KURUDI KWA MOZA: 4 Wakati anatandika kitanda cha Ana akasikia kama sauti inamwambia afunue godoro, wakati anataka kufunua mara Ana akaingia ndani na kumuuliza kwa ukali, “Unafanya nini?” Moza alipatwa na bumbuwazi tu, alishikwa na kigugumizi asiweze kujibu, mara Ana akamsogelea na kumzabua kofi. Moza alivumilia kile kibao cha Ana, ambapo Ana alimuuliza tena “Unatafuta nini huko?” Akili ya Moza ikacheza pale pale maana alitambua kuwa Ana anapenda kunyenyekewa kwahiyo alipiga magoti na kumuomba msamaha, ambapo Ana alimwambia atandike haraka haraka na aondoke chumbani kwake, Moza alifanya hivyo na kutoka. Wakati Moza anatoka chumbani kwa Ana ndio akamsikia Rose akimtoa mumewe huku akimwambia, “Na leo kakae sebleni hadi kunakucha utulinde” Ndio hapo Moza akaelewa kuwa kwanini jana yake alimkuta yule baba amejikalia sebleni tu, Moza alisikitika ila hakuwa na la kufanya hapo. Alienda moja kwa moja kwenye chumba chake huku akitafakari vitu vingi sana kwa wakati mmoja hadi alihisi akili yake inagoma kufanya kazi. Alitafakari kuhusu Ashura, akatafakari kuhusu wafanyakazi waliopita kwenye nyumba hiyo wako wapi, akatafakari kuhusu baba mwenye nyumba kwanini anateseka vile, akatafakari kuhusu Ana na chini na godoro la Ana kuna nini, mwisho wa siku alipitiwa na usingizi pale pale. Akiwa amelala, akajiona kama yupo kijijini kwao na bibi yake halafu bibi yake anamwambia, “Moza, upo kwenye ile nyumba kwa makusudi kabisa. Unatakiwa kumuokoa Yule baba, unatakiwa kumuokoa mtoto wa Yule baba, Unatakiwa kumfanya Yule mama aache kuyatenda anayoyatenda upo pale kwa makusudi. Moza mjukuu wangu, nipo na wewe siku zote usijione upo mwenyewe.Twende nikakuonyeshe sasa” Moza alishtuka na kuhema juu juu huku akijisemea, “Jamani bibi yangu si ameshakufa? Sasa namuona ndotoni kivipi? Mbona sielewi?” Usingizi wa Moza ulikata kabisa, ila alikuwa kama anasikia sauti za watu nje, akaamua kuinuka na kwenda kuchungulia dirishani, kwakweli alichungulia kwa tahadhari kubwa sana na kufanikiwa kuona vivuli vya watu vikiwa vinaishia, Moza alishtuka sana na kujikuta akihemea juu juu. Jambo hilo lilimfanya uoga umshike na usingizi akose kabisa. Kulipokucha akafanya shughuli zake kama kawaida ikiwa ni pamoja na kumuamsha Ana aende shuleni, leo Rose alionekana nyumbani kwake na kuwafanya wanae waage tu kuondoka bila kutoa oda ya chakula wanachotaka wapikiwe, hapo ndio moza akaelewa kuwa walifanya vile jana sababu walijua kuwa mama yao hayupo. Ila leo ilikuwa siku ya tofauti kidogo kwani hadi mr.Patrick aliruhusiwa kutoka, “Nenda tu kwenye shughuili zako, zunguka tani yako leo. Utarudi nyumbani pindi tu nikikupigia simu kuwa urudi” “Je usiponipigia nisirudi? Na je naweza kwenda kwa ndugu zangu?” “Ole wako Patrick, usitake nibadili mawazo.Kwanza nenda ofisini kwetu, wamekumisi sana maana ni kitambo sana hawajakuona” Mr.Patrick akaondoka zake na hakupenda kuongea sana. Baada ya muda mfupi alikuja mgeni, mgeni huyu alikuwa ni Ashura ila alijifanya kamavile hamfahamu Moza yani utadhani ni mara yake ya kwanza kumuona, kitendo ambacho Moza kilimpa shauku kubwa ya kutaka kujua kuna nini katikati. Rose na Ashura walikaa katika maongezi ila Moza alienda kukaa sehemu ambayo angewasikiliza, maana maongezi yao walifanyia sebule nyingine ambayo mara nyingi wale mapacha walifanya kama chumba chao cha kusomea vitabu. Moza alikuwa makini kabisa kusikiliza maongezi ya Rose na Ashura. “Sikia nikwambie Ashura, mi nilishakwambia sitaki Patrick ajue ukweli kuhusu Yule mtoto Salome lakini kwanini ameanza kuulizia?” “Anamuulizia hadi jina?” “Hapana, jina la mtoto halijui” “Lakini mimi dada ukweli kabisa sijamwambia wala sijawahi kukaa na shemeji Patrick kumueleza chochote kile kuhusu mtoto wake. Nadhani ni watu waliomuona Salome kuwa kafanana sana na shemeji ndio wamemwambia” “Mmh hivi kafanana nae sana eeh!” “Yani dada uongo dhambi kwakweli ila kadri Yule mtoto anavyozidi kukua ndio shemeji mtupu” “Mmh tuachane na hayo kwanza. Unajua wewe ndio unajua kila kitu kuhusu Yule mtoto. Wengine wote hawajui Ashura, mimi nimekupeleka kwenye ile familia kwa makusudi ili siri isitoke sitaki habari za Yule mtoto zisikike. Tena natamani ningekuwa na uwezo ningekimaliza kabisa” “Mmh dada usifikie huko jamani” “Sasa unadhani tutafanyaje? Nataka kuizima kabisa hii ishu maana hata ndugu wa Patrick wakijua wataleta varangati. Unafikiri mchezo, hata kumfanya huyu Ana ahisi ni mtoto wake” “Kwakweli cha kufanya sijui” “Halafu kwanini nakutafuta sikupati mpaka ukutane na wakina Sara” “Hapana dada, unajua wakina Sara walianza kuhisi kitu ndiomana nikajiweka mbali kabisa ili wasifikirie chochote” “Achana na wale watoto bhana, unajua Ashura nakutegemea sana. Huniangushagi wewe” “Ila dada kuna jambo nataka nikwambie” “Jambo lipi” “Ni kuhusu huyu mdada wa kazi uliyemuweka sasa hivi” “Eeh hebu nieleze” “Yani huyu aliwahi kufanya kazi kwa Neema, kule ninakoishi mimi na watoto wa Neema akiwepo na Salome anawajua vilivyo” “Mmmh inamaana anajua kila kitu?” “Hamjui baba wa Salome ila nina mashaka nae sana, ngoja nimuone kama ananikumbuka vizuri” Moza akasikia harufu kama mboga inaungua ikabidi akimbilie jikoni, na kweli alikuta mboga inaungua, hapo sasa wakati anahangaika iliafiche soo la kuunguza mboga akasikia Rose akiita kwa nguvu huku akitembea, “Moza, weeee Moza wewe” Moza aliitikia na kwenda, “Ulikuwa unafanya nini hadi umeunguza mboga” “Nisamehe mama” Rose akacheka kisha akamwambia Moza, “Dawa yako inachemka” Halafu akatoka na Ashura wakaondoka. Hapo Moza alikuwa na maswali mengi sana, kuwa Ashura na Rose wako vipi vipi, na kwanini Ashura alikuwa akiishi kule ambako Moza alikuwa akifanya kazi mwanzoni na mbona anaishi nao kama ndugu kivipi? “Mmmh kumbe Yule Salome ndio mtoto wa mzee Ptrick. Ila sasa naanza kupata picha, Yule Salome kweli amefanana na huyu mzee. Masikini mzee Patrick jamani, masikini na dada Neema nae jamani anaishi na nyoka ndani bila kujua dah” Kisha Moza akarudi tena jikoni, ni kweli alikuwa ameunguza mboga sababu ya kufatilia umbea. Akaanza kufanya jitihada za kuiweka sawa, akaibadilisha kwenye sufuria linguine, muda kidogo Rose alirudi na kumuita sebleni, Moza alienda “Hivi nilikwambiaje kuhusu habari za humu ndani?” “Nisizifatilie” “Haya, niambie sasa Ashura unamjua?” Hili swali lilikuwa la mtego sana kwa Moza, akajikuta akiwa kimya tu kwani hakujipanga na hakutegemea kuulizwa swali la namna ile, Rose akamuuliza tena kwa kumshtua “nijibu basi, unamfahamu vipi Ashura?” Moza akatetemeka na kujibu, “Simfahamu” Rose akacheka kisha akamwambia “Vizuri sana. Humfahamu eeh!” “Ndio simfahamu” “Na kipi kimekufanya uunguze mboga?” “Nisamehe mama” “Hivi unadhani msamaha wangu ndio unatoka kirahisi rahisi hivyo?” “Nisamehe mama” “Nadhani wewe hunijui vizuri, ila nataka unijue ili safari ijayo ujiheshimu. Msamaha wangu utaupata leo saa nane usiku” Moza akashtuka na kuuliza kwa hamaki, “Saa nane usiku!” “Ndio saa nane usiku, mbona unashtuka? Huo si muda tu kama muda mwingine. Mbona kuunguza mboga hukufikiria kuiambia mboga ikusamehe isiungue? Leo saa nane usiku utaona msamaha wangu utakavyoupata. Haya kaendelee na kazi zako, na unikaangie ndizi. Hiyo mboga ya kuungua iweke pembeni halafu saa nane usiku nitakwambia inafanywa nini ila sitaki uwape wanangu mboga ya kuungua” Moza aliondoka na kuendelea na shughuli zake huku akiulaumua umbea wake kwani ndio uliomponza hadi