KURUDI KWA MOZA: 12 Kisha Ashura akaenda kuwaita wadogo zake Salome, ila kwa muda huo huo Salome aliweza kubadilisha zile sahani za chakula. Ashura aliporudi akaenda kuwapakulia chakula chao watoto, kisha kwa pamoja wakaanza kula mara gafla Ashura akadondoka huku akitapatapa na povu likimtoka mdomoni. Hapo ndio hofu iliwashika hata wadogo zake Salome waliogopa sana na kumuuliza dada yao, “Kwani imekuwaje dada?” “Min a mamdogo Ashura tunacheza mchezo kwahiyo hata msiwe na mashaka” Ila Salome alikuwa jasiri sana kwa wakati huo kwani alimchukua mamake mdogo huyo na kumburuza hadi chumbani kisha akamfunika na kitenge halafu akachukua simu ya Ashura na kuifungua halafu akaangalia namba aliyoipiga mwishoni akaona ni namba ambayo haijaandikwa jina ila akahisi ndio hiyo hiyo namba ya Rose, akaamua amtumie ujumbe mfupi, “Dada, mbona hii dawa nimempa huyu Salome ameanguka na povu linamtoka mdomoni?” Baada ya muda ujumbe ule ukajibiwa, “Hahaha, tayari huyo yani hapo kazi umamiliza mdogo wangu. Unaweza ukaondoka sasa” Naye Salome akaandika ujumbe mwingine, “Jamani dada tayari nini tena?” “Kwani huji? Ameshakufa huyo” “Kheee kumbe dawa ilikuwa ya kummaliza kabisa! Mbona mwanzo hukuniambia?” “Hivi wewe Ashura unasahau sahau nini, nilishakwambia toka mwanzo kuwa huyo mtoto nataka nimmalize. Tena toka siku ya kwanza nilikwambia hiyo dawa ni ya kummaliza kabisa, wewe cha kufanya saivi ni kuondoka hapo upesi iwezekanavyo maana kazi tushamaliza. Si nilishakwambia na nguo zako upange kabisa, nakutumia na hela muda sio mrefu ili uondoke” Na kweli baada ya muda mfupi ikaingia meseji kwenye simu kuwa amepokea milioni mbili na elfu kumi na tano. Kisha ikafatia meseji ya kawaida, “Toa hiyo milioni mbili itakusaidia kwenye safari yako, ukishafika nishtue nikutumie hela nyingine” “Hivi dada hawatanikamata kweli?” “Akukamate nani bhana, kuna mtu anapajua kwenu hapo? Hakuna anayepajua kwenu, hawakukamati wala nini. Kwanza Ashura sio jina lako, kwahiyo watakutafuta hadi wachanganyikiwe” “Ila hawa wadogo wameona kama dada yao ameanguka” “Achana nao hao, waondoe hapo nyumbani. Wape hata hela ya biskuti ili wakatembee. Mimi hao nao nitawatokomeza ingawa sijui kuhusu ukweli wao, ila usipoteze muda saivi. Ondoka upesi” “Sawa dada, ngoja niondoke” Salome akamtazama Ashura waliyeishi nae kwa kipindi kirefu sana ila kumbe kuna kazi alitumwa aifanye hapo, kisha akatoka nje na kuwapa wadogo zake hela ya biskuti kama ambavyo Rose alikuwa amemshauri Ashura kwani wale watoto walipenda sana michezo na kwa vyovyote vile wamepewa na hela ndio kabisa. Hiyo hela aliipata kwa mama yake ambayo aliiacha kwaajili ya mboga ya jioni. Kisha Salome akarudi tena chumbani kwa Ashura na kuanza kupekua begi lake, ila alikuta nguo zote za Ashura zimepangwa vizuri sana na vitambulisho vya Ashura alivikuta, na kushangaa sana. “Hadi vitambulisho vimeandikwa Ashura kumbe sio jina lake mmmh!” Wakati anapekua zaidi, alikutana na pochi yenye hela, alipozihesabu zile hela ilikuwa ni milioni tatu na laki saba, “Mmh na mbona kila siku anasemaga hana hela jamani!!” Alipopekua vizuri aliona kijitabu kimeandikwa andikwa namba za simu, halafu kiliandikwa na namba za siri za kutolea hela kwenye simu, halafu kilikuwa na namba zenye maelezo “Hawa ni watu