KURUDI KWA MOZA: 24 Salome alimpisha huku akicheka sana, Rose alikuwa na hasira sana na alijiuliza kama dawa itafanya kazi kama alivyoambiwa na mganga maana kashakosea masharti na kuongea wakati aliambiwa asiongee chochote. Aliingia na Yule mlinzi kwenye chumba cha Moza na kumuweka kitandani, kisha yeye akainuka na kuanza kuvua nguo zake ila alipomaliza tu kutazama kitandani hakumuona mtu yeyote. Mlinzi alikuwa ametoweka, kitendo hiki kilimshtua sana Rose na kumfanya achukue nguo zake haraka haraka na kuvaa kisha kukimbia kutoka kwenye kile chumba cha Moza, ila kwenye korido akakutana na Salome yani muda huu hakuweza hata kuongea na Salome zaidi ya kukimbilia nje alipo mtoto wake, Salomealicheka sana kisha akaenda kukaa sebleni na kuwaangoja Rose na mwanae watakavyorudi tena ndani. Basi Rose alifika alipo mwanae Ana kwenye kile kijumba cha mlinzi, Ana alimuuliza mama yake, “Tayari mama?” “Tayari nini mwanangu? Mambo yameharibika” “Kivipi?” Mara geti lilifunguliwa halafu wakamuona mlinzi ambaye aliingia na kwenda kufungua geti kubwa na liliingia gari la Patrick. Rose alishtuka sana na kufikicha macho yake kwani alihisi ni kiini macho. Alimshika mwanae mkono na kumpakiza kwenye gari kisha akaondoa gari nje hata mlinzi na Patrick walikuwa wakishangaa ila Patrick alihisi kuwa Rose anamkimbia kwani anajua kuwa anaujua ukweli wa mambo yote sasa. Patrick na mlinzi waliingia ndani na kumuta Salome, kwakweli Salome alimpongeza sana Patrick kwani aliona jinsi alivyomfanyia kazi yake kuwa rahisi kwa siku hiyo, kisha akamkaribisha Patrick pale ndani, “Karibu tena kwenye nyumba yako” “Ni kweli hii ni nyumba yangu mwanangu, ila sina hamu nayo na siwezi kuishi humu tena” “Kwanini?” “Sijisikii tena kuishi na mwanamke shetani kama Rose, nilimuacha mke wangu mpole, mzuri na mcha Mungu Neema, aliyenipenda kwa dhati. Lakini nilimuhisi vibaya kwa makosa ya kusingiziwa, kumbe alisingiziwa kila kitu juu yake. Ashura ni ndugu wa mama yako ila ni mtu mbaya sana” “Hapana Ashura hakuwa ndugu wa mama” “Kivipi hakuwa ndugu yake na wakati alikuwa akiishi nae?” “Niambie kwanza Ashura ni mtu mbaya kivipi na nitakueleza ni namana gani hakuwa na undugu na mama” Patrick alianza kumueleza kwa kifupi jinsi ilivyofikia hadi kuachana na mama yake, “Sikia, sikuwa namjua Ashura ila nilikutana nae nyumbani kwa Rose na alitambulishwa kwangu kama msichana wa kazi wa Rose, wakati tunamuongelea mke wangu basi Yule Ashura alidai ya kwamba anamfahamu yani yeye na Neema wamechangia baba. Na akaanza kunieleza kuhusu historia ya Neema, anasema Neema alianza uhuni mapema sana toka yupo darasa la tano na ametoa mimba nyingi sana, ingawa mimi nilimuoa mapema pia ila hakuweza kunizalia sababu kizazi chake hakikuwa na uwezo wa kuzaa maana katoa mimba sana. Ndiomana sikuona umuhimu tena wa kuendelea na Neema wakati ukweli nimeujua. Niliporudi kwa Neema nilikuwa na lengo moja tu la kumuacha kwani mawazo yangu kwa muda huo yalikuwa ni kuanzisha maisha na Rose. Ila Neema aliweza kunishawishi hadi tukashiriki nae tendo la ndoa, na baada ya hapo nikaondoka ila nikapata shinikizo la kumfukuza kwani niliambiwa Neema alikuwa na mahusiano na kijana Fulani pale mtaani, na