akaunguza mboga, na ndio uliomponza hadi anapewa msamaha saa nane usiku. Siku hiyo Ana nae aliwahi kurudi ila alionekana kuwa amechoka sana kwani alivyofika tu sebleni akalala. Ikabidi kama kawaida aende getini kuchukua begi la Ana kwa mlinzi. Alipoenda kuchukua, mlinzi alimuuliza, “Na leo Ana anaonekana kuchoka sana, ameenda wapi saa hizi?” “Amelala sebleni kwenye kochi” “Sikia sasa, cha kukusaidia. Peleka begi lake, kisha urudi kumbeba na kumpeleka chumbani kwake akalale.” Moza akamshukuru na akafanya vile, akambeba Ana na kwenda kumlaza ambapo kitandani akaamua amvue viatu kisha amwache amelala halafu yeye akatoka. Kufika sebleni wale mapacha nao walikuwa wamerudi na walimwambia Moza awaandalie chakula ila muda huo huo mama yao nae alienda pale sebleni, akamzuia Moza kuandaa chakula kisha akatoa pesa na kuwapa watoto wake, “Nendeni mkanunue na mkale mnachotaka” Wale mapacha walifurahi sana na kutoka zao, Moza alimuuliza Yule mama “Mbona umezuia nisiwaandalie chakula?” “Moza, unataka nikutukane au? Hivi mboga yako iliyoungua hiyo uwaandalie wanangu wakiumwa matumbo je!” Moza akawaza kuwa tatizo ni mboga kuungua au kuna lingine. Sara nae aliporudi ikawa vilevile, mama yake alimpa pesa akatafute chakula, kwakweli Moza aliwaza sana siku ya leo kuwa tatizo bado ni kuunguza mboga au kuna linguine, muda huu akaamua kumuuliza tena huyu mama, “Mama, tatizo ni kuunguza mboga au kuna linguine?” “Lingine lipi?” “Sijui” “Lakini unataka kujua?” “Ndio, ningependa kujua” “Wewe si mbea, utajua tu” Huyu mama aliinuka na kwenda chumbani, kwakweli Moza aliogopa ukizingatia ni kweli mboga iliungua sababu ya kufanya umbea. Moza alikuwa na mawazo sana, kitu kilichomfanya atoke na aende kwa mlinzi ili kujaribu kumdadisi kama kawaida yake, “Kaka samahani, naomba unisaidie” “Nini tena? Umefanya vituko vingine ndani?” “Nimeunguza mboga bahati mbaya kaka, ila mama kawapa watoto wake wote hela wakale nje sababu nimeunguza mboga” “Sasa wewe umekuuma nini kuwapa watoto wake hela wakale?” “Kumbuka nimepika ila amewapa watoto wake hela wakale, kwahiyo kile chakula kitamwagwa?” “Unajua katika wafanyakazi vimeo bosi aliowahi kuwaleta, basi wewe ni kimeo namba moja. Kwa kifupi, hii nyumba haiunguzwagi mboga, yani kama umeunguza mboga leo ujipange” Moza alizidi kupatwa na uoga, mara akaitwa na mama mwenye nyumba alikuwa mlangoni, Moza akaenda kisha Yule mama akamuuliza “Na leo ulikuwa unaulizia masoko?” “Hapana” “Ila ulikuwa unaulizia nini?” Moza akawa kimya tu, na kumfanya Yule mama aongee tena “Wewe Moza wewe yani nitakachokufanya leo hutakaa kusubiria umbea tena, akili itakukaa sawa. Nitakukomesha” “Ila mama nimekuomba msamaha” “Unadhani huo msamaha wako ndio umenunua mboga? Huo msamaha wako ndio hela? Nakwambia nitakukomesha” “Mama nina ombi” “Eeeh ombi gani?” “Naomba kurudi kwetu” Rose akacheka sana, na kumuangalia Moza kisha akamwambia “Yani wewe hata mwezi huna kwenye nyumba hii unataka kurudi kwenu, tena baada ya kufanya makosa. Hivi unafikiri kuondoka hapa ni rahisi kiasi hicho? Mboga yangu uliyounguza una hela ya kunilipa? Nijibu sasa” Kabla hajajibu alimsikia Ana akimuita kwa nguvu sana, “Mozaaa” Rose alimuangalia Moza na kumsonya kisha akamwambia “Nenda huko, malkia anakuita” Moza alienda huku akitetemeka maana aliitwa kwa nguvu sana. Alipoingia chumbani kwa Ana alizabuliwa kofi kwanza, kisha Ana akamwambia kwa ukali “Nani amekutuma univue viatu” Kabla Moza hajajibu alishtukia akizabuliwa kofi lingine lililompeleka hadi chini, yani la sasa hivi alipigwa na mtu mzima kabisa sio kofi la kitoto kama la Ana. Itaendelea kesho usiku kama kawaida……….!!!!!!

at 2:30 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top