nitakaowatumia kupoteza ushahidi” Kidogo Salome alishtuka ila swala la kukuta namba za siri kwenye kile kitabu zilimfurahisha kwani aliona kila kitu kimetimia sasa, akitoa na zile hela atakuwa na hela za kutosha, alipojaribisha ile namba kwenye simu ili aangalie tu salio lililopo kwenye simu kakuta kuna 10,050,000/= kwakweli Salome alishangaa sana, “Kheee milioni kumi kwenye simu! Kumbewalikuwa wanaishi na pedeshee humu ndani” Akaona ni vyema hiyo hela kabla ya kuitoa aifanyie maarifa ya kuihamisha kwenye simu nyingine halafu ndio aitoe ila kwa wakati huo akafanya namna ya kuweza kuzima lile swala la Ashura. Hivyo akatoka na kwenda kununua viroba vikubwa vya kuweza kumtumbukiza mtu, na aliifanya kazi ile mwenyewe alimtumbukiza Ashura kwenye vile viroba halafu akavifunga kwa juu halafu akamviringisha shuka na kumtumbukiza kwenye kiroba kingine. Halafu zile namba za wale watu alizozikuta kwenye kile kitabu cha Ashura ambao alikuwa ameandika historia zao, akawasiliana nao kwa njia ya ujumbe kwa kutumia simu ya Ashura kisha akawaelekeza pale kwao na mahali alipoweka huo mzigo wa mtu kwani alikuwa ameuburuza hadi sebleni. Halafu yeye akatoka kwenda kutafuta simu nyingine na laini ya kutumia yeye kwa kutumia zile hela alizozikuta kwenye begi la Ashura, hakuwa na wasiwasi na wadogo zake kwani wale huwa wanarudi nyumbani mpaka watafutwe na kuitwa. Ila alitumia ujanja wa kujificha sehemu hadi wale vijana walipofika na kutoka na ule mwili na kuupakia kwenye gari na kutokomea zao. Hapo alirudi tena pale kwao na kufunga milango halafu akatoka. Rose alikuwa ni mtu mwenye furaha sana kwa wakati huo hata akasahau kila kilichomtokea kwani mambo yote yalikuwa yamefutwa na kifo cha mtu mmoja tu, kifo cha Salome. Kwakweli furaha yake ilikuwa maradufu, akaenda kwa mumewe na kumwambia, “Leo, nataka nipike mwenyewe. Sema nikupikie chakula gani?” “Mmmh leo umefurahi na nini mke wangu jamani?” “Wewe sema tu ni chakula gani unataka” “Nipikie chochote tu” Akaenda jikoni na kumuita Ana, kisha akamwambia “Mwanangu, dadako si umuachie mdomo tu” “Hapana mama, hawezi huyu ataropoka tu” “Ameshajifunza mwanangu, halafu leo nina furaha sana muachie bhana” “Furaha ya nini mama?” “Yule mtoto aliyekuwa ananisumbua kichwa siku zote, kila nilipojaribu kummaliza nilishindwa hadi kuamua kumtafuta mtu wa kunisaidia. Ila leo naongea habari nyingine kabisa tena kwa furaha, Yule mtoto amekufa” “Kheee mama, kweli hiyo ni habari njema tena njema haswaaa” “Sasa sikia mwanangu, chukua simu yangu ile na utoe hela benki halafu utume kwenye namba ya Ashura. Mtumie milioni tano, nataka atulie kabisa huko alipoenda” “Sawa mama” Ilionyesha hii habari pia Ana ilimfurahisha sana, kwahiyo akaenda kuchukua simu ya mama yake na kufanya hivyo. Ana alikuwa ndio mtoto pekee aliyejua siri za mama yake, hata namba zake za siri zote alimwambia mwanae huyo. Alipomaliza alimfata tena mama yake na kumwambia, “Tayari mama nimemtumia” “Sawa, mtumie na meseji kuwa nimemtumia hela nyingine maana najua kuongea kwa sauti hawezi sababu ya hili tukio” “Sawa mama” Ana alituma ujumbe kwenye namba ya Ashura, na baada ya muda tu ujumbe huo ukajibiwa, “Nimeipata asante dada, saivi ndio niko njiani naelekea kule kijijini. Nishafuta hadi ushahidi, yani hawawezi kujua Salome ametokomea wapi au amefia wapi maana nimewaagiza vijana wautokomeze mwili wake kabisa kwahiyo hakuna ushahidi, na mimi nimeondoka kabisa” Ana alimsomea mama yake ambaye kwa hakika alikuwa na furaha zaidi, kisha akachukua simu ile kwa Ana na kuwapigia vijana ambao yeye alikuwa anawafahamu, “Vipi mmeshafanya kazi ya Ashura?” “Tushamaliza bi.mkubwa si unajua sisi hatucheleweshagi” “Sasa mmemtupia wapi?” “Kwenye mapango huko, hawezi kuonekana kamwe. Yani kama watu wataenda miaka ijayo hiyo basi watakuta mifupa. Ila Ashura ni jasiri sana kwani tumekuta amemfunga vizuri kabisa.” “Sawa, sasa amewalipa?” “Bado, amesema kuwa yupo safarini” “Basi msimdai yeye hela, nawatumia sasa hivi” Kisha Rose akakata ile simu huku akiwa na furaha zaidi halafu akawatumia hela wale vijana, kwakweli leo ilikuwa ni siku ya furaha kabisa kwake. Salome aliamua kufanya jambo moja la akili sana, alitafuta dalali siku hiyo hiyo na kuulizia kuhusu nyumba, kwakweli ilipatikana yani maisha ukiwa na hela mkononi mambo mengi yanawezekana ila kama huna hela kila kitu kinakushinda. Salome alilipia ile nyumba waliyoipata kisha akatafuta vijana na usafiri wa kuanza kusafirisha vitu kwenye nyumba mpya, kisha akawaita wadogo zake na kwenda nao huko kupya. Walipofika walikuwa wakishangaa shangaa tu, “Dada, tumehamia kwingine! Mamdogo na mama wako wapi?” “Mama atakuja, ila mamdogo kagoma kuja huku” “Jamani dada, mwambie mamdogo aje” Mwingine akasema, “Ila bora agome, Yule mamdogo simpendagi” “John, usiwe hivyo bhana. Mama ametufundisha upendo” “Hatakama tumefundishwa upendo na mama, ila si kagoma mwenyewe. Akiendelea kugoma dada Salome achana nae. Aje mama tu” “Sawa sawa mdogo wangu John, wewe ndio kidume. Achana na Jose huyu anajifanya mlokole” Basi Salome aliwaacha pale wadogo zake na kwenda kumalizia vitu kwenye nyumba yao, halafu alitafuta watu wa kuwapangia vitu vyao ndani. Yote hayo yaliwezekana kwa nguvu ya pesa tu. Walipomaliza kupanga, alirudi pale kwenye nyumba yao ya zamani na kuwaacha wadogo zake kwenye nyumba mpya, alienda kwa lengo la kumsubiri mama yake kwani usiku tayari ulishaingia. Kwenye mida ya saa mbili hivi, Neema alirudi na kuingia ndani. Alikuta nyumba yote nyeupe hakuna hata kitu ndani. Alipatwa na mashaka na kuhisi kuwa wameibiwa, wakati anataka kutoka ili aulize kwa majirani ndipo akakutana na Salome, “Imekuwaje mwanangu mbona sielewi!” “Tumehama mama” “Tumehama, kivipi sikuelewi” “Yani elewa tu kuwa tumehama mama, hapa nimekuja tu kukufata ili twende kwenye nyumba mpya” “Tutahamaje wakati hapa kodi haijaisha?” “Mama, mbona unakuwa mbishi hivyo! Nenda tu kazungumze na mwenye nyumba mkabidhi funguo atafute mpangaji mwingine, sisi tumehama” “Wengine wote wako wapi?” “Wapo huko kwenye nyumba mpya” Kwakweli Neema alishindwa kuelewa kabisa kile kitendo cha kuhama kwa gafla vile halafu Salome anamwambia akakabidhi funguo. “Hapana siwezi kukabidhi funguo wakati sijui tulipohamia” “Inamaana mama huniamini mimi?” “Nakuamini vizuri mwanangu ila kwa hili unanichanganya” “Mama, tulikohamia ni mbali. Funguo twende tu ukakabidhi leoleo” Kwavile Neema alimuamini sana binti yake, ikabidi aongozane nae mpaka kwa mwenye nyumba na kumkabidhi funguo, “Mbona hamkusema jamani kama mnahama? Halafu mbona