KURUDI KWA MOZA: 5 Moza alienda huku akitetemeka maana aliitwa kwa nguvu sana. Alipoingia chumbani kwa Ana alizabuliwa kofi kwanza, kisha Ana akamwambia kwa ukali “Nani amekutuma univue viatu” Kabla Moza hajajibu alishtukia akizabuliwa kofi lingine lililompeleka hadi chini, yani la sasa hivi alipigwa na mtu mzima kabisa sio kofi la kitoto kama la Ana. Moza aliugulia pale chini na kusikia sauti ya Rose sasa, “Unamvuaje mwanangu viatu bila ruhusa yake?” Rose akamwongezea Moza teke, kisha akamwambia atoke mule chumbani. Moza alitoka na kwenda bafuni ambako alijikuta akilia sana huku akijiuliza, “Kwani kosa langu ni nini jamani? Hivi kumvua mtu viatu ni vibaya?” Akaitwa tena na mama mwenye nyumba, kwahiyo Moza akajifuta machozi yote na kwenda, “Unafanya nini?” “Sifanyi kitu mama” “Unanificha eeh! Hujui kama nyumbani kwangu huruhusiwi kulia bafuni?” “Nisamehe mama” “Yani wewe ni hodari sana wa kuomba msamaha, sasa nataka ukae hapa sebleni hadi hiyo saa nane usiku ifike ikukutie hapa hapa. Umenielewa?” “Ndio mama” Moza alikaa pale sebleni huku akiwa na mawazo sana, kwakweli leo hakuwa na raha kabisa alijiona yupo ufungwani. Muda kidogo, Rose na mwanae Ana wakatoka, Moza akaelewa tu kuwa nao wanaenda kula. Alikaa pale sebleni amenyong’onyea kama kamwagiwa maji. Kwenye mida ya saa tatu usiku wale mapacha walirudi na walimkuta Moza pale sebleni, walimsalimia tena na kutaka kuelekea chumbani ila mmoja akamuuliza moza “Mbona unaonekana umenyong’onyea sana” Moza akajibu bila hata kufikiria mara mbili, “Nimeunguza mboga kwa bahati mbaya” “Yani kuunguza mboga ndio unyong’onyee hivyo!” “Mama kaniambia nikae hapa hadi atakaporudi kunipa adhabu” Yule pacha mwingine akacheka na kusema, “Yani mama yetu bhana, ana vijimambo vya ajabu ajabu. Sasa mtu kuunguza mboga ndio mpaka adhabu!” Wakaondoka zao na kumuacha Moza pale sebleni, muda kidogo Sara nae alirudi na alimuuliza Moza swali lile lile aliloulizwa na wale mapacha nae akamjibu kama vile vile ila Sara alionyesha mshtuko kidogo, “Mungu wangu, umeunguza mboga? Nyumba hii haiunguzwagi mboga” “Ni bahati mbaya Sara” “Pole sana” “Asante” “Unatia huruma sana” Sara akawa anaelekea chumbani ila akaonekana anakumbuka kitu, kisha akamfata Moza na kumuuliza, “Kwahiyo mama ndio kakwambia ukae hapo sebleni hadi atakaporudi?” “Ndio kaniambia hivyo” “Kakwambia adhabu yako anakupa saa ngapi?’ “Kasema saa nane usiku” “Pole sana, nina uhakika mama na Ana watarudi hiyo saa nane muda wa adhabu ila kwa kukuokoa wewe na hiyo adhabu nenda chumbani kwako muda huu kalale yani hiyo saa nane ikukute umelala” “Mmmh mama si atasema nimekiuka amri zake?” “Moza, nimekusaidi tu ila usinitaje. Wewe nenda kalale, akikuuliza mwambie usingizi ulikushika kwa uoga. Mwambie kuwa wewe ukiogopa kitu unapatwa na usingizi” Moza aliamua kumsikiliza Sara na kwenda chumbani kwake kulala ingawa ilimchukua muda sana kupatwa na usingizi. Moza alikuwa amelala lakini usingizi wake ulikuwa umejawa uoga wa hali ya juu huku akihisi kwamba hiyo saa nane atakuja kuamshwa na kufanyiwa hiyo adhabu ila alishangaa hiyo saa nane ilionekana kupita kwani alisikia kwa mbali majogoo yakiwika na kuhisi kuwa huenda ikiwa saa tisa na nusu au saa kumi alfajiri. Usingizi ukampitia sasa, akajiona kwenye ndoto yupo kwenye kile chumba na wale wadada watano wakimshukuru sana kwa kuunguza mboga, mmoja akamwambia Moza “Ila wewe una bahati sana, kwani wenzako unafikiri makosa yetu nini kuwa huku. Ni kuunguza mboga tu” “Kuunguza mboga!” “Ndio, tuliunguza mboga tukaletwa huku. Ila wewe una bahati sana. Yani unafanya makosa makubwa zaidi yetu ila bado upo. Sikia Moza kile chumba unacholalia kuna kitabu change kidogo sana, kapekue utakiona. Kina habari za bibi yangu atakupa mbinu za kutusaidia” “Mbona huku unaongeaga wewe peke yako?” “Wenzangu wote vinywa vyao vimefungwa, hwawawezi kuongea chochote. Kuhusu mimi ukisoma kile kidaftari change utaelewa. Kipo kwenye droo, kuna taiti nyeusi katikati kuna kitabu changu” “Ila bado sijaelewa, yani kuunguza mboga ni furaha yenu ili mimi niletwe humu?” “Furaha yetu ukiunguza mboga tunakuwa huru sana, ila siku ukifikia kuunguza na kuwa kama mkaa……” Moza akashtuliwa na kelele za kuitwa, ambapo akashtuka kutoka kwenye ile ndoto, aliyekuwa anamuita ni Sara ambaye aliingia ndani na kumgusa Moza, kisha akamwambia “Kheee bado umelala tu! Amka bhana utuandalie chai unajua muda umeenda sana” Kisha Sara akatoka mule chumbani, Moza alikurupuka na kufungua dirisha ambapo aliona jua kali limeshawaka yani pameshakucha kabisa, alipotazama saa ilikuwa ni saa mbili asubuhi, “Mungu wangu, yani nimelala hadi saa hizi! Sijamuamsha Ana aende shule, sijafanya usafi bado. Mungu wangu” Alijitoa matongotongo kwa kidole kisha akatoka nje, ila sebule ilikuwa kimya sana ambapo alikuwepo Sara tu akichezea simu yake, “Nisamehe madam Sara, nilipitiwa na usingizi” “Nimekuelewa, niandalie chai tu halafu nikaangie na mayai” “Wengine wameenda wapi?” “Wote wameshaondoka” “Ana nae?” “Hebu acha kunichekesha na wewe, Ana awepo anafanya nini muda huu? Kashaenda shule” Moza akaenda jikoni na kuanza kumtaarishia Sara kifungua kinywa ila kichwa chake hakikuwa sawa kabisa, alijikuta akijiuliza maswali mengi sana bila ya majibu. Alipomaliza alimuandalia Sara mezani na kumkaribisha, ila aliona karatasi mezani na hela, akalifunua lile kafratasi limeandikwa ‘KANUNUE SAMAKI’ Sara aliposogea pale mezani akamuuliza, “Eti huu ujumbe kaacha mama” “Itakuwa ni yeye tu” Moza akamuacha Sara pale anakunywa chai kisha yeye akaenda kujiandaa ili akanunue hao samaki. Alikuwa akijiandaa huku akijiuliza maswali mengi sana ila bado hakupata majibu ya maswali yake yote, hakuna jibu alilolipata. Akawa amezubaa tu, ila akasikia sauti ya Sara ikimuaga “Tafadhali Sara naomba unisubiri ili unionyeshe tu mabucha ya samaki” “Fanya upesi, nina haraka zangu” Moza akafanya haraka akatoka na Sara, ila walipokuwa njiani Moza alimuuliza Sara “Kwani wewe unafanya kazi au unasoma?” “Kwanini umeniuliza hivyo?” “Kila siku unatoka” “Mimi nafanya kazi ila nasimamia miradi ya mama” “Na wale mapacha je!” “Nao wanasimamia miradi ya mama sehemu nyingine, na leo wametoka na mama” “Na baba je!” “Sasa nimeelewa kwanini mama anataka kukuadhibu wewe” “Kwanini?” “Hivi hujioni kuwa ni mbea sana, yani unajifanya kama FBI.” “FBI ndio nini?” “Sitaki maswali bhana, mabucha ya samaki yale pale. Kwaheri” Sara aliondoka na kumuacha Moza akielekea kwenye yale mabucha, ila moza tabia ya kuuliza maswali alikuwa nayo kwenye damu yani hata akijifanya siulizi tena anajikuta tu ameshauliza. Moza alienda kwenye bucha la samaki kununua samaki, wakati anaondoka akashikwa bega kutazama alikuwa ni Salome ambapo alimkumbatia kwa upendo, “Kheee Salome umekuwa, umekuwa sana” “Ndio dada, shikamoo” “Marahaba, upo darasa la ngapi saivi?” “Nipo kidato cha tatu” “Kheee hongera sana. Mama hajambo!” “Hajambo” “Nimewakumbuka sana, na wale wadogo zako mapacha” “Nao hawajambo” “Twende ukapafahamu ninapofanyakazi siku hizi” “Mmh dada, nitachelewa. Unajua tumehama pale tulipokuwa tunakaa” “Hakuna shida, huchelewi wewe twende ukapaone basi” Moza akaongozana na Salome hadi kwenye ile nyumba aliyokuwa anafanya kazi, na kumkaribisha Salome ndani. Kwakweli mlinzi alishikwa na bumbuwazi alipomuona Salome ila hakuweza kuuliza zaidi. Waliingia ndani, kwakweli Salome alishangaa ukubwa wa nyumba ile, “Kumbe ndiomana ulitukimbia dada, kumbe matajiri walishakuiba” “Hapana sio hivyo mdogo wangu, kipindi kile nilirudi kweli kijijini kwetu. Bibi yangu alikuwa anaumwa sana na nimemuuguza kipindi chote hiki ila mwisho wa siku alikufa. Nilikaa kijijini nikaona sina ishu nikarudi mjini, nilikuja pale mlipokuwa mnakaa nikaambiwa mmehama ila ndio nikapata kazi hii, yani hata sina siku nyingi hapa” “Pole dada” “Asante, ila umlete na mama yako hapa aje kuniona na apafahamu” Salome akamuaga Moza, na wakati anamsindikiza Mr.patrick nae akawa anaingia akawakuta ndio wanatoka wakamsalimia pale na kuondoka ila moyo wa Mr.Patrick ulihisi kitu, alijikuta akitamani sana kujua kuhusu huyo mtoto kwahiyo alikuwa anangoja Moza aingie ndani amuulize. Mlinzi nae, Moza alivyoagana tu na Salome kisha kurudi ndani akamuuliza, “Yule mtoto ni nani?” “Anaitwa salome Yule” “Mbona kafanana sana na mzee Patrick!” “Si ulisema wewe ni mtoto wa kiume, umbea hupendi. Kwaheri” Moza alienda ndani na kumuacha mlinzi ameduwaa tu, ila alipoingia sebleni tu alibambana na swali kutoka kwa mzee Patrick, “Yule mtoto ni nani?” “Anaitwa Salome Yule” “Ni mtoto wa nani na anaishi wapi?” “Nilikuwa nafanya kazi kwao kabla ya hapa” “Mbona swali na jibu haviendani? Nimekuuliza ni mtoto wa nani na anaishi wapi?” Mara mlango ulifunguliwa na aliingia Rose, ambaye alionekana kumungalia kwa hasira sana mume wake, kisha akamuuliza bila hata ya salamu “Kwanini jana hujarudi?” “Sasa ningerudi vipi mke wangu na umeniambia mpaka unipigie simu” “Sasa leo nimekupigia simu?” “Nimehisi labda umejisahau mke wangu ndiomana leo nimeamua kurudi. Jana mbu wamening’ata sana usiku pale ofisini” Rose akacheka sana, kisha akamuangalia Moza na kukunja sura, halafu akamwambia “Na wewe unasikiliza nini? Yanakuhusu haya? Hivi kwanini wewe ni mbea mbea, hebu kwenda kwenye kazi zako huko” Moza aliondoka pale sebleni na kuelekea jikoni, ila ingawa alikuwa jikoni ila masikio yote yalikuwa sbleni akisikiliza tu kinachozungumzw na Rose pamoja na Patrick. Aliwasikia vilivyo mazungumzo yao kwani hayakuwa ya kunong’ona yani yalikuwa ya sauti kabisa, “Sikia nikwambie Patrick, humu ndani kuna kidudumtu naa hicho kidududumtu lazima nikikomeshe” “Ni nani huyo?” “Si huyu mfanyakazi, yani ni mbea sijapata kuona. Ndio amefanya nisahau kukupigia simu jana, ni mbea ameshindikana, unaelewa maana ya umbea mume wangu. Huyu msichana ni mbea na lazima nimkomeshe” “Sasa unataka kumfanya nini?” “Utaona leo usiku yani akilala tu ninae” “Mmmh mke wangu yani akilala ndio unamkomesha? Kwanini usimsamehe?” “Nimsamehe! Thubutuuu, jana kaunguza mboga yangu sababu ya umbea wake. Yani leo akilala tu namkomesha” “Sasa mbona unaongea kwa sauti, huoni kama anakusikia?” “Hanisikii bhana, na