KURUDI KWA MOZA: 14 Basi Salome akachukua dawa na kunyunyiza kwenye macho ya Sara, na hapo hapo Sara akafikicha macho yake na kuona ila alipoinua macho vizuri ili amtazame aliyemsaidia alishtuka sana na kusema kwa nguvu, “Kheee Moza!” Sara alikuwa akihema juu juu na muda kidogo akazimia ila Salome akammwagia maji na kuzinduka, Sara akawa anamuangalia Salome sasa, na kumuuliza “Mara ya mwisho nilikuona na Moza eeh!!” “Ndio nilikuwa na Moza” “Ila mbona wakati ule nilipoanza kuona nimekuona kama Moza!” “Sijui, labda mawazo yako unamfikiria Moza” “Inawezekana, ila asante kwa kunisaidia maana nilihisi ndio mwisho wangu” “Usijali, sikuweza kuvumilia ilihali najua unateseka ingawa nataka hapa niletwe na mama yangu” “Aaah unataka kuja kuishi hapa eeeh!” “Ndio si kwa baba yangu, nataka niishi na baba yangu” “Karibu sana, hivi unaitwaga nani vile maana mimi najua jina la Maria ndio alikuwa mtoto wa baba ila Moza alisema jina lingine” “Naitwa Salome ingawa sijui ni kwanini walinibadilisha jina” “Na umejuaje kama baba ni baba yako?” “Siku nyingi sana nilitamani kumjua baba yangu, ila sasa nimemjua ni furaha kubwa sana kwangu. Je wewe unatambua chochote kuwa kwanini walinificha nisijue?” “Hata sijui kwakweli, hata mimi sielewagi ni kwanini ila nilikuwa namsikia mama na Ashura wakiongea kuwa haipaswi kabisa wewe kuujua ukweli” “Sawa, ila saivi nimeshajua. Naomba ndugu zako wasijue kama nilikuja na nimekufanya uone na kuongea” “Hawa si ndugu zangu kwakweli, ni wachawi. Kumbe mdogo wangu Ana ni mchawi sana, hata sikujua kama nitapona. Sijui wewe ni mganga?” “Hapana ila nimewasikia wakikuongelea roho ikaniuma sana, ndio nikaamua nikusaidie. Ila usiseme kama ni mimi nimekusaidia” “Sawa sisemi, ila wewe utakuja lini kuhamia hapa nyumbani?” “Nitakuja tu hata usijali!” “Niambie ni lini bhana, mimi nitaondoka humu nyumbani hadi urudi” “Hata usiondoke, wakukute hapa hapa na kwa hakika hawatakufanya chochote halafu wakirudi jifanye haujapona uweze kuwasikiliza maongezi yao yote kwanza. Hata usiwe na mashaka nitakusaidia, ila usimwambie yeyote kama nimekuja hapa. Kwaheri, mimi naondoka hadi wakati mwingine nitarudi rasmi” Salome aliondoka, ila Sara alijiangalia mara mbili mbili na kwenda chumbani kujiangalia kwenye kioo ila bado hakuamini kama amepona kabisa na anaona na kuongea. Akachukua simu yake na kumpigia Ommy kuwa aje nyumbani kwao, kwakweli Ommy alifurahi sana na kumuahidi kufika muda sio mrefu. Basi Salome nae alitoka getini na kumuangalia Yule mlinzi kisha akamwambia, “Wewe si upendi umbea eeh halafu umbea ufanyagi, tafadhali iwe ni siri yako kama nilifika hapa siku ya leo” Salome akaondoka zake huku mlinzi akimshangaa na kujiuliza, “Huyu dogo aliambiwa na marehemu Moza nini kuwa mimi sipendi umbea mmmh!” Alimshangaa sana na kumuangalia hadi alipoishia kuondoka. Muda kidogo Ommy alifika na kugonga geti kisha kuingia ndani, na alipoingia tu akamuita sara