EPISODE 3: MAPENZI YA JINI LA MAJI Mwandishi: Dominick Chuwa Whatsapp: 0787325447 ........ILIPOISHIA......... Ghafla maji yakageuka kuwa machafu kupitiliza hali iliyompelekea mpaka yeye kunyanyuka..............SASA ENDELEA....... Ile hali ilimshangaza Ashura kupita kiasi mapigo yake ya moyo yalienda mbio sana kuona maji meupe kubadilika kuwa kama chai ya maziwa. Kwakweli hapo ndipo alipoamini kwamba Shikorobo ni JINI kweli na pia sio mtu wa kawaida kuchezea. Ila Ashura kilichomshangaza hakuweza kumuogopa kabisa ata kama ni JINI ama kweli kila ndege hutua katika mti aupendao ata kama una miba na majani kibao vivyo hivyo iliku kwa Ashura nyota yake ilikua ya mbuyu kupendwa na majini bila kujua itakuja kumuhatarishia maisha hapo badae. Baada ya mda mfupi kupita aliacha ku panic akatulia nakuanza kukumbuka ule wimbo aliofundishwa mda mfupi uliopita. Haikuwa rahisi kwa kichwa panzi kushika ule wimbo kwa sababu ulikua mgumu na maneno yake yalikua kama kilugha. Alisafisha koo kwa kumeza fundo la mate kubwa kisha alianza kuimba "Marines sobre a agua!!, os deuses da agua!!! proteger a agua!!!dessa agua para que eu pudesse beber sempre" Baada ya kuimba wimbo huo alitulia kama sekunde tatu kwa maajabu mengine maji yalikua masafi kama hapo awali. Kwa Ashura iliku ni maajabu ya kwanza tangu azaliwe hakuwahi kuona mazingaombwe na maajabu kama yale. Lakini licha ya maji kuwa masafi Shikorobo hakutokeza. Ndipo alipokumbuka kwamba kuna wimbo kafundishwa wa kumuita. Hakuwa na namna nyingine aliimba ule wimbo mwingine wa kumuita Shikorobo. Hali ilikua kama awali ya kwenye maji baada ya sekunde chache Shikorobo aliibuka kwa kasi ya ajabu akirusha maji kama kambale. Ashura alibakia ana furaha na mshangao wa hali ya juu ila ilibidi akubaliane na hayo pia amuamini SHIKOROBO. Hivyo kuanzai siku hiyo walikua marafiki na pia mwishoni kila mmoja akamueleza mwenzake hisia zake maana Ashura alikua anaenda mwenyewe mtoni Kwa kisingizio kile cha kupigwa na kaka, kwa sababu ya Ashura kupendwa na JINI wanakijiji walianza kupata mda wa maji machafu na masafi ilipita mwezi ile hali wakaizoea lakini fumbo lilibaki kwa wazazi wa ASHURA mwanae alivyopenda mtoni mda wote na kubadilika tabia ghafla. ********** Baada ya Ashura kuweka ndoo ya maji chini nae alikaa kwenye kale ka ardhi miguu akiwa kaitumbukiza ndani ya maji. Kwa upande wa Shikorobo yeye bado alikua ndani ya maji akimtazama mpenzi wake kwa matamanio ya hali ya juu kwa sababu tangu waanze kuwa na uhusiano hawakuwahi ata kugusana midomo kwa ajili ya kuogopana na pia SHIKOROBO alimwambia Ashura hawezi lolote kwa ajili ya ule mkia wake. Kwa mapozi na macho ya mlegezo Ashura alivuta kinguo chake chini kisha aliendelea na maongezi. "Mhuuu! Nambie mpenzi wa mie, mbona leo umetokeza ata kabla sijakuita?" Alisema Ashura "Hapana ujue leo nina furaha sana yani, nikasema siwezi kukusubiri mpaka uniite na unaona ningesubiri ata usingeniita" alisema Shikorobo akionesha furaha yake ambayo hajawahi kuionesha kabla. Ashura alishangaa kumuona shikorobo ana hali ya furaha kiasi kile.Alimuuliza nini siri ya furaha yake ndipo shikorobo alipomfungukia kwamba amepata uwezo mwingine wakukibadilisha kuwa na miguu ya binadamu. Ashura alilipuka na bonge la furaha akatoka pale alipokua amekaa akataka kwenda kumkumbatia shikorobo lakini Mara Shikorovo alimnyooshea mikono kuonesha kwamba aache kitendo kile. "Usije kwanza sasa hivi bado sijaenda kujibadili" alisema shikorobo akimzuia ashura bado "Jamaniiiiiii! Ah mi staki, bac nenda kajibadilishe urudi fasta kuna kitu nataka kwako" Ashura alideka kwa manung'uniko aking'ata kidole. Yale maneno na ile staili ndio ikamfanya shikorobi kuona kama akijibadilisha mda ule bac atapata tunda kwa Ashura. Haraka haraka alimuaga ASHURA akitaka kuzama kwenye maji "Shikorobo ngoja nipeleke maji haya kwanza nikirudi ndio tuwe pamoja, kwa sababu nimekaa huku mtoni yapata nusu saa sasa" alisema Ashura baada ya kujua kwamba shikorobo akiwa katoka umbo la binadamu lazima kuna kitu kitatokea halafu mda utakua umeenda. SHIKOROBO hakukataa ila alimwambia ahadi yake ya kurudi mtoni afanye hatmraka maana akizama akiibuka atakua katika Umbo la kibinadamu. Kama ilivyo ada SHIKOROBO alizama kwenye maji na ASHURA alirudi nyumbani kupeleka tripu ile na pia arudi nyingine mda ule ule waje kufanya yao bila kujua kitakachoenda kutokea nyumbani. Alijitwika tena ndoo na safari ya kurudi nyumbani ikaanza akiwa anacheka njia nzima asipate picha akimkuta shikorobo yupo kama binadamu. ******* Akiwa njiani anarudi alifikia karibu na nyumba yao ambapo mbele yake chini ya mti aliwaona Kaka yake juma Baba yake pamoja na Rafiki wa kaka yake wakifundishanna kutumia mapanga kama wacheza sinema za kininja. Ashura aliigopa kidogo baaflda ya kugundua kuwa alienda mtoni mda mrefu sana na sijui kaka au baba yake atamuuliza alikua anafanya nini. Lakini kilichomuumiza Ashura kichwa ni kuwa yapata wiki sasa anaona mabadiliko ya familia yake kama kumtilia mashaka pamoja na kufanya mazoezi ya mapanga kama wanaenda kwenye vita. Ila hilo hakujali sana aliendelea kwenda na ndo yake kichwani mpaka alipowafikia akapita kwa kujikausha kama hajawaona, "We Ashura yani mda wote huo uliku mtoni unateka maji? Hayo maji yamekua matope mpaka uyachuje au?" Ni swali alilouliza baba yake wakiwa wameacha kucheza ule mchezo wa mapanga, ASHURA alikua ashawapita kama hatua tatu. Lakini Ashura hakujibu alionesha kiburi kwa sababau hata mawazo yake hayakuwa kwao bali yalikua kwa SHIKOROBO akikaza mwendo kwenda kumimina maji ili arudi fasta. "Baba mimi nilikwambia huyu mtoto wenu ana jeuri nyie mnabisha we huoni unamuiliza halafu hajibu?" Alidakia Juma kaka yake wakiwa wanamfata kule kule nyumbani anapoelekea. "Ashura! Ashura! Ashura!" Baba yake aliita kwa hasira mda huu ndipo Ashura aliposhtuka toka kwenye mawazo na kugeuka "Beee Baba" aliitika akiwa amefikia pipa la kumiminia maji "We nimekuita nda wote huo hukusikia ee" aliuliza baba yake kwa hasira zaidi "Sikusikia kweli baba" alijibu ASHURA mda ule ule Mama yake nae alitoka nje. Sasa ikawa ni familia nzima wanamuangalia huku kugombezwa ikaanza upya mana walivumilia kuona ASHURA kila siku anachelewa mtoni. "Mwanangu siku hizi umebadilika kila siku unaenda mtoni unachelewa kama umepata mchumba si useme ili tumjue kuliko kutuficha" alidakia mama yake ASHURA alikaa kimya kwa mda kisha akamimina maji. Hapo ndipo alipowaacha midomo wazi wazazi wake na kaka yake. Kwani walizoe kuona maji machafu ata siku za nyuma Ashura akileta maji huwa haleti masafi vile. Kiukweli walizidi kuingia shaka zaidi malumbano ya kumgombeza yakazidi mara mbili wakihoji kwamba inakuaje kaka mtu mwingine akienda mtoni anarudi na maji machafu akati yeye anatudi na maji masafi. Ashura hakuwa na la kujitetea zaidi ya kusema "Sa hivi maji yamekuwa masafi" tena kwa ufupi sana akitaka arudi tena mtoni kutimiza Ahadi yake. Wazazi wake hawakukubaliana na lile wasiamini mara moja, Sasa kwa bahati mbaya kaka yake Juma alipenda sifa kwa hiyo ili kuonesha kwamba nayeye anaweza kuleta maji masafi kwani yeye alizoea kuleta machafu alienda pale Ashura alipokua anamimina kisha akamwambia "Nigee hiyo ndoo niende mtoni nikachote maji zamu yangu" Ashura hakutegemea kitendo kama kile kuja kubadilishiwa kazi kwa sababu alimuacha SHIKIROBO kule anarudi duniani. Hapo mwanzo alikataa kumpa ili kumuokoa Kaka yake katika majanga maana anajua SHIKOROBO akimuona JUMA itakua ni mbaya maana anamchukia ile mbaya na alishamuahidi ASHURA kwamba siku akimkuta mtoni lazima atanfanyia kitu mbaya ata kama kaka yake, lakini mama yake alimkaripia kwa hasira kuu "Mpe ndoo kaka yako akachote maji? Wewe Osha vyombo haraka" maskini hakuwa na lingine na ahadi yake ikaishia pale pale akiashumu Shikorobo atakavyokuwa anamsubiri halafu atokeze Juma. Alimkabidhi ndoo, JUMA asijue huko mtoni kuna kipande cha mtu kinamsubiri dada yake halafu atokeze yeye anayechukiwa na JINI............ITAENDELEA.........

at 1:23 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top