nikambamba akiongea nae kwakweli nilikuwa na hasira sana nikamfukuza kabisa. Nikashangaa baada ya mwaka mama ananiambia eti kuna mtoto nimezaa na Neema, sikuamini. Kuna moyo mwingine ulikubali lakini niliendelea kujazwa ujinga kuwa haiwezekani lazima mimba ile ilikuwa ya mtu mwingine kwahiyo nisijihusishe na huyo mtoto. Sikutaka kujihusisha kweli, ila niliamini zaidi baada ya kuona Neema akiishi na Ashura, hapo ndio nikajua ni ndugu yake.” “Pole sana, hizo zote ni mbinu za Rose. Neema hakuwa na undugu wowote na Ashura ila kuna mipango ilipangwa ndiomana ikawa hivyo na utaelewa tu” “Ila wewe nae unanishangaza, mara nyingine unamuongelea Neema kamavile sio mama yako nan i mtu uliyekuwa nae labda sawa” “Usijali kuhusu kuongea kwangu, huwa naongea ili mtu anielewe, ila huyu mlinzi amefanya kazi nzuri sana” Salome akamuita Yule mlinzi na kuwaandalia chakula mezani. Kisha akawakaribisha mezani Patrick na mlinzi wale chakula, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mlinzi kula ndani ya ile nyumba. Wakina Sara walifikishwa na Jesca kwa mkaka ambaye anasadikika kuwa alimbeba Salome wakati ameanguka kaburini, waliweza kufika baada ya Yule Jesca kuwaunganisha na Yule ambaye alikuwa akimjua vizuri Yule dereva. Walifika na kusalimiana kisha wakaanza maongezi ya hapa na pale na haswa ni kuulizia kuhusu Salome, “Jamani hata mimi mwenyewe sielewi, Yule mtoto alikuwa na mama yake kwenye gari na mama yake alikuwa akilia sana, gafla nilisikia akiongea na mama yake na muda kidogo mama yake akaniambia kuwa tusiende tena hospitali bali twende nyumbani kwao. Basi nilifanya hivyo kwa kuwapeleka nyumbani kwao” “Mmmh kwahiyo hujui alizindukaje zindukaje. Wewe si ulimbeba na uliiona hali yake?” “Ni kweli nilimbeba na alikuwa kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme tena nilijua amekufa yani nilikuwa naenda nao tu hospitali ila nilikuwa najua lazima tutaambiwa kuwa amekufa. Hata mimi nilipomsikia anaongea tena akiwa mzima kabisa nilishtuka sana” “Mmmh inabidi tukaongee na mama yake, lazima kuna kitu anakijua. Unapajua kwao?” “Napakumbuka vizuri sana, kwa tukio kama lile lazima nikumbuke kwao ni wapi” Basi wale kaka wa Sara wakamuomba huyu dereva awapeleke kwao na Salome ili wakaongee na mama yake kwani kuna kitu walianza kuhisi kuwa hakipo sawa na Salome na walihisi kuwa wakiongea na mama yake wataujua ukweli wa mambo yote. Basi safari ikaanza ya kuelekea kwakina Salome, na kweli walifika ila kwa bahati mbaya ilikuwa ni kwakina Salome kwa zamani na hakuna hata mmoja pale mtaani aliyejua nyumba mpya waliohamia wakina Salome, na waliambiwa ni kitambo sana wamehama. Ikabidi waachane pale na kila mmoja kuelekea sehemu yake, ambapo wale mapacha na dada yao waliamua kurudi tu nyumbani kwani siku ya leo hakuna walichofanya zaidi ya kufatilia mambo hayo. “Ila mnakumbuka kuwa mama alisema tusirudi mpaka atupigie simu” “Sasa mpaka saa hizi jamani, saa mbili hii labda mama kasahau. Tumpigie tu simu sisi wenyewe” Wakaamua kumpigia simu mama yao ila simu ya mama yao iliita bila ya kupokelewa ikabidi wakubaliane tu kurudi nyumbani. Rose na Ana waliamua kwenda hotelini kwanza kutuliza akili, Rose alianza kuongea na