ambaye alitoka sebleni, “Eeeh Sara unaongea?” “Ndio naongea” Ommy akamkumbatia sara, pale kisha akakaa nae, “Eeeh niambie ni dawa za Yule babu eeh!” Sara akatamani kumueleza yaliyojiri ila akahofu kwamba Salome alimwambia kuwa asiseme, “Mbona kama unasitasita hivi?” “Natamani kukueleza yaliyotokea ila nashindwa sababu nimeambiwa nisiseme” “Aaah jamani Sara umenza kunificha tena mpenzi!” “Hapana sikuficha, ila kiukweli Yule babu amenisaidia sana. Ndio kafanya nipone kwakweli” Ommy alifurahi sana na kumkumbatia tena Sara, kisha wakaenda pamoja jikoni na kupika chakula na kula, chakula kilikuwa kingi tu kwahiyo walikula na kubakisha kisha Sara akafunika kile chakula jikoni kwao. Kwakweli walikuwa na furaha sana, tena siku hiyo Ommy alishinda nae sana Sara hapo nyumbani kwao, hadi alivyoona jioni jioni akaaga na kuondoka zake. Kwahiyo sara akabaki mwenyewe ndani, tena alienda kukaa pale pale sebleni, muda kidogo mama yake pamoja na Ana walikuwa wamerudi na walikaa pale pale sebleni wakizungumza kwani Sara alikuwa kama mtu aliyelala, “Leo shuleni mwanangu imekuwaje maana sijaelewa eti” “Mama nadhani kuna walimu pale wachawi pia” “Kwanini?” Nilitaka kwenda ofisini ila nikajibanza na kusikia mazungumzo yao, eti Yule mwalimu niliyemuangusha jana chooni leo kaja kazini” “Kheee kaja kazini wakati ulisema hata kuinuka hatoweza?” “Ndio ilitakiwa iwe hivyo mama, sasa nikamkuta Yule mwalimu akiwasimulia wenzie. Kuwa jana shule nzima ilikuwa kimya nay eye ameanguka choono mara gafla akatokea binti mmoja ambaye hamjui na hajawahi kumuona, eti binti Yule alimuinua na kumpaka dawa halafu akamwambia amepona. Eti Yule binti akaondoka na kumuacha Yule mwalimu akienda nyumbani kwake” “Jamani mbona hiyo habari ya ajabu sana, au kuna waganga pale shuleni kwenu?” “Mama, kwa uchawi wangu hakuna mganga anaeuweza hata nashangaa imekuwaje. Ndio wamenibamba pale nasikiliza umbea ndio wamenipa adhabu ya kukaa ofisini mpaka wewe ulipokuja kunichukua. Kwakweli wale walimu wamenikera sana ila sijawafanya chochote sababu nilikuwa na mawazo” “Ila mwanangu inabidi tujue huyo mwalimu kwanini imekuwa hivyo. Na huyo binti aliyemtokea ni nani” “Mama hata usijali, nitahakikisha najua kila kitu na kama ni mganga huyo mtu nitamkomesha” “Yani nimeshangaa sana mwanangu jinsi ulivyo hatari saivi eti vinatokea vitu vya kuzuia mambo yako. Nimeshangaa sana” “Mama tulia, nitafanya kitu utaona tu” Akainuka na kwenda ndani, kisha Rose akamuangalia Sara aliyeonekana amelala pale kwenye kochi halafu akainuka na kwenda chumbani. Sara alikuwa akiwasanifu tu maana alisikia kila kitu walichokuwa wakiongea. Walipoenda chumbani, nae akainuka sasa na kwenda chumbani kwake. Ila muda kidogo akakumbuka kile chakula ambacho alikifunika jikoni, basi akataka kwenda kukitoa ili wasielewe kama alipika siku hiyo, alipofika jikoni kile chakula hakukikuta ila aliona sahani nyeupe kabisa kanakwamba kuna mtu