ni haraka haraka?” “Nisameheni mimi ila haya ni mambo ya Salome na mdogo wangu Ashura hata sijui wamefikiria nini ila ndio hivyo tumehama” Neema aliwaaga pale kisha akaondoka na mwanae kuelekea huko kupya walikohamia. Walifika kwenye mida ya saa nne usiku hata wakawakuta wale wadogo zake Salome wamelala kwenye viti, “Mmh jamani mmewachosha watoto na kuhamahama kwenu, hivi wamekula kweli hawa? Ashura, Ashura” Neema alijikuta akimuita Ashura kwani alitaka ndiye amjibu kwani yeye ni mtu mzima na atakuwa anjua mambo mengi sana, Salome alimuangalia mama yake na kumwambia, “Ashura hayupo” “Wewe si nishakukataza, ni mamako mdogo Yule. Haya hayupo yuko wapi?” “Kuna mahali ameenda, alisema atarudi kesho” “Sasa na kuhamia hapa nani ametoa wazo hilo?” “Ni yeye tena tumesaidiana nae hadi kuja hapa ila baada ya kupanga kila kitu akaniaga na kuondoka. Wakati huo mimi nilikuja kukufata wewe, halafu yeye alikuwa ameondoka” “Sasa watoto wamekula hawa?” “Ndio, walinunuliwa chips wamekula, hata wewe za kwako zipo” Akaenda kumletea mama yake, ambaye alikula bila kuhoji zaidi kwani njaa ilikuwa inamuuma, kisha akaenda kumuonyesha chumba cha kulala yeye. Sababu alikuwa amechoka sana akasema ile nyumba ataiangalia vizuri kesho yake, Salome akawachukua na wadogo zake na kuwapeleka chumbani kulala. Kisha yeye alienda chumbani kwake. Hiyo nyumba ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala kama ile waliyokuwa wanakaa mwanzo ila ilikuwa ni nzuri zaidi ya ile ya mwanzo. Neema alilala fofofo kutokana na uchovu alionao wa siku hiyo kitu kilichomfanya ashindwe hata kuhoji vizuri kuhusu ile nyumba na wazo la kuhama. Ila kulipokucha alichukua simu yake, na akashtushwa na ujumbe kutoka kwa Ashura, “Dada samahani najua utakuwa umefadhaika sana kwa kutokunikuta ila mimi lengo langu ilikuwa ni kuona dada yangu unaishi kwenye mazingira safi na mazuri. Hiyo nyumba nimelipa kodi ya mwaka mzima kwahiyo usihangaike kabisa dada yangu. Mimi nimeamua kurudi kijijini kwetu kwa ndugu zangu nimewakumbuka sana, na huko mjini sitarudi tena. Wala usihangaike kunitafuta dada yangu. Halafu huku mtandao unasumbuaga sana kwahiyo mara nyingi nitakuwa sipatikani kwenye simu. Usihangaike kumuuliza Salome, hajui chochote kuhusu kuondoka kwangu kwani ningemwambia ukweli kama naondoka angelia ndiomana nimeondoka kimya kimya. Nawapenda sana ten asana, hata msiwe na wasiwasi na mimi nipo salama kabisa” Neema alisoma ule ujumbe mara mbili mbili ila alishindwa hata aanzie wapi kuhoji na ukizingatia kashaambiwa hata Salome asimuulize. Kwakweli alibaki kimya tu akitazama ile nyumba kisha akatoka na kwenda kuitazama vizuri zaidi. Wakati anaenda kwenye kila chumba kukagua aliingia na kwenye chumba walicholala watoto wake mapacha na kuwaona bado wamelala, kwakweli aliuthaminisha uzuri wa ile nyumba. Kisha akaingia chumba anacholala Salome tena aliingia bila hodi, ila alimuona Salome amesimama akiwa amempa mgongo hivi ila Neema alishtuka sana na kujikuta akisema kwa mshtuko, “Aaah Moza!!” Salome aligeuka sasa na kumuangalia vizuri Neema, lakini Neema alijikuta anaanguka chini. Itaendelea kesho usiku kama kawaida…..!!!!!! By, Atuganile Mwakalile. Mapenzi na Maisha iko kwenye Facebook. Ili kuunganisha kwa Mapenzi na Maisha, jiunge kwenye