafanye nini wakati mtu huyu alikuwa mpagani. Hebu niondoleeni ujinga mie” “Basi tukamsafishe” “Hivi mbona mnakazania sana au nyie wachawi? Maana sio kwa kukazania huko. Nitamsafisha mwenyewe” Ikabidi wawe kimya na wangoje huo muda ambao amesema wa kuzika ufike, Rose na mwanae wakaingia ndani ila watu pale msibani yani kila mtu alikuwa akiongea lake kuhusu ule msiba na mwenendo wa pale msibani. Kwenye saa sita na nusu, mzee Patrick nae alifika nyumbani kwake, ila muda huu mkewe alikuwa ndani kumbe alikuwa akijiandaa kwa maziko. Moja kwa moja alionana na Sara kwanza ambapo alimuuliza, “Maiti ya Moza iko wapi?” “Chumbani kwake baba” “Nahitaji kuiona” Patrick aliongozana na Sara hadi chumbani kwa moza, ambapo Patrick alimuomba Sara akamletee maji, wakati Sara ameondoka Patrick akatumia muda huo kuipulizia ile maiti dawa aliyoambiwa na mtu aliyekutana nae huku akisema kama itafanya kazi sawa na hata isipofanya kazi hakuwa na namna zaidi kwani alifanya vile alivyoelekezwa. Kisha alienda kuifunua ile maiti na kumpaka ile dawa puani, Sara alikuwa amerudi na kumshangaa baba yake, “Baba, unafanya nini tena?” “Unajua nilikuwa siamini kabisa kama Moza amekufa kweli, ndio nikawa namuangalia hapa” Wakasimama, muda kidogo akaja Rose ambapo alishangaa kumuona mume wake hapo, “Mchezo gani huo umeanza wa kurudi bila kusema?” “Nisamehe mke wangu, ila niliambiwa kuna msiba ndiomana nikarudi” “Haya sasa mtoke nataka kuita vijana wambebe tukazike maana wachimba kaburi washanipigia simu kuwa tayari” “Mmh mke wangu kwahiyo tunamzika kama hivyo tu?” “Ndio, tunamviringisha nguo zake tunamzika” “Mmmh mke wangu jamani, kwanini tusimwagizie jeneza!” “Sina hela za mchezo, huyu msichana hana hata mwezi halafu nianze kumgharamikia hivyo. Siwezi kwakweli wanakuja kumchukua tukazike. Kwanza nimechoka kukaa na maiti yake humu ndani kwangu” Patrick akawa anawaza ni njia gani atumie ili waweze kidogo kupeleka mbele muda wa kuzika kama alivyoombwa na Yule mtu, basi akajifanya amemuitikia pale mke wake kisha akawa anatoka akaanguka chini na kumfanya Rose aache kuwapigia simu vijana wa kuja kumbeba moza ili kuzika na kuanza kushughulika na mumewe, “Vipi tena?” "Mguu wang" “Mguu wako! Umeteguka au?” Ikabidi amshike na kumkongoja hadi chumbani kwao ambapo Patrick alionekana kulalamika kweli kuhusu mguu, ikabidi Rose amchue kwanza. Mapacha wa Rose nao walifika kwenye saa saba kwahiyo Sara alikuwa akiwapokea ndugu zake na kuwaeleza kinagaubaga kuhusu kifo cha Moza kwa uelewa wake, “Kwahiyo ulimkuta tu ndani ameshakufa?” “Ndio, ila mama kafanya vituko sana” “Ila mama yetu tunamfahamu, na watu hawa walivyojaa hapa najua ndio amechefukwa balaa” “Na amesema tunaenda kuzika muda sio mrefu” “Ila hicho kifo nina mashaka nacho hata sio cha kawaida ila wengine tukisema midomo michafu, ngoja nikae kimya tu.” Wakamsubiria mama yao pale, mzee Patrick nae alimpotezea muda Rose hadi alihakikisha saa nane inamfikia pale ndio akamuacha achukue vijana aende kuzika ila yeye alisema haendi sababu bado alikuwa na maagizo mengine aliyopewa na yule mtu kwahiyo alitaka kuyatekeleza wakienda makaburini na kubaki mwenyewe nyumbani. Rose alitoka na kutaka watu waharakishe huku akiwaelekeza maeneo ya makaburi ili waanzage kwenda, basi alichukua na vijana wakumtoa Moza mule ndani ila hata wale vijana walimshangaa Moza kwakweli alikuwa mwepesi kabisa kama hawajabeba mtu vile ingawa aliviringishwa mashuka ila bado alikuwa mwepesi sana. Wakati watu wanatoka ndio njiani wakakutana na Salome na mama yake ambao walikuwa wanaenda kwa Moza, walipoona watu wengi wengi wanatembea ikabidi waulize, “Kuna nini kwani?” “Kuna msiba, Yule msichana muongeaji. Mpenda watu amekufa” “Nani huyo?” “Anaitwa Moza” Kwakweli nguvu ziliwaisha kabisa ila ilibidi waongozane na hao watu makaburini, lakini Salome alikuwa haamini kabisa. Walifika makaburini, na wale waliobeba maiti nao walifika makaburini. Wakataka kuzika sasa, ila Salome aliwafata na kuwaomba “Naombeni hata mnionyeshe tu dada Moza nimuone kama kweli amekufa” Wale vijana wakamuangalia Rose na kumuuliza, “Eti tumruhusu amuone?” “Ametoka wapi huyo, aone nini na yeye embu atutolee balaa huko. Hakuna cha kuona, zikeni na nyie tumalize watu waende zao maana wanataka tu kushuhudia moza anavyozikwa” Kwa wakati huo Rose hakumtambua Salome kabisa kwani alikuwa na mawazo yake, kwanza kashachelewa muda wa kuzika. Wale watu walimtumbukiza Moza kwenye shimo, ila bila kutegemea Salome nae aliingia kwenye lile shimo. Ndani ya muda huo kila mmoja akistaajabu tukio la Salome, walipoenda kumchungulia Salome kwenye kaburi la Moza alionekana amekauka kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Itaendelea Jumatatu usiku……!!!!1 Kesho kuna majukumu ninayo kwahiyo kesho kutwa tutaendelea.

at 2:33 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top