KURUDI KWA MOZA :1 Moza alikuwa msichana mrembo ila aliishi maisha ya shida na kumfanya ajaribu kufanya kazi za ndani, na kwa bahati akapata kazi kwenye nyumba ya mama mmoja tajiri, aliyejulikana kwa jina la Rose ila huyu mama mara nyingi alikuwa hadumu na wafanyakazi wa ndani mara nyingi huwa anawafukuza na watu walijua hivyo hakuna aliyejua ukweli kuhusu wafanyakazi wa Rose kwani gafla utakuta wamepotea na ameleta mfanyakazi mpya kwahiyo wengi walihisi huwa anawafukuza. Siku ya kwanza kumleta Moza nyumbani kwake alimpa onyo kabisa, "Mambo ya nyumba hii uyaache kama yalivyo, wewe fanya kazi zako tu basi. Usiingilie mambo yasiyokuhusu" "Sawa mama nimekuelewa, unadhani naweza kuingilia yasiyonihusu? Siwezi kufanya huo ujinga " "Yani usithubutu kuingilia utaishia kubaya" "Mbona unanitishia mama?" "Sikutishii ila nakwambia hali halisi, umbea kwangu sitaki kabisa kama huwezi kazi unaweza umbea useme kabisa uondoke" "Hapana mama simaanishi kuwa naweza umbea, kwanza binafsi umbea siupendi kabisa kwahiyo hata usijali kuhusu mimi" Basi huyu mama alimuonyesha kazi zote za ile nyumba na vyumba vyote vya kusafisha, kwakweli nyumba ilikuwa ni kubwa sana lakini alimuonyesha yote, ila kulikuwa na chumba flani kilikuwa na chumba kwa ndani kile chumba kilikuwa kama choo cha ndani ya chumba na vigumu kujua kama kuna chumba ndani ya chumba, yule mama alimwambia Moza "Hiki chumba ukishasafisha unakifunga halafu funguo unaweza juu ya mlango" "Na hiko choo je nitakuwa nakishafishaje maana naona kufuli au hakisafishwagi?" "Wee binti mbona umeanza kunitisha, umekionaje hiko?" "nilijikuta nimeangalia tu nyuma ya hilo kabati, nisamehe lakini. Kwani hakisafishwi au?" "Hiko kilitengenezwa kwa lengo la kuwa choo ila kishazibwa na hakitumiki, nyuma yake kushabomolewa ila hapa mwanzo mlango ulibakia na kufuli, huwa hapafunguliwi maana hakuna choo wala nini na ukitoka ni nje kabisa ndiomana nimeweka kabati kama kuziba. Na wewe uache kuchunguza chunguza, kazi yako kwenye chumba hiki ni kusafisha tu nikikwambia ili kusiwe na vumbi basi ingawa halali mtu lakini panatakiwa kusafishwa." Wakatoka nje na kumuonyesha sehemu zingine za kusafisha kisha alipomaliza ndipo Moza alianza kazi rasmi kwenye nyumba hiyo.... je umeipenda hii riwaya?? piga kura ya NDIYO na HAPANA Hiki ni pande kidogo cha storii yetu wahimize wale mafans wetu warudi tena kwa page yetu maana mambo yameanza mwandishi ni dada etu ATUGANILE MWAKALILE

at 2:28 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top