Facebook leo. Jiunge au Ingia Mapenzi na Maisha KURUDI KWA MOZA: 12 Kisha Ashura akaenda kuwaita wadogo zake Salome, ila kwa muda huo huo Salome aliweza kubadilisha zile sahani za chakula. Ashura aliporudi akaenda kuwapakulia chakula chao watoto, kisha kwa pamoja wakaanza kula mara gafla Ashura akadondoka huku akitapatapa na povu likimtoka mdomoni. Hapo ndio hofu iliwashika hata wadogo zake Salome waliogopa sana na kumuuliza dada yao, “Kwani imekuwaje dada?” “Min a mamdogo Ashura tunacheza mchezo kwahiyo hata msiwe na mashaka” Ila Salome alikuwa jasiri sana kwa wakati huo kwani alimchukua mamake mdogo huyo na kumburuza hadi chumbani kisha akamfunika na kitenge halafu akachukua simu ya Ashura na kuifungua halafu akaangalia namba aliyoipiga mwishoni akaona ni namba ambayo haijaandikwa jina ila akahisi ndio hiyo hiyo namba ya Rose, akaamua amtumie ujumbe mfupi, “Dada, mbona hii dawa nimempa huyu Salome ameanguka na povu linamtoka mdomoni?” Baada ya muda ujumbe ule ukajibiwa, “Hahaha, tayari huyo yani hapo kazi umamiliza mdogo wangu. Unaweza ukaondoka sasa” Naye Salome akaandika ujumbe mwingine, “Jamani dada tayari nini tena?” “Kwani huji? Ameshakufa huyo” “Kheee kumbe dawa ilikuwa ya kummaliza kabisa! Mbona mwanzo hukuniambia?” “Hivi wewe Ashura unasahau sahau nini, nilishakwambia toka mwanzo kuwa huyo mtoto nataka nimmalize. Tena toka siku ya kwanza nilikwambia hiyo dawa ni ya kummaliza kabisa, wewe cha kufanya saivi ni kuondoka hapo upesi iwezekanavyo maana kazi tushamaliza. Si nilishakwambia na nguo zako upange kabisa, nakutumia na hela muda sio mrefu ili uondoke” Na kweli baada ya muda mfupi ikaingia meseji kwenye simu kuwa amepokea milioni mbili na elfu kumi na tano. Kisha ikafatia meseji ya kawaida, “Toa hiyo milioni mbili itakusaidia kwenye safari yako, ukishafika nishtue nikutumie hela nyingine” “Hivi dada hawatanikamata kweli?” “Akukamate nani bhana, kuna mtu anapajua kwenu hapo? Hakuna anayepajua kwenu, hawakukamati wala nini. Kwanza Ashura sio jina lako, kwahiyo watakutafuta hadi wachanganyikiwe” “Ila hawa wadogo wameona kama dada yao ameanguka” “Achana nao hao, waondoe hapo nyumbani. Wape hata hela ya biskuti ili wakatembee. Mimi hao nao nitawatokomeza ingawa sijui kuhusu ukweli wao, ila usipoteze muda saivi. Ondoka upesi” “Sawa dada, ngoja niondoke” Salome akamtazama Ashura waliyeishi nae kwa kipindi kirefu sana ila kumbe kuna kazi alitumwa aifanye hapo, kisha akatoka nje na kuwapa wadogo zake hela ya biskuti kama ambavyo Rose alikuwa amemshauri Ashura kwani wale watoto walipenda sana michezo na kwa vyovyote vile wamepewa na hela ndio kabisa. Hiyo hela aliipata kwa mama yake ambayo aliiacha kwaajili ya mboga ya jioni. Kisha Salome akarudi tena chumbani kwa Ashura na kuanza kupekua begi lake, ila alikuta nguo zote za Ashura zimepangwa vizuri sana na vitambulisho vya Ashura alivikuta, na kushangaa sana. “Hadi vitambulisho vimeandikwa Ashura kumbe sio jina lake mmmh!” Wakati anapekua zaidi, alikutana na pochi yenye hela, alipozihesabu zile hela ilikuwa ni milioni tatu na laki saba, “Mmh na mbona kila siku anasemaga hana hela jamani!!” Alipopekua vizuri aliona kijitabu kimeandikwa andikwa namba za simu, halafu kiliandikwa na namba za siri za kutolea hela kwenye simu, halafu