mtoto wake jinsi ndani ya nyumba alivyopatwa na mauzauza, “Ila mama si ungejitahii usiongee!” “Mwanangu, ningewezaje kujitahidi kufanya hivyo? Ilihali nishakwambia hali halisi ilivyokuwa. Yule mwehu alikuwa ananizuia mlangoni, yani Yule mtoto sijui katumwa Yule loh!” “Sasa mama tutafanyaje? Ni kurui kwa Yule mganga au?” “Ndio, hakuna jinsi zaidi ya kurudi kwa Yule mganga tu” “Kwahiyo mama usiku wetu wa leo tutamalizia humu hotelini?” “Ndio, hakuna namna mwanangu” “Hapana mama turudi nyumbani, hatutakiwi kuwa waoga kiasi hicho kwenye nyumba yetu wenyewe. Turudi nyumbani mama, yani ni nyumbani tu ndiko tunakoweza kufanya hata dawa zetu zikafanyika, ila huku hotelini tutachukua muda mrefu sana kufanya mambo yetu” Ana akatumia muda mrefu sana kumshawishi mama yake ili aweze kukubali warudi nyumbani na hatimaye akakubaliana na Ana, kisha wakaagiza chakula kwanza na kula halafu ndio safari ya kurudi nyumbani ikafatia ingawa ilikuwa ni usiku tayari. Salome alikuwa nyumbani ila Leo aliongea sana na Patrick pamoja na yule mlinzi, kisha Patrick akataka kuondoka tena ila muda huu Salome alimruhusu kuondoka kiasi cha mlinzi kushangaa kuwa imekuwaje tena wakati alimpa hadi hela kuwa amlazimishe mzee huyo warudi nae nyumbani, sasa iweje amruhusu kuondoka tena ila hakutaka kuhoji zaidi. Kisha yule mlinzi alirudi getini halafu nae Patrick alienda kupanda gari yake na kuondoka zake. Basi mlinzi akiwa amekaa pale karibu na geti, Salome alienda na kumuuliza maswali, "Hivi kifo cha Moza, wewe umekionaje onaje au unahisi kama ni kitu gani?" "Mimi nahisi kamavile ni kifo cha kimazingara maana sukuelewa mwanzo wala mwisho" "Na Moza mwenyewe ulikuwa unamuonaje?" "Sijui niseme nini ila nakiri wazi kuwa nilimpenda" "Mbona hukumwambia?" "Ningemwambiaje vile alivyokuwa anafanya mambo anayopenda yeye, ila nilitaka kumwambia hivyo hivyo sema umauti tu ndio umeharibu mambo" "Je unaamini kama Moza amekufa kweli?" "Hata Sijui niamini au, ila kama hajafa kweli basi atakuwa wapi yani najiuliza bila jibu" "Mbona mimi unanijibu kila ninachokuuliza tofauti na Moza ulimwambia hupendi umbea" Mlinzi akacheka kidogo na kujibu, "Hela hii yani hela inafanya mtu hadi aongee ya ndani, mbona na wewe unaniuliza bila kujali kuwa ni usiku sasa?" Kabla hajajibu, waliwasili wale mapacha pamoja na dada yao Sara. Ila baada ya salamu tu, Salome aliwakaribisha nao ndani hata wakashangaa kuwa Leo inakuwaje wanakaribishwa kwenye nyumba yao wenyewe, wakaingia ndani na kumuuliza Salome kama mama yao alirudi, “Bado hajarui, kwani mmeshawasiliana nae?” “Hapana, hapokei simu” “Basi, na mimi sijamuona kurudi” Kila mmoja aliendelea na shughuli zake nyingine pale nyumbani kwao kama kula halafu kwenda chumbani kila mmoja, ila Salome alikuwepo pale pale sebleni siku hiyo maana hakwenda kabisa chumbani kwake kule. Kwenye mida ya saa tano usiku, Rose na mwanae Ana walirudi na kumkuta Salome pale sebleni ila hawakuongea nae kitu chochote kile zaidi ya kupitiliza na kwenda vyumbani mwao. Rose aliingia chumbani kwake akihisi kwamba Patrick atamkuta maana alimuona akirudi ila alijiuliza kitu, “Inawezekana akawa Patrick wa mazingaombwe Yule. Mlinzi mwenyewe hata kumsalimia namuogopa maana sina hakika kama ni yeye kweli” Akaenda kuoga kisha akarudi, ila leo akakumbuka dawa zake ambazo huwa zinamsaiia kumtoa uoga kabisa, na mara nyingi huzitumia kama anataka kufanya tukio la tofauti ili asipatwe na uoga. Sasa kutokana na matukio ya siku hiyo na yale ya siku za karibuni akaona ni vyema kuchukua hiyo dawa yake na kuanza kuichoma, kwahiyo akachukua kiberiti na kuanza kuwasha dawa zake hizo ambapo harufu ya dawa zile ilienea nyumba nzima. Mara akasikia mlango wake ukigongwa, akainuka na kwenda kufungua, akamkuta Salome mlangoni akionyesha kujawa na hasira halafu akamwambia, “Zima hizo dawa zako” “Nizime ili iweje? Kwani wewe zinakusumbua nini?” “Sizitaki zinaniumiza kichwa, nimekwambia zima” “Wewe mtoto usinitishie maisha, kwanza umeharibu sana mfumo mzima wa maisha yangu halafu saivi unajifanya unajua kila kitu. Dawa hizi sizimi na utanitambua baada ya kumaliza kuchoma hizi dawa” “Unasema huzimi?” “Ndio sizimi” “Unajiamini kabisa?” “Najiamini ndio na sizimi, usinibabaishe” Rose akafunga mlango wake kwa nguvu kwani aliona kamavile Salome anampigia makelele tu, kisha akarui na kuendelea kuchoma dawa zake ambazo kwa yeye zilikuwa zinmburudisha sana na alikuwa anajisikia vyema moyoni ila ile dawa ilikuwa inawaumiza sana watu aliowafungia kwenye chumba chake na ndiomana Salome hakuitaka maana aliweza kuyahisi maumivu waliyoyapata watu wale. Rose akiwa amestarehe kabisa na dawa zake, huku amezishika akizichoma gafla alihisi kama kuna mtu amekuja na kuzizima, alipoangalia vizuri alimuona Salome. Rose akashtuka kidogo kisha alimuuliza Salome, “Hivi wewe ni mchawi? Umeingiaje humu?” “Dawa imeanza kukupa ujasiri eeh!” “Nijibu umeingiaje?” “Kama ambavyo wewe huingiaga kwenye vyumba vya watu vikiwa vimefungwa” “Wewe ni mchawi” “Hapana mimi si mchawi” Gafla Rose akainuliwa na nguvu ya ajabu yani alikuwa kama yupo juu akimtazama Salome kwa chini na mara akaona kama macho ya Salome yakiwaka waka taa, kwa mara ya kwanza Rose alishikwa na uoga kiasi na kutaka kupiga kelele ila alihisi kama akizibwa mdomo na hapo hapo akapata jibu kuwa mtu pekee anayewasumbua kwenye nyumba ile si Moza bali ni Salome, yeye alihisi kuwa Moza ameshakufa ila Salome ana nguvu za kichawi ndio anawasumbua. Kitu kilichomshangaza kuhusu Salome kuwa ni mchawi wa aina gani ambaye hatambuliki na wachawi wengine. Mdomo wa Rose ulikuwa umezibwa na akaamua awe mpole, alimuomba jambo moja tu Salome, “Niruhusu hata nikalale sebleni kwa siku ya leo” “Kwani unaogopa? Wewe ni jasiri, unatoa wapi uoga wa namna hiyo? Kama umeweza kufuga watu na hawafurukuti kwako unawezaje kumuogopa mtu kama mimi?” Rose alikuwa kimya tu akitetemeka kwani ukweli ni kuwa uoga ulimshika vilivyo. “Muda wa kufanya uwanga wako unafika? Unajua matatizo ya uchawi wa kununua? Utakudhuru mwenyewe tu. Haya toka ukalale sebleni” Akajikuta tu ameachiwa na kuanguka kisha akainuka upesi na kuanza kutoka chumbani kwake kwa uoga na kufanya haraka haraka, kufika sebleni akamkuta Salome amekaa kwenye kochi, hapo ndipo akili yake ikapoteza dira kabisa. Itaendelea kesho usiku…….!!!!!! By, Atuganile Mwakalile.

at 4:45 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top