Home → simulizi
→ EPISODE 1: MAPENZI YA JINI LA MAJI
Mwandishi: Dominick Chuwa
Whatsapp: 0787325447
NB:Hii simulizi ni kwa walioikosa tu. Haiuhusiani na simulizi zinazoendelea ndani ya PAGE hii iko full..
Upepo wa eneo lile la mto, kelele za kutiririka kwa maji pamoja na ndege waliolia kama kinanda au kinubi, ndio zilimvutia binti yule kukaa chini na kuanza kutafakari hali ya hewa ya pale ilivyokua nzuri kama yuko peponi. Haikuwa kawaida kwa msichana mwenye akili timamu kama yule kukaa chini katika mto mkubwa kama ule na pia msitu uliozunguka pale ulikua mnene wenye wanayama wa kutisha pamoja na mambo ya ajabu ajabu kama ilivyo misitu mingi iliyo mizito.
Lakini kwenye miti hapakosi wajenzi na pia usione vyaelea jua vimeundwa. Sina maana kubwa kusema maneno hayo ila ni binti yule ndio alinitatanisha kukaa vile.
Kwa jina yulr Msichana walimuita ASHURA mtoto wa kike pekee katika familia ya mzee NGWENE kati ya watoto wawili alionao mmoja wa kime mkubwa na yule Ashura.
Waliishia katika kijiji chenye uhaba wa maji kupita kiasi yani japo kilikua na mto mkubwa ila iliwapasa wanakijiji waamke asubuhi na mapema ili kweda kuchota maji.
Kilochowashangaza wanakiji wa eneo lile ni kwamba endapo ukiwahi asubuhi ndio unakuta maji yakiwa masafi kupitiliza lakini ulichelewa kidogo yani uende ata sa nne maji ya mto utakayokuta hayafai hata kwa kunywa mnyama.
Hali ile walifkisha mpaka kwenye uongozi wa kijiji lakini walibaki kuishia kuambiwa atakua ni jini kwa hiyo walihitajika kufanya matambiko.
Walifanya matambiko ya kila aina kuchinja, kumwaga na kutia sadaka katika ule mto lakini maji yalibaki kuwa na tabia ile ile asubuhi sana masafi mchna machafu. Kwa hiyo ilibidi kila mwanakijiji awe anaamka asubuhi na mapema kwenda kuchota maji japo kulitisha lakini hawakuwa na namna nyingine.
*******
ASHURA akiwa bado amekaa chini hakuna mwanakijiji hata mmoja aloyetokeza kuchota maji ilionesha ule mda wa maji kuwa masafi ushapitiliza lakini maajabu ni kuwa maji yalikuwa masafi tafikiri yaliwekwa 'water guard' na pia alionesha mwenye furaha kupita kiasi. Ashura hakuwa mbishi ni Mchapakazi kila alipoambiwa afanye kitu flani na wazazi wake.
Lakini tabia alkyokua nayo yule binti na pia ndio chanzo cha yote ni kuwa hakutaka kuoelewa wala kuwa na mahusiani yoyote na mwanaume wa aina yeyote pale kijijini hali iliyowaacha wazi wanakijiji walioleta posa ila walitolewa nje kwa makali na majivuno ya ASHURA.
"Sina mda mchafu wa kuolewa na mwanaume kama wewe, kwanza hujui ata kunyoa ndevu, itakuaje nikiishi na wewe nyumba moja, nitoleeni uchafu mbele yangu" ni maneno aliyotoa Ashura siku moja alipokuja kuposwa akamtukana huyo mvulana mbele ya wazai wake na wazazi wa yule kijana.
Kwa kuwa wazazi wake walikua wanampenda na ndio binti pekee walimwacha afanye chaguo lake japo hali ya sintofahamu iliwabaki kichwani kwanini ASHURA akatae kuoelewa na walikuja wanaume wa kila aina ila hawakuwa kitu kwa Ashura.
Baada ya kukaa chini mda mrefu na kuona kuwa inamtosha kwa siku ile kuvuta harufu nzuri ya majani na maji ya mto ule ASHURA aliamua kunyanyuka na kuchukua ndoo yake iliyokua pembeni nakuanza kwenda ndani ya maji ili kuchota maji.
Hakika binti yule alikua kaumbika haswa yani upande wa nyuma ndio ulimfanya mgongo wake kupinda na kuonesha umbo zuri la namba nane.Na hiyo ndio sababu iliyowafanya wavulana kumpigia misele ya kumuoa.
Akiwa amevaa kanguo cha kitego chenye kuonesha mchoro wa kufuli alilovaa sikujua labda ndio nguo ya kutumbukia kwenye maji au ni mitego.Ila alipoinga kwenye maji kale kanguo kalipoloana ndio ikaleta tafsiri nzuri ya umbo lake.
Sidhani kama kuna mwanaume aliyekamilika kama akimuona Ashura namna ile anaweza kumuacha ila yeye alijamini kupita kiasi.
Alitembea ndani ya maji mpaka alipofika katikati ya maji yanapotirirka ndio alishikilia ndoo yake vema nakuanza kukinga yale maji yaliyokua yakitiririka kina kirefu kidogo ila yeye hakuogopa.
Alopohakikisha ndo yake imejaa mpaka maji kumwagika alijianda vizuri ili kujitwikwa arudi nyumbani akaendele na kazi zake za siku hiyo.
"Leo ata simuiti naondoka kimya kimya maana nimechelewa sana nikimuita hapa na ninavyomjua atang'ang'ania nikae nae mpaka achoke" yalikua ni maneno aliyosema kimoyo moyo akimzungumzia mtu ambaye hakuonekana mara moja mda ule.
Alisema hayo akiwa anakaribia kufika kwenye ukingo wa mto. Mda wote alikua ni mtu wa furaha na tabasamu. Alipofika kwenye ukingo kabla hajatoka kuna maua fulani huwa anayependa kupita kiasi yani kabla hajatoka kwenye mto lazima ayashike ndio aondoke.
Aliyafikia maua yale akayashika kama kawaida yake aliporidhika nayo alinyanyua mguu wa kulia na kuupandisha nchi kavu ili atoke ndani ya maji.
Mguu wa kushoto ukiwa ndani ya maji bado ndio anajianda na huo kuutoa aondokea kabisa ghafla bila yeye kujua wala kugeuka Ulitokeza mkono wa binadamu kutoka chini ya maji nakuanza kueleke kama unataka kumshika ule mguu wa Ashura uliobaki ndani ya maji..............ITAENDELEA..........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: