JINA: NYOKA WA KUTUMWA SEHEMU YA 10 …………………… ilipoishia …………………….. Walipomaliza maongezi wakaondoka na kumuacha mfalme akitafakari maneno yao huku akipanga na adhabu ambazo watapata pindi ikijulikana wanamsingizia mzee sube. Kuanzia hapo masaa yalienda na hatiamaemda wa kwenda kwenye kazi ukawadia, wale vijana wakajikusanya sehemu moja na kwenda kwenye ile nyumba waliyokuwa wamekaa siku ya kwanza. …………………… Endelea …………………………………………. Baada ya mda kidogo kupita mfalme akawasili sehemu ile na kuwakuta vijana wakiwa wamejianda na kila aina ya dhana kwa ajili ya kupambana na yule nyoka pindi wakifanikiwa kumuona, kijana mmoja ambae ndie alikuwa kama kiongozi wa wale wenzake akamkaribisha mfalme. KIJANA: Karibu sana Mtukufu mfalme, tumefurahi kukuona maana ukweli utadhihrika mbele yako.. MFALME: Sawa lakini endapo sitaona kitu chochote mahara hapa nawaahidi adhabu ya kifo itakuwa juu yenu sitakuwa na msamaha na mtu, na wala sitaangalia umuhimu wenu hapa kijijini. Japokuwa mfalme alikuwa akiongea maneno makali, wao hawakuogopa maana waliamua kujitolea kwa ajili ya kijiji chao, waliendelea kuongea nae huku baadhi yao wakiwa makini kuangalia kwenye kile kichaka wakisubilia kuona nini kitatokea. Mda ulienda bila ya mafanikio ya kuona kitu chochote hofi zikaanza kutawala nafsini mwao vijana wale kila walipokuwa wakikumbuka maneno ya Mfalme, baadhi yao walijuta na kujirahumu kwanini walienda kumpa taarifa mfalme lakini walikuwa wameshachelewa. ilipofika majira ya saa sita usiku wale vijana walijishukuru na kuona wameshindwa kuifanya ile kazi na kuhisi walidhania kitu kisichokuwa kweli, ndipo wakaamua kulala wakisubilia adhabu yao ikifika kesho yake asubuhi. Kwa upande wa mfalme hakuitaji kulala alijitahidi kupambana na usingizi ilimradi aone kile walichokisema vijana, japokuwa wenyewe walikata tama na kukili wamekosea. Sasa kwa upande wa Sube na mke wake na wao walikuwa macho wakiongea kuhusu Yoka. SUBE: Kuna wazo nimelipata kuhusu Yoka. BIBI SUBE: Wazo gani . SUBE: Ninaona huyu nyoka tumwamishe tumpeleke msituni awe anaishi huko maana naona kama watu wameanza kutuchunguza. BIBI SUBE: Sawa sio vibaya kama umeona hivyo, kwahiyo huku kijijini hata onekana tena. SUBE: Ataonekana ila sio sana, ila sasa hivi ninataka awe anaenda mpaka kwenye kijiji cha Mbui kwa mfalme Koe ilituzidi kujulikana. BIBI SUBE: Sawa nimekuelewa. SUBE: Sawa, alafu twende tukamuangalie mdudu mwenyewe maana tuna siku nyingi hatujamwangalia. Wakanyanyuka kuelekea kwenye kile kichaka, wakikwa awajui hili wala lile linaloendelea zidi yao. Mfalme wakati anaendelea kuangalia angalia huku macho yake yakilazimiisha kufumba, Ghafla akamuona Sube akiwa ameongozana na mke weka, kisha wakatazama pande zote kama mwizi anapoenda kuiba. Mfalme akashtuka na kufikicha macho yake yaliojaa ukungu kutokana na usingizi mzito aliokuwa nao, kisha akatulia na kuangalia kwa makini nini wawili wale wanataka kufanya. Sube alipoona nje hakuna mtu yoyote akaanza kupiga mluzi mara kwenye kile kichaka akatoka nyoka mkubwa mwenye kung’aa na kusogea walipo wawli wale. Mfalme alishtuka sana utadhani yule nyoka alikuwa amemfuata yeye alitamani kupiga makelele kutokana na uwoga lakini akajikaza kiume na kuendelea kuangalia nini kitafanyika. Sube akachuchumaa na kumpaka unga Yoka kisha akaongea maneno Fulani ambayo mfalme hakusikia kisha nyoka akaondoka, wawili wale na wao wakarudi ndani kulala maana walikuwa tayari wamemaliza kazi yao. Mfalme alisikitika sana kisha akawatazama wale vijana alitamani awaamushe ili awaambie kile alichoona lakini moyo wake ulisita, kutokana na ukaribu aliokuwa nao yeye na mzee sube, Ndipo akaamua kulala huku mawazo mengi yakitawala kichwa chake maana alikuwa ajui aanze wapi kuwaambia wanakijiji pamoja na wale viongozi kuhusu swala lile. ilipofika asubuhi na mapema mfalme aliamke na kurudi nyumbani kwake bila kumuaga kijana yoyote pale ndani maana wao walikuwa bado hawajaamka. Alipofika kwao mda wote alikuwa mtu wa kijiinamia, jambo ambalo lilimshangaza sana mke wake kwa sababu haikuwa kawaida yake kuwa vile, ndipo akahitaji kufahamu nini kimemkuta huko atokako. MKE: Mume wangu mlikoenda mlifanikiwa au wale vijana walikuwa wanamsingizia yule mzee wa watu. Mfalme kwa kuwa hakutaka mzee sube ajulikane akaona bora amdanganye mke wake japokuwa hakupenda kufanya hivyo. MFALME: Hapana hatujafanikiwa maana hatukuona kitu chochote kwahiyo sijui kama wanamsingizia au laa. Mfalme aliongea huku akiwa na wasiwasi na kumfanya mke wake ahisi kitu Fulani. . MKE: Mh! Ila kutokana na unavyoongea naoka kama sio kweli unavyonimbia . MFALME: Kwanini unasema hivyo mke. MKE: Nakuona jinsi unavyoongea una wasiwasi sana . MFALME: Hapana mbona nipo kawaida, na wala sijakudanganya. MKE: Sawa ila naomba uniambie kwanini tangu umerudi umekuwa mtu wa mawazo wala hauna furaha kuna kitu gani kimekukwaza huko utokako. Mfalme baada ya kuulizwa vile, akamtazama mke wake na kuamua kumwambia ukweli wa kile kilichotokea. MFALME: Mke wangu kwanza naomba unisamehe kwa kutokukuambia kweli kuhusu kule nitokako. Ila jambo ambalo walikuja kilisema wale vijina kuhusu mzee sube ni kwel kabisa tena nimeshuhudia kwa macho yangu mwenyewe, na nimegundua kitu kumbe mzee Sube ndie mwenye yule nyoka. Mke wa mfalme alishangaa sana kusikia vile maana na yeye alitokea kumuamini mzee sube kama alivyokuwa akiaminiwa na mume wake. MKE: Eeeeeee ! Mume wangu kwahiyo unataka kuniambia kumwamini kote kule kumbe ni mbaya kias hiko. Sasa baada ya kuona hivyo umechukua huamuzi gani. MFALME: hapa kichwa chote kinawaka moto maana hata sijui cha kufanya kwa mzee yule. Alafu kitu kingine, jambo hili nataka iwe siri yangu mimi na wewe tu maana watu wengene wakisikia wanaweza kudhania kuwa mimi na mzee sube tulikuwa tunashilikiana kufanya jambo hili kutokana na kuwa karibu nae. MKE: wewe unataka iwe siri wakati wale vijana na wao wamemuona huyu mzee sube. MFALME: Hapana hawakumuona walikuwa wamelala. MKE: Sawa ila mume wangu mzee sube inabidi ahukumiwe kama watu wengine wanavyofanya kitu kibaya hapa kijijni kwetu. MFALME: sawa ila kabla sijafanya hivyo ninataka nimuite ili nimuonye endapo atarudia au ataendelea kufanya vile nitamuhukumu. MKE: Mh! mume wangu bado unataka kumtetea mzee sube ila basi kwa kuwa wewe ndio mfalme fanya utakalo. Waliendelea kuongelea jambo lile na mwishoe wakaachana nalo huku mke akimshangaa mfalme kwanini amekuwa akimtetea Sube kiasi kile. Kwa upande wa wale vijana walishtuka sana baada ya kuamku maana hawakutegemea kuona mfalme ameondoka mahara pale bila kuongea na wao, hofu ilitawala kwao, kila mmoja alimuuliza mwenzake nini ameona ule usiku lakini hakuna jibu liliopatikana maana wote walikuwa wamelala fofofo. Wote kwa pamoja wakaanza kupanga mipango jinsi gani wafanye ili mfalme asiwape adhabu ya kifo maana walikuwa awajui, nini mfalme ameona mwishowe wakapanga kwenda kumuomba msamaha endapo atakataa basi watakuwa tayari kupokea adhabu hiyo. Wakiwa wanaendelea kuongea ghafla wakasikia mlango wa ile nyumba ukigongwa kuashiria kuna mtu anataka kuingia humo, mapigo ya mioyo yao yakaanza kwenda mbio maana walihisi wamekuja kuchukuliwa na askari wa mfalme ili wakapewe adhabu yao. Japokuwa walikuwa wanaogopa lakini hawakuwa na jinsi mmoja wao akanyanyuka kwenda kufungua mlango na kukutana na kijana mwenzao anaeshughulika kule kwa mfalme, haraka akaingia ndani. Akasalimiana na wenzake kisha akaanza kuwaeleza nini kimempeleka mahara pale. KIJANA: Nimeagizwa na mtukufu mfalme nije kuwapa taarifa anawahitaji majira ya mchana mfike nyumbani kwake. Taarifa ile ilizidi kuwatisha na kujua kuwa mda wao wa kuishi hapa duniani umefika tamani, Yule mtoa taarifa alipomaliza akaondoka zake na kuwaacha wenzake wakiwa wamejiinamia. Waliendelea kukaa mle ndani kila mmoja akiwa na mawazo yake na hatimae mda walioambiwa waende kwa mfalme ukawadia, wakatoka kwenye ile nyumba na kuanza safiri ya kuelekea huko, Kwa kuwa ni vija walitembea kwa mwendo wa kijeshi { haraka } mda mfupi mbele wakafanikiwa kufika huko, na kamkuta mfalme akiwa amekaa pamoja na mke wake, wakawasalimia na kusubilia kuambiwa walichoitiwa, ndipo mfale akaanza kuongea. MFALME: Nimewaita hapa ninataka mniambie nani kati yenu ameona kitu kwa mzee sube, maana nyie mlisema yeye ndie msababishaji wa mambo yote. Wale vijana baada ya kuulizwa vile, walijikuta viungo vya miili yao vikifa nguvu na kulegea maana moja kwa moja wakagundua kuwa mfalme na yeye hakubahatika kuona kitu chochote kwa Sube, kumbe Mfalme aliwauliza vile kama kuwatega ili aone kama kuna ambae alikuwa ameona kile alichokiona yeye kwa mzee sube. Wale vijana walikaa kimya na kuinamisha vichwa vyao chini kuashiria hakuna kitu walichokiona, Mfalme alipoona vile akaona bora awaambie ukweli kile alichokuwa amekioa yeye japokuwa alihitaji afanye siri. MFALME: Najua hakuna hata mmoja ambae ameona kitu kwa kuwa mlilala, ila mimi nilifanikiwa kuona kila kitu kwa mzee sube na sasa naamini yale maneno ambayo nyie muliniambia. Vijana hawakuamini kile walichokisikia haraka waliinua vichwa vyao na kumtazama mfalme huku furaha ikitawara nafsini mwao na kufukuza huzuni, walipongezana kwa kazi mzuri walioifanya lakini mwisho wakahitaji kufahamu nini mfalme atafanya kwa mzee sube. . KIJANA 1: Tunashukuru sana mtukufu mfalme kama umeliona jambo hili maana sisi tulikuwa na wasiwasi tulidhani na wewe haukuona kitu chochote. Ila tunahitaji kujua kitu gani umepanga kumfanyia mzee Sube. Baada ya kuulizwa vile akaa kimya kwa sababu yeye hakutaka kufanya kama wao walivyokuwa wakidhania atafanya kwa yule mzee, lakini mwisho akaona bora awaambie ukweli jinsi yeye alivyopanga kufanya kwa Sube. Lakini mda huo Sube na mke wake walikuwa awajui chochote kuwa tayari wamefahamika wao ndio wabaya wa kile kijiji bali waliendelea kufanya shughuli yao ya kutibu watu walioumwa na yule nyoka. MFALME: Mimi sina lengo la kumpa adhabu mzee sube kwa kuwa hii ni mara yake ya kwanza kokosea hapa kijijni. Kwahyo nataka nimuite ili nimuonye na endapo ataendelea kufanya hivi hapo nitampa adhabu. Jibu la mfalme liliwashangaza sana wale vijana maana wao walijua kama mfalme ameshajua ukweli kilichobaki ni hukumu kwa mzee sube. Lakini vijana hawakukata tama wakaendelea kumuuliza maswali kutokana na uamuzi aliouchukua. KIJANA 2: Lakini mfalme sheria ya hiki kijiji chetu inasema mtu akifanya jambo la kuhatarisha maisha ya wenzake kwa makusudi anatakiwa kupewa hukumu ya kifo mbele ya wanakijiji. Sasa inakuaje mzee sube unataka kumuonya na wakati yeye inatakiwa ahukumiwe kifo. MFALME: Ni kwel kijina unachosema ila kwa hili ninaomba mnisamehe maana siwezi kumuhukumu haraka hivi kwa kuwa kwa sasa najua ana mambo mengi hapa kijijini pia amekua akitoa mawazo na ushauri mzuri kwangu jinsi ya kuongoza hiki kijiji. Kwahiyo endapo nitachukua uamuzi wa kumuua nitakuwa nimempoteza mtu muhimu kwangu. Jibu la mfalme liliwaacha vijana mdomo wazi na kuhisi kitu Fulani kutoka kwake, maana kosa alilolifanya sube hakutakiwa kutetewa na mtu yoyote yule. Kwa kuwa mfalme ameshaamua kufanya hivyo wale vijana ikabidi wakubari kuwa wapole japokuwa waliumia kupita kiasi. Lakini kabla awajaondoka kijana mwingine akauliza swali. KIJANA 2: Mtukufu mfalme hivi mtu muhimu anaweza kufanya jambo baya na hatari kama hili, hivi unajua nia ya yeye kufanya hivi, inakuaje kama alikuwa anahitaji kukuangamiza wewe. { Kijana aliongea hivyo ili kumjengea chuki mfalme lakini mfalme hakujali } MFALME: Hayo unayoniuliza ni sahihi ila jua kuwa na yule ni binadamu kuna siku anakuwa anapitiwa na shetani na kujikuta akifanya vitu kama vile. Kwahiyo ni wajibu wetu kumrudisha mzee sube kutoka kwa shetani. Maneno ya mfalme yalimchukiza sana mke wake pamoja na wale vijana, ndipo mke akadakia na kuanza kuongea maneno ya kumshangaa kwanini anafanya vile. MKE: Hivi mume wangu kwani huyo mzee sube amekufanyia kitu gani kizuri mpaka umtete kiasi hiko kama washauri si utampata wingine mbona wazee wamejaa hapa Mbaka. Mara ngapi umewahukumu watu ambao ilikuwa ni mara yao ya kwanza kukosea au ndio unataka kubadilisha sheria. Ila kumbuka ulimuhukumu mke wako uliempenda sana pamoja na mkwe wako kwa kosa ambalo lilikuwa la kwanza wao kulifanya hapa kijijini au wale hawakuwa na umuhimu kwako na kwa hiki kijiji. Amka mume wangu huyu mtu unaemtetea leo ni zaidi ya Shetani kwa hiki kitendo alichokifanya kwetu sisi pamoja na hiki kijiji chetu cha mbaka. SEHEMU YA 11 JINA : NYOKA WA KUTUMWA SEHEMU YA 11 ……………… Ilipoishia ………………. Maneno ya mfalme yalimchukiza sana mke wake pamoja na wale vijana, ndipo mke akadakia na kuanza kuongea maneno ya kumshangaa kwanini anafanya vile. MKE: Hivi mume wangu kwani huyo mzee sube amekufanyia kitu gani kizuri mpaka umtete kiasi hiko kama washauri si utampata wingine mbona wazee wamejaa hapa Mbaka. Mara ngapi umewahukumu watu ambao ilikuwa ni mara yao ya kwanza kukosea au ndio unataka kubadilisha sheria. Ila kumbuka ulimuhukumu mke wako uliempenda sana pamoja na mkwe wako kwa kosa ambalo lilikuwa la kwanza wao kulifanya hapa kijijini au wale hawakuwa na umuhimu kwako na kwa hiki kijiji. Amka mume wangu huyu mtu unaemtetea leo ni zaidi ya Shetani kwa hiki kitendo alichokifanya kwetu sisi pamoja na hiki kijiji chetu cha mbaka. …………….. Endelea ……………………….. Baada ya kusemaa vile kwa asira akaainuka na kuingia ndani na kuwaacha wale vijana wakiendelea kusubilia, Japokuwa maneno ya mke yalikuwa makali lakini hayakuweza kubadilisha msimamo wa mfalme, jambo ambalo lilizidi kuwachukiza wale vijana. walipomaliza kuongea wakaruhusiwa warudi majumbani kwao huku wakiwa wamepewa onyo endapo baya lolote litamkuta mzee Sube hukumu itakuwa juu yao, vijana wakaondoka huku wakisononeka. Baada ya kupita dakika kadhaa Mfalme akachukua walinzi wawili na kwenda nao nyumbani kwa sube na kumkuta akitengeneza dawa, sube akafurahi sana alipoona ametembelewa na Mfalme akamkaribisha vizuri kama sio yeye anaefanya mabaya, akaenda ndani kumuita mke wake, mda huo alikuwa ajui lolote bali alijua mfalme ameenda kumtembelea tu. Wakasalimiana nae ndipo Mfalme akamuomba Sube wasoge pembeni ili waonge kidogo, bila uwoga sube akasogea na kumuacha mke wake akiwa pamoja na wale walinzi, ndipo maongezi yakaanza. MFALME: Mzee sube nimekuja hapa kwa ajili ya jambo moja ambalo limenisikitsha sana baada ya kufahamu ukweli wake. Sube alipooambiwa vile hakuogopa maana alijua hilo jambo litakuwa linamuhusu mzee Bugu kwa kuwa yeye ndie alizaniwa kufanya mambo mabaya. MZEE SUBE: mmmmh !!!. Jambo gani hilo mtukufu mfalme. { Aliuliza bila uwoga } Sube alipouliza hivyo, Mfalme akaa kimya kwa huku akimtazama na kujiuliza wapi aanze kumwambia, mwishoe akaamua kuongea . MFALME: Kuhusu nyoka anaesumbua hapa kijijni. MZEE SUBE: Ehe niambie umegundua ukweli gani kuhusu huyo nyoka. { alijifanya kuongea kwa mshangao mkubwa } MFALME: Sube usijifanye kushangaa wakati wewe ndie muhusika wa jambo hili. Mlipuko mkubwa mithiri ya bomu la nyukilia ulitokea kwenye moyo wa Mzee sube na kuanza kutetemeka maana hakutegemea kusikia kile alichoambiwa na mfalme, lakini akajitahidi kujikaza na kuendelea kuongea. MZEE SUBE: Sijakuelewa mtukufu mfalme. MFALME: Lazima usinielewe kwa kuwa ukweli umejulikana, sasa nataka uniambie yule Nyoka ulieniambia anaitwa Ruka wa nani. { Mfalme aliongea kwa hasira } Sube alikataa na kusema amfahamu mwenye yule nyoka lakini mfalme aliendelea kum’bana na mwishoe sube akakosa kitu cha kujitetea na kubaki akiwa ameinamisha kichwa chni kuashiria kukubali lile kosa, Mfalme alisikitika sana alipoona jambo lile ndipo akaanza kumuonya. MFALME: Sube nilikuamini sana na sikufikiria kama wewe ungekuwa muhusika wa jambo hili nimekufanya uwe mshauri wangu na ukanishauri mambo mazuri kumbe ulikuwa ukiniuma huku unapoliza, kwanini uliamua kufanya hivi nimeumia sana nilipofahamu ukweli huu. ujio wangu kwako nimekuja kukupa onyo mzuie huyo yoka wako, na usirudie tena kufanya jambo hili maana sitakusamehe tena bali hukumu ya kifo itakuwa juu yako kama nilivyofanya kwa wenzako waliosababisha matatizo hapa kijijini. Aliposema hivyo akawachukua walinzi wake na kuondoka nao bila kuaga huku akiwa na hasira, kitendo kile kilimshangaza sana bibi sube na kujiuliza nini kimetokea, haraka akakimbilia sehemu aliyokuwa mume wake na kumkuta akiwa amesimama huku ameinamisha kichwa chini kama mtu alieonewa, ndipo akaona bora amuulize kilichotoekea. BIBI SUBE: Meme wangu kwani kimetoke nini mbona mfalme ametoka kwa hasira vile. Sube hakujibu kitu na kuendelea kuinamisha kichwa chake chini, jambo ambalo lilizidi kumchanganya bibi sube. BIBI SUBE: Mume wangu kwani si ninakuuliza au aunisikii, kimetokea nini kati yako na mtukufu mfalme. Sube aliopna mke wake ameng’ang’ania jambo hilo ndipo akamjibu huku misuri ya kichwa ikiwa imemsimama kutokana na kuchukia yale maneno ya mfalme. MZEE SUBE: Mfalme amegundua ukweli kuhusu Yoka nahisi kuna mtu amemwambia. Bibi sube alishtuka kupita kiasi na kuishiwa nguvu ya kusimama BIBI SUBE: Eeeeeeeee !! Mume wangu mfalme amejua kweli ?. Sasa itakuaje jamani si kufa huku mume wangu. aliposema hivyo Sube akajibu huku akiwa na jaziba kama mtu aliefumania ugoni au kuona mtoto wake akipigwa na jirani. MZEE SUBE: Hafi mtu eti anasema amenisamehe ila nisirudie tena, chamoto watakiona sitajificha tena na nitafanya juu chini mpaka mfalme na yeye nimuangushe madarakani, na huyo alieenda kumwambia nikimgundua lazima arudi kuwa mavumbi, sipendi mtu aingile mambo yangu. BIBI SUBE: Hapana mume wangu kama tumesamehewa tuachane na mambo haya tutakufa. MZEE SUBE: Siogopi kufa na leo Mfalme ama zake ama zangu. BIBI SUBE: Kwahiyo unataka kumfanya nini. MZEE SUBE: Subilia utaona ikifka usiku. Sube akatoka na kwenda kusikojulika na kumuacha mke wake bado akiwa amekaa pale pale chini, Bibi sube alisikitika sana na kujirahumu kwanini alikubali wafanye jambo lile lakini alikuwa ameshachelewa kuwaza jambo hilo. Mfalme alipofika nyumbani kwake kama kawaida mawazo yaliendelea kumtawala huku ajirahumu kwanini alimuamini mzee sube haraka vile mpaka inapelekea anashindwa kufanya hukumu inayo mstahiri. alijirahumu kwanini alikuwa akifanya mambo bila kuomba ushauri kwa wazee wengine na kusababisha kuondoa viongozi waaminifu na kumuweka mzee sube. Masaa yalienda hatimae usiku ukafika, Sube na mke wake wakajiaanda vizuri kufanya kazi yao kisha wakaenda nyumbani kwa mfalme kwa nija ya kichawi, na kumkuta akiwa amelala fofofo pamoja na mke wake, Ndipo wawili wale wakaanza kuimba na kucheza zile nyimbo zao za kichawi huku wakizunguka kitanda cha wawili wale. Mda huo Yoka na yeye alikuwa akizini kuuma watu kwa kasi maana Sube aliamua kufanya ubaya zaidi kwa wanakijiji wote. Walipomaliza kucheza Sube akachukua unga na kumlisha mfalme huku akisema maneno ikiwa kama kunuia kile anachomlisha. MZEE SUBE: Wewe mfalme ninapokulisha unga huu ninataka usiwe na kauli yoyote kwangu na kila nitakachokisema mimi ukakikubali mara moja. Na endapo utaenda kinyume kifo kiwe juu yako. Bibi sube akachukua maji yaliyokuwa kwenye kibuyu na kumnywesha mfalme, kisha wakatoeka na kutokea nymbani kwao huku wakiwa na furaha kutokana na kufanikiwa jambo lao. Ndipo Sube akaanza kumueleza mke wake vitu gani anatakiwa yeye afanye ikifika kesho yake ili ile dawa ikamilike asilimia zote. MZEE SUBE: Mke wangu mpaka sasa hivi kazi tulioifanya imefikia asilimia Hamsini kwahiyo bado hamsini zingine ili kazi yote ikamilike kabisa. BIBI SUBE: Kwanini umesema hivyo. MZEE SUBE: Hii dawa itakamilika kesho asubuhi inabidi mimi nikamuamushe mfalme kabla ajaamka yeye mwenyewe au kuamshwa na mtu mwingne yeyote na endapo nitafanikiwa kufanya hivyo dawa itakuwa tumeifanikisha kwa asilimia zote.. Bibi sube hakua na chakuongea zaidi ya kumuomba mume wake awe makini atakapoenda huko kwa mfalme, wawili wale wakala. Mfalme akiwa kwenye usingizi alianza kuota ndoto. Alikuwa yeye pamoja na mzee sube wakiwa wanatembe huku na kule katika kijiji chao huku mzee sube akiwa amebeba ule unga wenye rangi nyeupe na nyekundu na begani mwake alikuwa amembeba yule nyoka anaeitwa YOKA.Wakati wapo katikati ya safari ghafla mzee sube akaanza kurefuka na kuwa mkubwa, hapo hapo mfalme akabadirika na kuwa kama mtoto wa miaka minne au mtano, ndipo Sube akaanza kumcheka na kuongea maneno ya kumdharau. MZEE SUBE: Hahahaha nahisi jeuri yako imefika mwisho. Siku zote siwezi kuongozwa na mtoto mdogo kama wewe na utakuwa ukifuata kila nitakachokuambia mimi. Kisha akachukua ule unga na kumlisha,,,,,,, ghafla mfalme akashtuka kutoka usingizini na kukaa kitako huku akiitafakari ile ndoto. Mda mchache mbele mke na yeye akaamka na kumkuta mfalme akiwa amekaa akamuuliza tatizo, mfalme bila kuficha akamwambia nini ameota, mke alisikitika sana na kumwambia itakuwa mizimu imeamua kukuonyesha ubaya wa mzee sube kwahiyo kazi kwake kumuhukumu au kumsamehe kama alivyosema yeye mwenyewe. Maneno ya mke wake yalimgusa na kumfanya abadili ule uamuzi wake, akatoka nje na kuchukua walinzi kadhaa na kwenda nao mpaka nyumbani kwa mzee sube, mda huo ilikuwa yapata majira ya saa kumi na moja alfajiri. Walipofika nyumbani kwa mzee sube ndipo mfalme akafungua mlango na kuingia ndani bila hata hodi na kukuta wawili wale wakiwa bado wamelala. Akaamuru wale walinzi wawachukue,,,, Sube na mke wake walishtuka kuona mfalme amekuja kuwakamata maana hawakutegemea kabisa kutokea jambo hilo. Bila kuchelewa walinzi wakafanya kama walivyoambiwa wakawachukua na kuwapeleka mpaka mbele ya nyumba ya mfalme ambako huko ndiko utolewa hukumu. Kijana mmoja akaenda kupiga ngoma ya dharula ili wanakijiji wasogee sehemu ile washuhudie hukumu itakayo tolewa kwa mzee sube na mke wake. Watu wengi walijiuliza kitu gani kimetokea mpaka ikapigwa ile ngoma maana wengi wao walikuwa awajui nini kinaendelea pale kijijni. Kutokana na shahuku waliokuwa nayo haraka walitoka majumbani kwao na kuwasili nyumbani kwa mfalme na kukuta wawili wale wakiwa wamefungwa kwenye mti uliopo sehemu hiyo. Watu wengi walishangaa kuona sube na mke wake wapo sehemu ile pia wale wazee na wao walishangaa na kujiuliza nini sube amefanya mpaka afikie hatua ile wakati alikuwa mtu wa karibu na mfalme. Lakini maswali ya watu wote waliofika sehemu ile yalijibuwa baada ya Mfalme kueleza kosa la watu wale. MFALME: Jamani nimewaita hapa kwa ajili ya kuona hukumu ya watu hawa kwa kosa la kutengeneza nyoka ambae ameleta madhara makubwa sana hapa kijijini kwetu na kusababisha vifo vya wenzetu wengi. Maneno ya mfalme yalisababisha kutokea kimya kisichokuwa cha kawaida kutokana na watu wote kubaki vinywa wazi, kutokana na kuto amini kile walichokisia, mara minong’ono ya chinichini ikaanza ndipo mfalme akaendelea kuongea. MFALME: Siku zote tumekuwa tukikataza watu kufanya mambo kama waliofanya wawili hawa na hukumu kali tumekuwa tukitoa kila anapopatikana mkosa lakini bado watu wanajifanya awaelewi wanaendelea kufanya mbambo yao, kwahiyo kutokana na kosa walilolifanya wanaukumiwa kifo kwa kupigwa mawe mpaka mwisho wa uhai wao. Mfalme aliposema vile baadhi ya watu walipiga makofi na kushangilia jambo lile lakini wengine waliwaonea huruma na kutamani wangewasamehe, lakini kwa kuwa hukumu ilikuwa tayari imetoka basi hakukua na jinsi. mfalme akaendelea kuongea. MFALME: Ila kabla ya yote napenda kutoa shukrani kwa vijana wa hiki kijiji kwa kazi yao kubwa walioifanya mpaka tukafanikiwa kumpata msaliti na hadui kwetu, na kuanzia sasa wale vijana wote walioshiriki kutika kumpata mbaya wetu watukuwa askari wangu. Ila kuna kitu nimejifunza sio kila anaekuchekea ni mwema kwao bali mda mwingine anasubilia ugeuze kisogo ili atoe makucha yake, nilimuamini sana huyu mzee na alikuwa akinipa ushauri mzuri kumbe huyo huyo ndie adui kwangu na kwa wanaichi wangu. ….. kwahiyo kuanzia sasa hukumu itolewe kwa watu hawa. Ndipo wakaja baadhi ya askari wakiwa wamebeba mawe na kuweka mbele yao, walipomaliza kazi hiyo ndipo waanza kuwarushia. Wakati wanafanya vile, ghafla kwenye kichaka akichoishi Yoka kikaanza kuwaka moto na kutekete Yoka akiwemo ndani yake. Wale askari wakaendelea kuwapiga huku umati wa watu wakishuhudia jambo lile mpaka wawili wale walipokata roho, wakachukuliwa na kwenda kutupwa msituni kuwa chakula cha wanyama na wadudu waishio huko……. Na Huo ndio ukawa mwisho wa Sube, mke wake pamoja na Yoka, kuanzia hapo kijiji kikarudi kuwa na amani kama dhamani na wawili wale wakabaki kuwa kama stori hapo kijijini. MWISHO ASANTENI KWA SUPPORT YENU NA KUNIFUATILIA KILA NILIPOKUWA NIKITUMA HII STORI SINA CHA ZAIDI, BALI JIANDAENI KUSOMA STORI NYINGI TUTAENDELEA NA UTAMU WA KAKA FUNDI

at 1:27 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top