leo nitamkomesha” “Halafu kama maajabu hivi, kwanini unanieleza yote hayo leo?” “Sababu nakupenda mume wangu, kila kitu ninachotaka kufanya lazima nikueleze” “Mmmh!” “Usigune mume wangu, yani huyu msichana leo akilala tu ninae. Anadhani nimesahau, twende chumbani mume wangu nikakukande kande kwa uchovu” “Kila siku ingekuwa hivi sijui ningenenepaje” “Unene mimi siupendi, twende bhana achana na mawazo hasi” Rose na mume wake walielekea chumbani huku Moza akiwa amejawa na uoga na kujilaumu kuyasikiliza yale mazungumzo, yani anawaza kuwa bora asingesikia chochote. “Mmmh mimi Moza leo silali yani silali kabisa” Alikuwa na uoga wa hali ya juu. Ana alirudi, na leo ni tofauti na siku zingine kwani begi lake alilibeba mwenyewe na kwenda kuliweka chumbani kwake, hakumuongelesha Moza kabisa. Ila muda kidogo alienda chumbani kwa mama yake, ambapo Moza kama kawaida akanyata ili akasikilize kitu ambacho Ana aliongea na dada yake. “Yani mama, huyu dada nikimuona nahisi kichefuchefu balaa kwa kitendo chake cha jana” “Hata usijali mwanangu yani huyu akilala tu leo ninae, nimepanga kumkomesha” “Mmh mama akilala? Sio akiwa macho?” “Akilala mwanangu, yani leo akilala tu ninae. Nitamkomesha leo” Kimya kikatawala na kumfanya Moza arudi jikoni huku amenyong’onyea maana leo aliona amepangiwa mapango kabambe. Huku akijisemea “Ila umbea wangu umesaidia maana mipango yote aliyonipangia huyu mama nimeijua” Kulwa, Dotto na Sara walirudi kwa kuongozana, mama yao alitoka sebleni na kumtaka Moza aandae chakula. Moza aliandaa kisha Yule mama aliita watoto wake wote na mume wake, yani leo familia nzima ilikuwa mezani wakila kasoro Moza aliambiwa akale jikoni. Wakati wanakula pacha mmoja akamwambia mama yake, “Mama ingekuwa hivi kila siku basi familia yetu ingekuwa ni kati ya familia znye furaha sana” “Hata hivyo tunafuraha, kwani hakuna mwenye furaha hapa? Mimi nafurahi sana kuwaona watoto wangu na mume wangu tukiwa pamoja tunakula” Sara akadakia na kusema, “Ila mama mmh leo sio bure, haijawahi kutokea kama hivi kwakweli. Sio bure kabisa mama” “Sasa sio bure ndio nini?” “Nahisi kuna kitu unataka kufanya” “Cha kufanya kipo ndio, kuna mjinga mmoja lazima nimkomeshe leo” “Nani huyo mama?” “Nyie kuleni tu wanangu, hata hamuhusiki” Moza bado tumbo joto hata hamu ya chakula hakuwa nayo kwani alijua hata akisinzia siku hiyo basi lazima atakomeshwa na huyu mama, na kinachomuumiza kichwa zaidi ni kuwa hajui atakomeshwaje komeshwaje. Moza akachemsha maji na kutia kahawa sababu alishawahi kusikia kuwa maji ya kahawa yanakata usingizi, alikunywa vikombe vinne ila bado alikuwa akihofia kuwa akisinzia itakuwaje. Muda wa kulala ulipofika, kila mtu alienda chumbani kwake hata Moza pia alienda chumbani kwake ila alikuwa na mawazo sana na alikuwa akiwaza ni jinsi gani anaweza kukaa macho kwa usiku wote hadi asubuhi, Ilipofika saa sita usiku akapata wazo la kwenda kukaa sebleni maana aliamini kama angekaa sebleni basi asingepata usingizi na mfano ungemnyemelea basi angeenda kunywa kahawa tena. Wakati anataka kutoka akasikia sauti, “Moza lala” Akashtuka sana na kugeuka ili aone sauti inatokea wapi, ila hakumuona mtu yoyote akataka akafungue malango tena, kasikia “Moza lala” Safari hii ile sauti ilimwambia kwa ukali kidogo. Itaendelea kesho usiku kama kawaida……….!!!!!

at 2:30 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top