amekula, “Inamaana muda huu huu Ana au mama ametoka kula au ni nini? Hivi wanaweza kula chakula bila kuuliza nani kapika?” Akajiuliza na kuondoka kule jikoni kisha akarudi chumbani kwake, ila ilikuwa ngumu sana kwake kuelewa kuwa kile chakula kimeliwa na nani maana hakutegemea kutokukikuta ukizingatia mama yake pamoja na Ana walishaenda chumbani. Alikaa chumbani kwake akitafakari tu ila aliweza kuhisi sasa kuwa nyumba yao ni zaidi ya anavyoifikiria yeye. Salome akiwa amefika nyumbani kwao, akamkuta mama yake yupo ndani, kisha Salome alipoingia tu akamuanza na maswali, “Unajua sehemu niliyokuaga naenda asubuhi, nimeenda na kurudi. Ila sasa niambie ukweli wewe ulikuwa wapi?” “Nilienda kwa baba” Neema akashtuka na kujikuta akimuuliza tena, “Unasemaje Salome?” “Nilienda kwa baba” “Unaoajua?” “Napajua ndio, si mamdogo Ashura alinielekeza!” “Wewe mtoto wewe usiniletee makubwa mimi” “Makubwa yapi mama? Yani baba kafurahi sana kuniona na alitaka nikae pale moja kwa moja nikamwambia bado sijamuaga mama” “Nitolee balaa lako hilo Salome” “Sio balaa mama, yani baba kwa furaha aliyokuwa nayo kanipa hadi pesa za matumizi” “Pesa za matumizi? Ziko wapi?” Salome akatoa pesa ambazo zilikuwa ni elfu kumi kumi, akampa mama yake. Kwakweli Neema aliishiwa nguvu kabisa kuona zile hela akataka aanze kuzihesabu, “Hata usijisumbue kuhesabu, kaniambia ziko milioni tatu” “Milioni tatu? Yani Patrick akupe wewe milioni tatu! Wakati huo mke wake alikuwa wapi?” “Mkewe alikuwepo na mbona kasapoti tu, tena alitaka niongezewe ila baba akasema hizo za kuanzia” “Mmh Salome wewe unanishangaza” “Mama hata usishangae ila nieleze ukweli kwanini ulinificha kuhusu baba yangu?” “Aaah unajua mwanangu, aaah yani hata sijui nianzie wapi. Achana na hizo habari bhana” Salome akachukua zile hela kwa mama yake, “Sasa mbona umechukua tena wakati ulinikabidhi mwanangu!” “Mpaka uniambie ukweli, mimi ni binti mkubwa sasa. Nataka kujua ukweli wa kwanini ulikuwa unanificha kuhusu baba yangu” “Basi naomba nikuelezee kwa kifupi, si utanipa hizo hela eeh!” “Mi nitakupa ila niambie ukweli” “Ni hivi, Patrick amewahi kuwa mume wangu, tena ni mume wa ndoa kabisa. Nilifunga nae ndoa ya kanisani huko kijijini kwao. Ila niliishi nae muda mrefu sana bila ya kupata mtoto, yani mimi na Patrick tulioana mapema sana. Kipindi hicho nilikuwa na miaka kumi na sita halafu yeye alikuwa na miaka ishirini. Baada ya kuishi muda mrefu bila kuzaa takribani miaka kumi ilipita ndipo tulipohamia mjini na kuendelea tena na maisha ila sikuwahi kupata mimba hata ya kusingiziwa hata mwenyewe nilikuwa nashangaa maana sikuwahi kutoa mimba maishani mwangu. Miaka ilienda tu sibebi mimba wala mdudu wa mimba, basi mjini hapa biashara za Patrick zikaanza kutanuka akawa na mali nyingi na biashara kubwa kubwa ila kilichokosesha furaha ndoa yetu ni mtoto tu. Siku moja mume wangu alizna kufanya biashara na mwanamama aitwaye Rose, Yule Rose alikuwa Rose kweli kipindi hicho alikuwa mzuri haswaaa sio kama siku hizi hata mimi mwenyewe nikawa na mashaka ya kuibiwa penzi langu na rose ingawa alikuwa ni mkubwa sana tu kwangu. Ila naye alikuwa mfanyabiashara, gafla nikaja kusikia Patrick kuna mjengo amejenga huko anaishi na Rose kumbe mimi ananiaga kuwa anasafiri halafu anaenda kuishi na Rose, kuna kipindi alipotea kama miaka mitatu kumbe ndio yupo huko anaishi na Rose. Akarudi na kuishi na mimi kama wiki kumbe ananitafutia sababu ya kunifukuza. Siku hiyo Patrick alikuja na kuniambia wazi kuwa amechoka kuishi na mwanamke asiyezaa, miaka inaenda lakini mwanamke sizai na akaniambia ameamua kuwa na huyo Rose mwenye watoto tayari kwani anaamini huyo atamzalia ukizingatia tayari ameshazaa watoto watatu, nilisononeka sana. Patrick akanifukuza pale nyumbani kama mbwa kisha ile nyumba nasikia alipangisha. Nilianza maisha ya kutangatanga na badae nikajigundua kuwa nina ujauzito, nilijua ile mimba ni ya Patrick nikawa nataka niende kumwambia ila siku hiyo nilikutana na Rose akaniambia nikithubutu kusema basi ataninyonga na kukinyongelea mbali kitoto changu. Ila bado nilijipa matumaini kuwa Patrick akigundua atafurahi, nilihangaika na ile mimba, nakumbuka nilienda kujifungulia kijijini kwa kina Patrick, na mtoto nilimuita Maria Patrick. Jina Maria ni jina ambalo mwanangu ulipewa na bibi yako yani mama mzazi wa Patrick nami nililifurahia sana. Yule mama alinipenda na ndio akaanza kumsumbua Patrick kuwa anirudie mimi na tulee mtoto wetu lakini mambo yakawa si mambo tena, siku hiyo isiyo na jina walikuja vijana na kuvamia pale nyumbani kwa mama Patrick na ndani tulikuwa tunaishi mimi, na mtoto mdogo ambaye ni wewe pamoja na mama yake Patrick. Wale vijana walimchinja mama Patrick mbele ya macho yangu, kwa hakika siwezi kusahau kamwe na nikaambiwa niondoke tena nisionekane kabisa hapo kijijini kwani nitachinjwa na mwanangu kama walivyofanya kwa huyo mama. Walinitishia na niliogopa sana, ingawa ulikuwa ni usiku nikatoka na kukimbia kwa bahati nilikuta watu njiani wakisubiri gari lao nikawaomba lifti na kuja nao mjini. Niliteseka sana na wewe mwanangu yani sikuwa na raha ya maisha kabisa, sikutaka tena kurudi kwa Patrick wala ndugu zake kwani nilihofia yasije yakawapata kama kilichompata mama Patrick. Nilikaa kama miaka mitatu au mine mjini nikitangatanga, ndio kwa bahati nikampata Ashura aliyejitambulisha kama mdogo wangu na toka siku hiyo nikaanza kuishi na Ashura tena ni yeye aliyenishauri nikubadilishe jina ili tusifatiliwe tena. Badala ya Maria tukuite Salome tena akaniambia kuwa Rose amezaa na Patrick mtoto anaitwa Ana basi nikajua furaha ya Patrick imetimia sasa maana kama mtoto ameshapata, basi ndio imekuwa hivyo hadi leo. Naomba nisiendelee sana mwanangu, mengine utayajua taratibu tu. Basi nipe hizo hela” Salome alichukua zile hela na kumkabidhi mama yake, kisha akainuka na kwenda chumbani ambako alikuwa akipanga mipango mipya sababu ameshajua yote aliyotaka kuyajua. “Sasa nimeelewa kwanini Ashura alitumwa, lakini lazima kuna kitu kilikuwa kizuizi cha kuwachinja wahusika na kuishia kumchinja mamake Patrick. Hivi Patrick anajua kweli kama Yule mwanamke ndiye alimuulia mama yake? Najua hajui ila atajua tu” Ila kumbe alikuwa anawaza kwa sauti halafu Neema nae alikuwa amekuja chumbani kwa Salome na kujikuta akimuuliza, “Kujua nini?” “Hamna mama kuna kitu nafikiria tu, ila mama na wewe jiwekee utaratibu basi wa kugonga mlango kabla ya kuingia ninapolala” “Hivi wewe Salome utanificha nini mimi, maana mimi ni mwanamke na wewe ni mwanamke. Hakuna cha kufichana” “Hatakama mama ila ni vizuri kuwe na utaratibu huo” “Basi nitakuwa najitahidi, ila hizi pesa zimenichanganya yani hadi najiona kama namiliki dunia vile” “Yani mama milioni tatu tu ndio inakuchanganya hivyo!” “Kwa mimi ni kubwa sana, ten asana yani hapa hadi sina maneno. Ngoja kesho nikafungue akaunti benki” Salome akacheka tu jinsi mama yake alivyopagawa na zile hela ila ukweli wa hela zile angeujua sijui angefanyeje. Mapacha wa Rose walirudi na moja kwa moja wakaenda kumsalimia dada yao chumbani, “Sara tumekuja kukujulia hali. Najua unatusikia tu ila kuongea na sisi huwezi ila tunakupenda dada yetu. Bado tunazunguka sehemu mbalimbali tukiulizia tiba ya tatizo lako.” Sara akainua kichwa na kuwatazama, kisha akawaambia, “Asanteni kwa upendo wenu” “Khee Sara unaongea!” “Ndio naongea” Kwakweli walifurahi sana na kumkumbatia dada yao, yani ile furaha yao hata ikawashtua Rose na Ana. Walishtuka na kujikuta kwa pamoja wakienda chumbani kwa Sara, kwakweli nao walishangaa sana kumuona Sara anaona na kuzungumza. Naye Sara aliwauliza, “Sasa mnashangaa nini jamani? Hamjapenda nilivyopona!” Ana alisonya yani sonyo ambalo hata kaka zake walishtuka ila hakuna aliyemkaripia, basi Sara akaongea tena, “Hata ukinisonya ni kazi bure tu, nimeshapona yani nimepona kabisa na huniwezi tena” “Unasemaje wewe Sara?” “Huniwezi tena” Ana akataka kufanya jambo pale ila mama yake akamzuia kuwa asifanye kisha akatoka nae na kumuacha Sara na kaka zake. Mmoja akamwambia, “Dada unajiamini sana eeh! Yule mtoto kawa noma” “Kuna noma zaidi yake, aliniweza mwanzo ila kwasasa haniwezi tena” Sara aliongea kwa kujiamini, hadi kaka zake wakataka sara awatajie huyo aliyemfanyia dawa akapona na huyo noma wa Ana. “Nyie subirini tu, akija nitawaambia kwamba huyu ndio kiboko ya Ana. Anajifanya mjanja sana kumbe kuna wajanja zaidi yake, najua hata akinifanyia kitu atakuja Yule na kunisaidia. Kma ameweza kumsaidia mwalimu asiyemfahamu sembuse mimi” Mara Ana akaingia tena chumbani kwa Sara na kusema, “Nimekusikia yote, subiri nikuonyeshe” Kabla hajaanza kufanya chochote chumba cha Sara kikaanza kutikisika. Itaendelea Jumatatu usiku……!!!!! Jumapili nakuwa nimebanwa

at 12:28 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top