Home → simulizi
→ EPISODE 5: MAPENZI YA JINI LA MAJI
Mwandishi: Dominick Chuwa
Whatsapp: 0787325447
........ILIPOISHIA.........
Alimtaza kwa hasira akakunja ngumi ndani ya maji na yeye akajianda kwenda nae sambaba mpaka amshike...............SASA ENDELEA.....
Haikuwa rahisi kwa juma kusimama katika hatari kama ile japo hakuangalia pembeni hata kidogo.
Alihisi nywele kusisimka wakati alikuaa kanyoa utadhani katoka Segerea ya Keko.
Kwa kuwa njia ile ilikua inaendana na mfereji wa mto ule ikamrahisishia Shikorobo kuogelea vizuri ndani ya maji kama samaki japk mpaka mkda ile alikua ana miguu.
Juma alivyoona yale maji yanacheza kwa fujo halafu ni pembeni yake alinunua pikipiki ya Boxer akaifungia miguuni mwake mwendo aliotoka nao ulikua ni wa spidi mia.
Tatizo la Juma ni kwamba alifata mkondo wa maji ikawa tabu tupu kila alipokimbia ndio kasi ya maji iliongezeka
Shida yake shikorobo alitaka amrukie juma kama nyani amrudishe kwenye maji kwa sababu kama unavyoelewa tatizo ka samaki hawawezi kuishi nchi kavu mda mrefu au mamba kupigana nchi kavu huwa hawana nguvu kama wanavyopigania ndani ya maji.
Vivyo hivyo ikawa kwa shikorobo kumtarget juma amvute ndani ya maji ila ile ndio ikasababisha Juma kuchezwa na machale na kuanza kuacha ile njia ya karibu na mto akaanz kukimbia kwa kupita ndani ya msitu mbali kabisa na mto.
Ama kweli siku hiyo alikua na bahati maana nahisi angekamatwa anagefanywa mboga haswa. Kitendo cha yeye kukinbia mbali na njia ya mto ndio ikawa usalama wake pia ikasbabisha shikorobo kuibuka tena kwa sababu aliyekua anamkimbiza ashakimbilia mbali.
Alivyoibuka ndio akaona kweli Juma anatoka mbio za kufa mtu ndoo ya maji aliyobeba ikimwagika na ukitegemea ilikua nusu nahisi nyumbani alifiksha robo
"Kistobe kweli jamaa, ningejua ningetokeza pale pale ili nimuite tupigane kavu kavu, shenzi nimemkosa hivi ngoja siku nyingine nitamshika tu" alisema maneno hayo shikorobo asijue kwamba liwezekano leo Lisingoje kesho kwa sababu hakuna anayejua kesho itakuaje ila maskini Shikorobo hakujua kwamba siku hiyk ndio raha, nuksi na kutoweka duniani kwake.
Hakuwa na njia nyingine alijua labda huwenda, Ashura hatokuja tena hivyo aliamua kurudi ndani ya maji katika falme yake ila roho yake haikuwa na amani kukosa penzi la Ashura pia kukosa kutokla kipondo kwa JUMA.
*******
Baada ya mbio ndefu na ndoo yake mkononi Juma alifika sehemu chini ya mti ikabidi apumzike akiwa anahema kama mbwa koko.
Alihisi kuponea chupuchupu ndani ya mdomo wa mamba isingekua hivyo angekua anaitwa majeruhi au marehemu.
"Leo kidume kizima nimetolewa puta na kajini cha maji, ila yule alikua ni mtu kabisa ndio maana sista akija huku harudi mapema sasa ngojea lazima hii inshu nikawambie wazee, atakuja kupotea mdogo wangu huyu kisa huyu shenzi" alisema maneno hayo Juma kwa hasira sana akikumbuka alivyokimbizwa ndio ikamfanya anyanyuke tena kuendelea na safari yake ya kurudi nyumbani
"Ata njia yenyewe hii sijui nimefikaje duh mbali na home sana," alizidi kuongea peke yake kama chizi akizidi kutembea.
******
Nyumbani hali ilikua mbaya kwa Ashura ambaye aliosha vyombo lakini baba na mama yake walingurumisha koo zao kwa kumsema.
Hakuwa na namna nyingine zaidi ya kukaa kimya japo wakati mwingine alihisi kuumia mpaka alitaka kuongea ya rohoni akashindwa.
Alijua lazima ipo siku watamuheshimu kwa ajili ya penzi la Shikorobo.
Mda ule ule Juma alionekana akija nyumbani na ndoo yake akiwa kachoka kama katoka umbali wa kilomita ishirini.
Walipomuona wazazi wake waliacha kumgkmbeza Ashura na kumsbiria Juma aje kutoa majibu kuhusu maji. Ashura nae moyo ulienda mbio akiatamani kujua nini kimetokea huko mtoni kwa sababu alihisi lazima kuna kitu sio bure kaka yake kuja vile.
Alifika nyjmbani Juma akendeea pipa la maji moja kwa moja bila kuongea lolote wala wazazi wake hawakumsemesha.
Kwa aibu alimimina yale maji kwenye pipa hapo ndipo wazazi wake tena Wakajikuta wanapigwa na butwa baada ya kuona maji aliyoleta juma ni machafu kupindukia ata zaidi ya siku zote.
Mama Juma alishindwa kuzuia nafsi yake akajikuta anaongea
"Haa! Juma mbona maji uliyoleta ni machafu hivyo?" Kabla Juma hajajibu lile alidakia tena baba yake
"Sasa ulitaka kwenda mtoni kutuchotea maji yaninj kama ni hivyo?, mbona Ashura katuletea masafi na menvi wewe umeleta robo?" Zile lawama zilimgeukia yeye sifa zake za kutaka kujiona kwamba nayeye anaweza kuleta maji masafi ikawa aibu. Ni kama wahenga qalivyosema mwisho wa ubaya ni Aibu.
"Naombeni mniache kwnza maana" alisema maneni yaliyowaacha njia panda wazazi wake akamfata Ashura pale aliko akamnyoshea ule mkono wenye ndoo kisha alimwambia
"Nenda kaendelee kuchota maji mimi nitaosha vyombo" lahaula alidiriki kuchukua Jukumu la kuosha vyombo mbele ya wazazi wake hali iliyowacha mmmidomo wazi wote.
Lakini juma hakuwa mjinga kumwambia Ashura kwamba akachote maji yeye aoshe vyombo lazima kuna jambo.......
Ashura hakugundua chochote zadi ya kutoa tabasamu akajisemea kimoyomoyo
"Nyoo huko alikotoka kakomeshwa anadiriki kuosha vyombo leo mxiiiiii" aliposema hayo alinyanyuka akakwapua ndoo kisha akaanza kuondoka ata bila kuaga.
Kitendo cha Ashura kuwaekea mgongo ikampa Juma nafasi ya kunyanyuka pale kwenye kiti alipotaka kuosha vyombo akawafata baba na mama yake kwa kasi ya ajabu alipowafikia akawanong'oneza
"Baba, mamma twendeni tumfate mkaone wenyewe" wazazi wake hawakumuelewa mapema ikabidi waduwae kwanza.
Juma aliwashika mikono wote wawili wakaaanza kumfatilia kwa nyuma nyuma Ashura bila kujua na wala wazazi wake bado waliikua wana fumbo kwanini Juma anataka wamfate Ashura.....ITAENDELEA.........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: