Home → simulizi
→ EPISODE 2: MAPENZI YA JINI LA MAJI
Mwandishi: Dominick Chuwa
Whatsapp: 0787325447
........ILIPOISHIA.........
Ulitokeza mkono wa binadamu kutoka chini ya maji nakuanza kueleke kama unataka kumshika ule mguu wa Ashura uliobaki ndani ya maj............SASA ENDELEA.....
Mda ule Ashura ni kama alipata msisimko kuwa kuna kitu kinataka kumgusa au kumfatilia kwa sababu zile kelele za maji wa ule mkono kutembea ndio zilimpa hisia hizo.
Hakutaka kuendelea kupandisha tena ule mguu alisubiri hicho kitu kinachokuja mpaka akione labda alizani ni samaki.
Kiganja cha mkono uliotokeza ndani ya maji mto ule kilienda moja kwa moja mpaka karibu ya mguu wa Ashura ndipo kiganja kilitua katika ngozi laini na yenye kuvutia kwenye mguu wa ASHURA.
Kile kitendo cha mkono kugusa mguu wa ASHURA, binti yule alishtuka sana kiasi kwamba mpaka maji yalimwagika kidogo, japo alijiandaa kuona kinachokuja lakini aliogopa kwa sababu ya msisimko aliopata.
Ndoo ikiwa kichwani na presha imepanda lakini mara hali ile ya kushtuka na mshangao ilimpotea ikaja Sura ya furaha na mapozi ya madaha ambayo sio rahisi kwa mrembo kutoe tabasamu kama lile pasipo kuwa na sababu.
Aligeuza shingo yake taratibu mfano wa twiga aliyeona majani mti wa nyuma.
Macho yake yalieleke moja kwa moja juu ya maji palipokua na mkono ambao mda huu ulimuaccha kumgusa.
Ashura alipoona vizuri alicheka kwa kuonesha meno kisha alitamka maneno yaliyoaambata na tabasamu zito
"Si uibuke juu na wewe" ni maneno ya kushangaza sanaa alisema ASHURA kuongea na ule mkono.
Lakini katikaa hali ya kushangza yale maneno yake baada ya sekunde chache kulianza kuibuka kichwa cha binadamu kilichosukwa nywele aina ya Dredi au rasta kwa jina lingine, tena rasta zile zilifanana na maua aliyotoka kushika Ashura mda sio mrefu uliopita..
Alitokeza juu pole pole rasta zake ndio zilimfanya yule binadamu aliyotokea chini ya maji kuvutia kila alipoangaliwa.
Alipoibua sura yake ilipofika juu ya maji wakakutana macho kwa macho na ASHURA hapo ndipo wote wawili walicheka.
"Hahaha SHIKOROBO na wewe una vituko, kumbe mda wote nilipokuwa hapa mtoni uliniona ukawa unanitega tu hukutokeza na nilitaka kuondoka bila kukuita"
Maneno ya ASHURA aliyasema huku akitua ndoo ya maji kuweka pembeni tena.
*************
SHIKOROBO kama jina alilopewa na miungu pia na majini ya maji. Alikua ni JINI lililoishi kwenye maji miaka mingi tangu enzi na enzi ila hakuzeeka wala kufa alibaki katika hali yake ya ujana na nguvu.
Aliishi katika ule mto chini ya kina kabisa ambapo ndio kuna falme yao ambapo hakuna binadamu yeyote aliyegundua kama mule ndani chini ya maji kuna majini watu wanaishi.
Wanakiji wa kijiji cha COCOA hapo awali walikua hawana tabu ya maji kuchafuka wala kukauka lile tatizo liliawatokea karibuni tu tena ghafla.
Sifa kuu ya SHIKOROBO jini lile maji aliwapenda wanadamu hasa waanawake kwa kusikia story zao kwamba wanawake wengi DUNIANI wanateswa hivyo alijikuta kuwaonea huruma na kuwachukia Wanaume ile mbaya.
Licha ya SHIKOROBO kuishi chini ya maji na majini mengine ila yeye peke yake ndio alikua ana uwezo wa kutoka nje ya uso wa Dunia na kuangalia mazingira ya maji.
Alipenda kutoka kila ifikapo usiku au mchana kuwaangalia wanadamuu waliokuja kuteka maji kwenye ule mto bila ya yeye kuonekana kwa sababu alijifcha ndani ya maji.
Ila ni siku moja ndio alijikuta anampenda binti wa Duniani tukio lilikua hivi.
ASHURA hapo awali walipenda kwenda mtoni na Kaka yake ambaye ni mkubwa kiumri. Na hii ni kutokana na wazazi wake kuona kwamba kama wanaume wengi wanamfatilia wanaweza kumbaka hivyo walifatana na kaka yake mtoni kilaa mara na mda wowote ule.
Kwa kawaida watoto wakifatana kuzaliwa yani kama wa kwanza na wa pili au watatu na wanne hawawezi kupatana siku zote lazima kuwe na mkwaruzo vivyo hivyo ndio ikawa kwa JUMA kaka yake ASHURA kila walipokua pamoja walijikuta wakigombana licha ya wazazi wao kuwasuluhisha ugomvi kila wakati
"Kaka, yule MBONI ata sio mzuri kwanza naona ni kama malaya wala usimchumbie" maneno yale aliyasema ASHURA siku Siku moja walipokua na JUMA mtoni wakiteka maji.
"Ashura nishakwamkbia sitaki unifagilie kuhusu wapenzi wangu mbona unataka kukatisha mahusiano yetu kila ninapolta mpenzi? Mbona wewe huolewi unakaa nyumbani kujaza choo tu" alijibu Juma siku hiyo akiwa ana hasira ile mbaya.
"Hahahaha! Kaka unajua nini wewe hutaki kushauriwa mimi sitaki kuolewa na maana yangu, sasa wewe mwenzangu unaelekea kuwa babu bado hujaoa na unaendelea kuchagua mabibi machangudoa kama Mboni" walijibaza kwa meneno makali ya kashfa Ashura akichukizwa na mahusiano baina ya kaka yake na huyo binti waliyemuita mboni.
Lakini Juma hakuelewa na ubishano uliendelea pale mtoni mpaka kufikia JUMA kufura kwa Hasira kupelekea kumpiga Ashura.
Ashura alichezea kichapo kutoka kwa kaka yaKe bila ya mtu yeyote kumuokoa kwa sababu waliku wako mtoni mda ule.
Juma alipomfinya vya kutosha yeye akachukua ndoo yake nakuondoka akimuacha Ashura peke yake kule mtoni.
Ashura alikaa pembeni ya mto akaanza kulia kwa nguvu na kwikwi za Hasira kwa kile kichapo alichopokea kutoka kwa kaka yake, alijuta kumwambia vile na akakoma vilivyo.
Lakini kumbe wakati analia na pia wakati alivyopigwa yule JINI la maji SHIKOROBO siku hiyo hakuwa mbali ya kina kwa hiyo alisikia na kuona yote na kile kilio cha Ashura kilimgusa sana, mpaka alijikuta anaibuka kitendo ambacho hakuwahi kufanya kwa binadamu yeyote yule kumuona.
Mara ya kwanza ASHURA kumuona Shikorobo kutokeza ndani ya maji ilikua kidogo akimbie kwa zile rasta zake pia hakuwahi kumuoma katika kile kijiji chao kwa hiyo kwake ilikua ni kama mshtuko wa aina yake.
Machozi yaliacha akawa anahema kwa Nguvu kumuogopa Shikorobo.
"Usiniogope mimi sio mbaya, nimesikia kilio chako na nataka kukusaidia" yalikua ni maneno ya kwanza kutoka kwa Shikorobo ambayo Ashura hawezi kuyasahau.
Ashura kuona kwamba ni binadamu japo hakutokeza mpaka chini aliishia kwenye kiuono alitulia kwa sababu walielewana lugha.
Hapo ndio ikawa mwanzo wa urafiki wa shikorobo pamoja na Ashura.
ASHURA alimwambia mambo mengi Shikirobo kuhusu familia yao na jins kaka yake anavyompiga. Shikorobo alijikuta anamchukia JUMA mara mia zaidi ya wanaume wengine anaowachukia basi alimbembelrza ashura na kumfairji ndio maswala yakuanza kujuana yalipoanza.
Kila mmoj alieleza sehemu aliyotokea na Ata shikorobo kusema kwamba yeye ni Jini la pale majini ASHURA bado hakumuogopa tena.
Siku hiyo Shikorobo kuonesha kwamba amechukizwa na kile kitendo alimwambia Ashura.
"Nataka nikufundishe wimbo ambao ukikuta maji machafu ukiimba lazima yawe masafi kwa maana kuanzia sasa nataka kuchafua haya maji kwa sababu watu wakijiji chenu wanatumia vibaya" Ashura kwanza alishangaa.
"Yatakuaje machafu yote wakati ni mengi sana?"
"Hapana sio kama unavyofikiri mimi nina uwezo mkubwa sana kwa hiyo usijali nitakufundisha nyimbo mbili moja, ya kufanya maji yawe masafi na nyingine wa kuniita mimi kutoka ndani ya maji kama utanihitaji"
Ashura hakuamini maneno ya JINI lile kwa sababu aliona kama miujuiza alichukulia poa tu. Itakuaje maji mengi ya mto mkubwa vile kuchafuka wakati miaka yote hayakuwahi kuchafuka ata na chembe ya uchafu wa mti.
Lakini kwa kuwa walikua washazoeana mda mfupi tu, ASHURA alikubali kufundishwa hizo nyimbo na shikorobo bila kupoteza mda alianza kumfundisha.
Ilichukua mda mrefu kidogo ASHURA kuja kuelewa ule wimbo siku ile na alipoushika kabisa akafundishwa na wimbo wa kumuita SHIKOROBO chni ya maji kisha shikorobo akamwambia baada ya kuishika yote miwili
"Haya ngoja nione kama kweli utaweza kufanya hivyo" aliposema hayo mara alizama ndani ya maji kama kimbinga Ashura kabaki akicheka vituko vya Shikorobo.
Lakini akiwa katika hali ile alikuja kushtuka sekunde chache toka Shikorobioazame ndani ya maji.
Ghafla maji yakageuka kuwa machafu kupitiliza hali iliyompeleke mpaka yeye kunyanyuka...............ITAENDELEA......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: