KURUDI KWA MOZA: 18 Rose akaenda zake sebleni na baada ya muda watoto wake walianza kurudi na wote wakawa pale sebleni na kuzisikia kelele za Sara kuwa afunguliwe, wale mapacha walimuhurumia sana dada yao, “Mama jamani, msamehe dada Sara, nadhani hatorudia tena” “Hebu na nyie niacheni” Gafla ikasikika sauti kali sana ya kelele za Sara ikisema, “Mozaaaaaaaaa” Na gafla kukawa kimya kabisa. Kitendo hicho kiliwashtua wote sebleni hata Rose mwenyewe akashtuka na kujikuta akienda kumfungulia Sara ili kujua tatizo ni nini, ila alipomfungulia alimuona Sara akiwa ameanguka chini na kuzimia, kwakweli Rose alichanganyikiwa sana kwani hakudhania kama mwanae kumfungia mule chumbani angezimia basi akamuinua mwenyewe na kumbeba hadi sebleni kisha akawaambia wale mapacha wasaidiane nae kumpepea hata wao wakashangaa kuwa mama yao kuna wakati kumbe anakuwa na huruma dhidi yao. Ana alimwambia mama yake, “Unajichosha bure mama” “Ni mwanangu huyu” Ana akaondoka zake huku Rose akiendelea na wale mapacha wake kumpepea Sara, na ilimchukua muda sana kuzinduka na hata alipozinduka hakukumbuka kitu chochote yani cha kushangaza hata kuhusu kuanguka kwa Ommy na kutoweka hakukumbuka pia. Rose alimsogelea mwanae na kumpa pole kisha akainuka nae na kwenda chumbani, akakaa nae kuzungumza, “Mwanangu una hakika hukumbuki chochote?” “Sikumbuki kitu mama” “Yani vilivyofanyika leo hukumbuki?” “Yani sikumbuki hata kuhusu leo nilitoka nimejua wewe ulivyosema ila sikumbuki chochote” “Kheee makubwa haya, hivi anayefanya kutoa kumbukumbu kwa watu wangu wa karibu ni nani!” Akakumbuka kuwa kauli ya mwisho ya mwanae kabla ya kuzimia ilikuwa ni neno ‘Moza’ na ilionyesha aliona kitu cha kustaajabisha sana ila akajiuliza kuwa inamaana huyo Moza karudi kama mzimu au ni kitu gani. “Ila inawezekana maana alitoweka pale makaburini na hatukumzika. Lazima nifatilie na nijue mbichi na mbivu” Akapanga pale na halmashauri ya kichwa chake kuwa kesho aende kwa mtaalamu mwingine ili kujua ukweli kuhusu Moza maana kitendo cha mtoto wake kusema Moza na kuzimia halafu kupoteza kumbukumbu zote kilimstaajabisha ingawa kilimfurahisha kwa kiasi Fulani kwani mwanae hakuwa na kumbukumbu za kupotea kwa Ommy. Alimuangalia pale mtoto wake aliyeonyesha kuwa hana kumbukumbu ya aina yoyote kisha akaondoka na kumuaga pale. “Mwanangu naenda chumbani, ikiwa utapatwa na tatizo lolote usisite kuniambia. Sawa mwanangu eeh!” “Sawa mama” Rose alitoka ila Sara alibaki akijiuliza sana upendo wa mama yake wa siku hiyo ni waajabu sana ukizingatia na siku zingine. Kaka zake mapacha nao wakaenda chumbani kwake na kumuuliza tena dada yao hali yake ila bado walimshangaa kuwa hana kumbukumbu ya aina yoyote. “Yani dada hukumbuki kitu chochote!” “Sikumbuki ndio, kwani ilikuwaje?” “Sisi wenyewe hatuelewi ila tulisikia tu ukipiga kelele kuwa ufunguliwe na mara ukapiga kelele za nguvu ukitaja Moza, halafu kimya kikatawala. Mama alikuja kukufungulia na kukuta umezimia ndio akakuleta sebleni tukupepee” “Kheee mama alinibeba pekeyake?” “Ndio alikubeba peke yake” “Mama amewezaje kunibeba peke yake jamani wakati anasemaga siku hizi nimenenepa sana, amewezaje kunibeba peke yake nikiwa mzito hivi!” “Yule ni mama, ametubeba wakati watoto na anaweza kutubeba hata sasa” “Mmh jamani kaka zangu, ni mama kweli sijakataa. Katubeba wakati watoto, sijakataa lakini kumbukeni utotoni tulikuwa wadogo ila kadri tunavyokua na uzito nao unaongezeka. Mama angembeba mtu kama Ana sawa ila sio mimi na ubonge huu, yani hata nyie hamjapata mashaka. Sikumbuki kitu ila swala la kusema mama alinibeba peke yake limenishtua kidogo” “Mmmh basi tuachane na habari hizo dada, cha muhimu unaendelea vizuri” Kaka zake nao waliondoka na kumuacha mule chumbani. Usiku wake Sara alikuwa amelala ila akajiwa na njozi kuwa Ommy yupo mahali anateseka sana huku akimuomba Sara msaada aokolewe, “Nisaidie Sara, nateseka naumia kwa kosa nisilolijua. Nisaidie Sara” “Uko wapi kwani?” Sara akashtuka na swali lake hilo, jasho likawa linamtoka tu ingawa chumbani kule feni ilikuwa inawaka. Alikaa na kujaribu kufikiria sana kuwa Ommy amepatwa na nini ila hakuelewa, akaamua achukue simu na kumpigia Ommy ila hiyo simu ilipoanza kuita aliiona chumbani kwake na kushangaa kuwa simu ya Ommy ipo chumbani kwake, hakuelewa imekuwaje hadi simu ipo pale na ni nani aliyeiingiza ile simu chumbani kwake. Akachukua simu ya Ommy na kuanza kuipitia kwani kwa upande mwingine alifurahi kuona simu ya Ommy kuwa ataweza kuona meseji zake. Na kweli alipochukua simu ya Ommy tu alibambana na ujumbe kutoka kwa Mishi, ujumbe ulikuwa unasema, “Mpenzi wangu Ommy uko wapi jamani? Nimekumisi sana, mpaka muda huu kweli hujaja! Nakupenda sana mpenzi wangu” Sara alijikuta akiumia moyo kupita maelezo ya kawaida, roho ya wivu iliingia ndani kwake na hapo akajikuta akisahau kabisa kama ameota kuwa Ommy yupo kwenye matatizo zaidi kilichomuuma ni kusalitiwa na Ommy basi, akajikuta akimjibu huyu Mishi, “Usinisumbue nipo kwa mwanamke wa maisha yangu Sara. Nampenda sana” Akatumia hiyo meseji ila moyo wangu ulijawa na wivu kiasi kwamba alijikuta akishindwa hata kulala, “Yani huyu Ommy nampenda kwa moyo wwangu wote, hakuna chochote anachonipa ila mimi nampa upendo. Shida yoyote kiipata namsaidia. Kila kitu nampa, eti leo ananisaliti na mwanamke sijui wa kuitwa Mishi! Lazima nimjue huyo mwanamke nijue tofauti ya mimi na yeye ni nini kwani mimi nina ubaya gani wa kuchanganywa kimapenzi na mwanamke mingine! Yani wanaume hawa” Alijikuta machozi yakimtoka tu na hakupata usingizi hadi kunakucha, wazo lake lilikuwa moja tu la kwenda kumtafuta Mishi ili ajue ni kwanini Ommy amemsaliti kwa huyo mwanamke. Rose siku ya leo alijiandaa kwenda kwa mganga wa kienyeji kwani bado swala la kupotelewa kwa pesa yake lilimuumiza sana na alitaka kujua huyo anayewatoa kumbukumbu familia yake bila yay eye mwenyewe kujua. Alimsihi mume wake asitoke kabisa siku ya leo, “Tafadhali usiende popote” “Sawa, sitaenda popote” “Nitakuagizia mtu wa kukuletea chakula, tafadhali leo usitoke. Narudia tena na tena tafadhali sana leo usitoke” “Nimekuelewa mke wangu sitatoka” “Na Yule panya ambaye jana hajarudi, sitaki uende kumtafuta wala sitaki umkaribishe hapa tena” “Panya gani huyo?” “Si huyo shetani wa kuitwa Salome, simtaki katika nyumba yangu. Tafadhali Patrick huyo mtoto simtaki, usitake kabisa kunikera” “Nimekuelewa mke wangu, sitafanya kinyume chako” Rose akatoka na safari yake ikaanza ila alipitia kwanza shuleni na kumuacha mwanae Ana shuleni kisha yeye akaenda na safari yake ya kumtafuta mganga, akiwa njiani akaanza kuwaza jinsi hela zake zilivyopotea kizembe halafu jinsi mume wake akiwa hana kumbukumbu yoyote kuhusu alipozipeleka hizo pesa yani aliwaza sana, ila gafla alifunga breki ya gari kwani mbele yake aliona begi jeusi likiwa na mfanano wa lile lile begi ambalo aliliweka kwenye gari yake na mumewe akaondoka nalo. Rose alishuka kwenda kuliangalia, akasogea na kulichukua kisha akapanda nalo kwenye gari yake na kulifungua, alishangaa kuona pesa nyingi, kwakweli alishangaa sana na kujiuliza, “Sio begi langu kweli hili? Ndio lenyewe bhana” Alilifunga na kuweka pembezoni mwake kisha akacheka, “Yani wamesikia naenda kwa mtaalamu wamerudisha begi, atakuwa kiboko sana Yule ninayemuendea. Na wala sirudi, naenda tu nimkomeshe huyo kidudu mtu asiyejulikana anayesumbua familia yangu” Akawasha gari yake na kuendelea na safari. Sara aliwasiliana na Mishi kwa njia ya ujumbe na kujifanya ni Ommy huku akimuomba msamaha kwa kauli ya jana yake, nia yake kubwa ilikuwa ni kumuona huyo Mishi anafananaje. Alifika hadi eneo alilopanga kukutana na huyo Mishi na akabahatika kumuona kabla Mishi hjamuona yeye, hasira zilimpata yani muda huo hata hakutaka kujua kuwa Ommy yuko wapi au kitu gani kimemkuta ila yeye alikuwa akiumizwa na wivu tu muda huo. Alitamani aende amsogelee huyo Mishi na amuanzishie varangati ikiwezekana amdunde maana alijiona yeye ni bonge ni Mishi ni mwembamba kwahiyo alihisi kuwa angemudu kumdunda ila kabla hajaenda kufanya chochote alishangaa akishikwa bega, kugeuka nyuma alishangaa sana maana alimuona Salome, “Kheeee Salome! Unafanya nini hapa?” “Nikuulize wewe dada unafanya nini hapa?” “Kuna mtu nilikuwa namsubiri maeneo haya” “Mmmh dada wakati ulikuwa unampango wa kwenda kupigana na Yule dada wa kuitwa Mishi” “Umejuaje?” “Najua tu, katu usipende kuruhusu mapenzi yakakutawala hivyo dada yangu hadi ushindwe kufanya vitu vyako vya maana” “Sikuelewi Salome” “Mapenzi yapo tu na siku zote yatakuwepo ila heshima yako ni kubwa sana kuliko hayo mapenzi, mfano ukaenda na kupigana na Yule Mishi akakupiga itakuwaje? Si aibu hiyo mtu bonge kupigwa na kimbau mbau. Na mfano ukaenda mkapigana weee ila ashishinde yoyote itakuwaje? Ni kujidhalilisha huko, na mfano ukaenda kupigana na mtoto wa watu bahati mbaya akaanguka na kufa, huoni kama utapata kesi ya kujibu! Dadangu usitake mapenzi yakutawale kiasi hiko, tafadhali twende nyumbani” Maneno ya Salome yalimuingia akilini Sara kwa kiasi chake, na kujikuta akitoa wazo la kutaka kwenda kupigana na Mishi badala yake kugeuza na Salome na kurudi nyumbani. Walifika nyumbani na moja kwa moja Sara alienda chumbani kwake ambapo Salome alimfuata kwa nyuma, Sara alifika na kulia sana ila Salome alikuwa akimuangalia tu. Sara alilia sana kuhusu mapenzi ila alipotulia kiasi Salome alisogea na kumbembeleza. Sara alimuangalia Salome, “Wewe ni mtoto mdogo, mapenzi huyajui vizuri” “Mimi ni mtoto kwa kuniangalia ila sio mtoto kivile unavyonifikiria. Nimekuacha ulie ili utoe uchungu wako, dada yangu narudia tena usipende mapenzi yakutawale” “Ila kwanini Ommy anifanyie hivi? Kwanini Ommy anisaliti?” “Ila dada jamani mara nyingine unaweza kumlaumu bure huyo Ommy ingawa ni kweli ana makosa, Ommy anakupenda sana na alitaka kukuoa ila mama yako hataki hata kunuona akikusogelea, mama yako hataki hata upate muda wa kwenda kuonana na Ommy. Jamani nae ni binadamu anamatamanio jamani” “Khabari za Ommy wewe umezijuaje?” “Usiniulize tu habari za Ommy nimezijuaje bali niulize pia habari za Mishi nimezijuaje, ila nakwambia tena usiruhusu mapenzi yakutawale kiasi hicho. Ommy ni binadamu kama binadamu wengine, si malaika Yule kusema atakuwa sahihi kwenye kila kitu” “Unasema tu kwasababu huyajui mapenzi, simtaki tena Ommy. Sitaki hata kumuona, akaendelea na hiko kimishi chake si kaniona mimi bonge sifai” “Hizo ni hasira Sara, tena hasira ni hasara. Hapo ulipo hata hujui Ommy yuko wapi ila unasema hutaki tena kumuona” “Sitaki ndio, sitaki kujua hata alipo” “Ila moyo unakuuma, jambo lolote usilitafutie jawabu wewe mwenyewe. Ni Ommy pekee anayeweza kukujibu kati yako wewe na Mishi anampenda nani. Tunatakiwa tufanye jitihada za kumrudisha Ommy” “Kumrudisha kwani yuko wapi?” “Ngoja nikuache ulale kidogo ila ukiamka utakuwa na kumbukumbu zote kuhusu Ommy” Sara alimshangaa sana Salome ila Salome alimuaga saran a kumuacha mule chumbani kisha yeye akatoka zake. Rose alifika kwa mganga wake na kukuta watu wengi sana kwenye foleni ila alishangaa akiitwa yeye ndani na kuwapita wote kwenye foleni huku wengine wakilalamika, “Sababu kaja na gari, yani waganga wanapenda matajiri sababu wanajua wanahela” Rose alitembea kwa madaha sana na kuingia kwenye kibanda cha mganga ila alishangaa kuona kibanda kile kikiwa tofauti na kwa waganga alipopazoea, na cha kushangaza alikaribishwa na sauti ya kike. Rose alikaa lakini alikuwa na wasiwasi mwingi sana, kulikuwa na mwanamke kajifunika na khanga mbele yake, mganga aliyemfata hapo ni mwanaume kwahiyo kitendo cha kuona mwanamke amekaa hapo kilimshangaza sana. Na kujikuta hata ameshindwa kusema chochote, “Elezea matatizo yako” Rose alishtushwa na sauti ya huyu mganga kwani ilikuwa ni sauti ya mtu anayemfahamu, akajikuta akisema kwa mshangao, “Mozaa!!!” Yule mganga alifunua sura yake na kumfanya Rose ashtuke zaidi kwani ni kweli alikuwa ni Moza. Itaendelea kesho usiku……!!!!!! Jamani, poleni sana mliokumbwa na mafuriko. By, Atuganile Mwakalile.

at 11:00 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top