kilikuwa na namba zenye maelezo “Hawa ni watu nitakaowatumia kupoteza ushahidi” Kidogo Salome alishtuka ila swala la kukuta namba za siri kwenye kile kitabu zilimfurahisha kwani aliona kila kitu kimetimia sasa, akitoa na zile hela atakuwa na hela za kutosha, alipojaribisha ile namba kwenye simu ili aangalie tu salio lililopo kwenye simu kakuta kuna 10,050,000/= kwakweli Salome alishangaa sana, “Kheee milioni kumi kwenye simu! Kumbewalikuwa wanaishi na pedeshee humu ndani” Akaona ni vyema hiyo hela kabla ya kuitoa aifanyie maarifa ya kuihamisha kwenye simu nyingine halafu ndio aitoe ila kwa wakati huo akafanya namna ya kuweza kuzima lile swala la Ashura. Hivyo akatoka na kwenda kununua viroba vikubwa vya kuweza kumtumbukiza mtu, na aliifanya kazi ile mwenyewe alimtumbukiza Ashura kwenye vile viroba halafu akavifunga kwa juu halafu akamviringisha shuka na kumtumbukiza kwenye kiroba kingine. Halafu zile namba za wale watu alizozikuta kwenye kile kitabu cha Ashura ambao alikuwa ameandika historia zao, akawasiliana nao kwa njia ya ujumbe kwa kutumia simu ya Ashura kisha akawaelekeza pale kwao na mahali alipoweka huo mzigo wa mtu kwani alikuwa ameuburuza hadi sebleni. Halafu yeye akatoka kwenda kutafuta simu nyingine na laini ya kutumia yeye kwa kutumia zile hela alizozikuta kwenye begi la Ashura, hakuwa na wasiwasi na wadogo zake kwani wale huwa wanarudi nyumbani mpaka watafutwe na kuitwa. Ila alitumia ujanja wa kujificha sehemu hadi wale vijana walipofika na kutoka na ule mwili na kuupakia kwenye gari na kutokomea zao. Hapo alirudi tena pale kwao na kufunga milango halafu akatoka. Rose alikuwa ni mtu mwenye furaha sana kwa wakati huo hata akasahau kila kilichomtokea kwani mambo yote yalikuwa yamefutwa na kifo cha mtu mmoja tu, kifo cha Salome. Kwakweli furaha yake ilikuwa maradufu, akaenda kwa mumewe na kumwambia, “Leo, nataka nipike mwenyewe. Sema nikupikie chakula gani?” “Mmmh leo umefurahi na nini mke wangu jamani?” “Wewe sema tu ni chakula gani unataka” “Nipikie chochote tu” Akaenda jikoni na kumuita Ana, kisha akamwambia “Mwanangu, dadako si umuachie mdomo tu” “Hapana mama, hawezi huyu ataropoka tu” “Ameshajifunza mwanangu, halafu leo nina furaha sana muachie bhana” “Furaha ya nini mama?” “Yule mtoto aliyekuwa ananisumbua kichwa siku zote, kila nilipojaribu kummaliza nilishindwa hadi kuamua kumtafuta mtu wa kunisaidia. Ila leo naongea habari nyingine kabisa tena kwa furaha, Yule mtoto amekufa” “Kheee mama, kweli hiyo ni habari njema tena njema haswaaa” “Sasa sikia mwanangu, chukua simu yangu ile na utoe hela benki halafu utume kwenye namba ya Ashura. Mtumie milioni tano, nataka atulie kabisa huko alipoenda” “Sawa mama” Ilionyesha hii habari pia Ana ilimfurahisha sana, kwahiyo akaenda kuchukua simu ya mama yake na kufanya hivyo. Ana alikuwa ndio mtoto pekee aliyejua siri za mama yake, hata namba zake za siri zote alimwambia mwanae huyo. Alipomaliza alimfata tena mama yake na kumwambia, “Tayari mama nimemtumia” “Sawa, mtumie na meseji kuwa nimemtumia hela nyingine maana najua kuongea kwa sauti hawezi sababu ya hili tukio” “Sawa mama” Ana alituma ujumbe kwenye namba ya Ashura, na baada ya muda tu ujumbe huo ukajibiwa, “Nimeipata asante dada, saivi ndio niko njiani naelekea kule kijijini. Nishafuta hadi ushahidi, yani hawawezi kujua Salome ametokomea wapi au amefia wapi maana nimewaagiza vijana wautokomeze mwili wake kabisa kwahiyo hakuna ushahidi, na mimi nimeondoka kabisa” Ana alimsomea mama yake ambaye kwa hakika alikuwa na furaha zaidi, kisha akachukua simu ile kwa Ana na kuwapigia vijana ambao yeye alikuwa anawafahamu, “Vipi mmeshafanya kazi ya Ashura?” “Tushamaliza bi.mkubwa si unajua sisi hatucheleweshagi” “Sasa mmemtupia wapi?” “Kwenye mapango huko, hawezi kuonekana kamwe. Yani kama watu wataenda miaka ijayo hiyo basi watakuta mifupa. Ila Ashura ni jasiri sana kwani tumekuta amemfunga vizuri kabisa.” “Sawa, sasa amewalipa?” “Bado, amesema kuwa yupo safarini” “Basi msimdai yeye hela, nawatumia sasa hivi” Kisha Rose akakata ile simu huku akiwa na furaha zaidi halafu akawatumia hela wale vijana, kwakweli leo ilikuwa ni siku ya furaha kabisa kwake. Salome aliamua kufanya jambo moja la akili sana, alitafuta dalali siku hiyo hiyo na kuulizia kuhusu nyumba, kwakweli ilipatikana yani maisha ukiwa na hela mkononi mambo mengi yanawezekana ila kama huna hela kila kitu kinakushinda. Salome alilipia ile nyumba waliyoipata kisha akatafuta vijana na usafiri wa kuanza kusafirisha vitu kwenye nyumba mpya, kisha akawaita wadogo zake na kwenda nao huko kupya. Walipofika walikuwa wakishangaa shangaa tu, “Dada, tumehamia kwingine! Mamdogo na mama wako wapi?” “Mama atakuja, ila mamdogo kagoma kuja huku” “Jamani dada, mwambie mamdogo aje” Mwingine akasema, “Ila bora agome, Yule mamdogo simpendagi” “John, usiwe hivyo bhana. Mama ametufundisha upendo” “Hatakama tumefundishwa upendo na mama, ila si kagoma mwenyewe. Akiendelea kugoma dada Salome achana nae. Aje mama tu” “Sawa sawa mdogo wangu John, wewe ndio kidume. Achana na Jose huyu anajifanya mlokole” Basi Salome aliwaacha pale wadogo zake na kwenda kumalizia vitu kwenye nyumba yao, halafu alitafuta watu wa kuwapangia vitu vyao ndani. Yote hayo yaliwezekana kwa nguvu ya pesa tu. Walipomaliza kupanga, alirudi pale kwenye nyumba yao ya zamani na kuwaacha wadogo zake kwenye nyumba mpya, alienda kwa lengo la kumsubiri mama yake kwani usiku tayari ulishaingia. Kwenye mida ya saa mbili hivi, Neema alirudi na kuingia ndani. Alikuta nyumba yote nyeupe hakuna hata kitu ndani. Alipatwa na mashaka na kuhisi kuwa wameibiwa, wakati anataka kutoka ili aulize kwa majirani ndipo akakutana na Salome, “Imekuwaje mwanangu mbona sielewi!” “Tumehama mama” “Tumehama, kivipi sikuelewi” “Yani elewa tu kuwa tumehama mama, hapa nimekuja tu kukufata ili twende kwenye nyumba mpya” “Tutahamaje wakati hapa kodi haijaisha?” “Mama, mbona unakuwa mbishi hivyo! Nenda tu kazungumze na mwenye nyumba mkabidhi funguo atafute mpangaji mwingine, sisi tumehama” “Wengine wote wako wapi?” “Wapo huko kwenye nyumba mpya” Kwakweli Neema alishindwa kuelewa kabisa kile kitendo cha kuhama kwa gafla vile halafu Salome anamwambia akakabidhi funguo. “Hapana siwezi kukabidhi funguo wakati sijui tulipohamia” “Inamaana mama huniamini mimi?” “Nakuamini vizuri mwanangu ila kwa hili unanichanganya” “Mama, tulikohamia ni mbali. Funguo twende tu ukakabidhi leoleo” Kwavile Neema alimuamini sana binti yake, ikabidi aongozane nae mpaka kwa mwenye nyumba na kumkabidhi funguo, “Mbona hamkusema jamani kama mnahama? Halafu mbona ni haraka haraka?” “Nisameheni mimi ila haya ni mambo ya Salome na mdogo wangu Ashura hata sijui wamefikiria nini ila ndio hivyo tumehama” Neema aliwaaga pale kisha akaondoka na mwanae kuelekea huko kupya walikohamia. Walifika kwenye mida ya saa nne usiku hata wakawakuta wale wadogo zake Salome wamelala kwenye viti, “Mmh jamani mmewachosha watoto na kuhamahama kwenu, hivi wamekula kweli hawa? Ashura, Ashura” Neema alijikuta akimuita Ashura kwani alitaka ndiye amjibu kwani yeye ni mtu mzima na atakuwa anjua mambo mengi sana, Salome alimuangalia mama yake na kumwambia, “Ashura hayupo” “Wewe si nishakukataza, ni mamako mdogo Yule. Haya hayupo yuko wapi?” “Kuna mahali ameenda, alisema atarudi kesho” “Sasa na kuhamia hapa nani ametoa wazo hilo?” “Ni yeye tena tumesaidiana nae hadi kuja hapa ila baada ya kupanga kila kitu akaniaga na kuondoka. Wakati huo mimi nilikuja kukufata wewe, halafu yeye alikuwa ameondoka” “Sasa watoto wamekula hawa?” “Ndio, walinunuliwa chips wamekula, hata wewe za kwako zipo” Akaenda kumletea mama yake, ambaye alikula bila kuhoji zaidi kwani njaa ilikuwa inamuuma, kisha akaenda kumuonyesha chumba cha kulala yeye. Sababu alikuwa amechoka sana akasema ile nyumba ataiangalia vizuri kesho yake, Salome akawachukua na wadogo zake na kuwapeleka chumbani kulala. Kisha yeye alienda chumbani kwake. Hiyo nyumba ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala kama ile waliyokuwa wanakaa mwanzo ila ilikuwa ni nzuri zaidi ya ile ya mwanzo. Neema alilala fofofo kutokana na uchovu alionao wa siku hiyo kitu kilichomfanya ashindwe hata kuhoji vizuri kuhusu ile nyumba na wazo la kuhama. Ila kulipokucha alichukua simu yake, na akashtushwa na ujumbe kutoka kwa Ashura, “Dada samahani najua utakuwa umefadhaika sana kwa kutokunikuta ila mimi lengo langu ilikuwa ni kuona dada yangu unaishi kwenye mazingira safi na mazuri. Hiyo nyumba nimelipa kodi ya mwaka mzima kwahiyo usihangaike kabisa dada yangu. Mimi nimeamua kurudi kijijini kwetu kwa ndugu zangu nimewakumbuka sana, na huko mjini sitarudi tena. Wala usihangaike kunitafuta dada yangu. Halafu huku mtandao unasumbuaga sana kwahiyo mara nyingi nitakuwa sipatikani kwenye simu. Usihangaike kumuuliza Salome, hajui chochote kuhusu kuondoka kwangu kwani ningemwambia ukweli kama naondoka angelia ndiomana nimeondoka kimya kimya. Nawapenda sana ten asana, hata msiwe na wasiwasi na mimi nipo salama kabisa” Neema alisoma ule ujumbe mara mbili mbili ila alishindwa hata aanzie wapi kuhoji na ukizingatia kashaambiwa hata Salome asimuulize. Kwakweli alibaki kimya tu akitazama ile nyumba kisha akatoka na kwenda kuitazama vizuri zaidi. Wakati anaenda kwenye kila chumba kukagua aliingia na kwenye chumba walicholala watoto wake mapacha na kuwaona bado wamelala, kwakweli aliuthaminisha uzuri wa ile nyumba. Kisha akaingia chumba anacholala Salome tena aliingia bila hodi, ila alimuona Salome amesimama akiwa amempa mgongo hivi ila Neema alishtuka sana na kujikuta akisema kwa mshtuko, “Aaah Moza!!” Salome aligeuka sasa na kumuangalia vizuri Neema, lakini Neema alijikuta anaanguka chini. Itaendelea kesho usiku kama kawaida…..!!!!!!

at 12:26 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top