EPISODE 6: MAPENZI YA JINI LA MAJI Mwandishi: Dominick Chuwa Whatsapp: 0787325447 ........ILIPOISHIA......... Juma aliwashika mikono wote wawili wakaaanza kumfatilia kwa nyuma nyuma Ashura bila kujua na wala wazazi wake bado waliikua wana fumbo kwanini Juma anataka wamfate Ashura.........SASA ENDELEA.... Siku za mwizi ni arobaini na nahisi za Ashura zilikua zishatimia. Alitoka pale nyumbani kwao mpaka njiani alikua anacheka njia nzima kwa ajili ya kwenda kukutana tena mpenzi wake SHIKOROBO akiwa katika umbo la kibinadamu. Alijihisi ni kama malkia ndani ya kijiji kile kwa mapenzi yale. Kuna mda alitanua mikono kama ana paa akifikiria angekuwa na uwezo huo angepaa afike mtoni haraka na kupata kile alichotaka. Asingekuwa yeye ni msichana au angekuwa na mbio angetoka mbio ili amuwahi SHIKOROBO Wake. Alifika eneo lenye maua yale yaliyofanana na nywele za Shikorobo kuashiria kwamba yupo karibu na mto. Kama ilivyo kawaida yake aliyaendea yale maua na kuyashika kama anapapasa. Mwili wake ulisisimka akihisi kile ndio kama kichwa cha Shikorobo. Am kweli mapenzi ni raha umpate anayekupa raha sio kila siku karaha. Lakini akiwa hajui hili wala lile kwa nyuma familia yake ilimfaliia akiwemo kiongozi Juma, pia mda huu aliongezeka yule rafikia yake juma akiwa kashika panga, ata wazazi wake waliokota vipande vya mti wakashika mkononi wakihisi labda wanaenda kumfumania mtu wa kawaida ili wakimkuta wamdondoshee kipondo cha haja, wao bado walikua kwenye Fungate ni Juma peke yake alijua huko mtoni kuna Jini kwa kuhisi ila hakupata uhakika ndio anaenda kuhalikisha Ashura kila alipopiga batua tatu wao walipiga moja kwa kunyata sana kuna wakati waligusa majani Ashura akasikia aligeuka lakini waliwahi kujificha ile ikamfanya Ashura ahisi kwamba huwenda ni kitu cha kawaida. Safari ilifikia mtoni, Maji ya mtoni mida ile halikua machafu kupitiliza. Alifika Ashura enek lile akaa pembeni kwa kuweka ndoo chini. Lile kundi walilokuwa Linamfatilia nalo lilijibanza pambeni ya kichaka cha karibu wakimuangalia kwa makini Ashura atafanya nini. Ashura alitazama eneo lile kwa makini kuangalia kama kuna kiumbe chochote kinamuona baada ya kuhakikisha usalama alisuunza koo lake kisha alianza kuimba ule wimbo wa kusafisha maji. Kwa jinsi alivyouimba nako kule waliusikia na Juma alivyoakuwa mjanja alishika ule wimbo tena mwanzo mpaka mwisho yani kichwa chake kilikua chepesi kuliko cha Ashura alkyefundisbwa mda mrefu. Baada ya ule wimbo kuimbwa ilipita sekunde kadhaa maji yakawa masafi kupitilixa ile hali iliwafanya mama, baba, na rafiki wa Juma kukaa chini kwa uwoga na mshangao tangu wazaliwe hawakuwahi kuona kitu kama kile. Juma alizidi kuwaambia watulie maana ile ni kama Treila sasa Muvi kamilia ndio inaaza, walitulia tena kuangalia kinachofata ni nini. Baada ya maji kuwa masafi Ashura haraka haraka aliuimba tena ule wimbo wa kumuita Shikiorobo kwa madaha na nyodo kwa sauti ya kumtoa nyoka pangono asijue kwamba pembeni kuna mtu ana rekodi yale maneno anayoimba. Kama ilivyokua hapo awali siku zote baada ya mda mfupi maji yalianza kupumua yani namaanisha kulia kama kisima fulani kisha nywele zenye rangi ya zamabarau, nyeusi, na brown zilianza kuonekana zikija juu taratibu. AShura alipoona vile alianza kuingia kwenye maji taratibu kitendo cha kutumbukiza miguu yake ndani ya maji SHIKOROBO aliibuka kama mzuka huku akitanua mikono yake kama anamuita Ashura amkumbatie... ***** Mama Ashura alijikuta anaishiwa Nguvu za miguu na kulegea mpaka kukaa chini macho yake yalikataa kuona lile tukio mtoti wake kumbe kweli ana mahusiano na jini. Hali ilkawa vile vile kwa Baba yake walipomuona SHIKIROBO ametokeza ndani ya maji na kumbe ndio Ashura anayemfataga mtoni kila siku, alijihisi kuchanganyikiwa maana washachelewa kumnasua mtoto wao. "Mmeona eee, sasa hii ndio tofauti yetu ya mimi kuleta machafu na yeye masafi ona mtoto qenu leo anamahusiano na Jini la maji Kakataa wanaume wote kisa yule" aliongea kwa kunong'ona Juma akiwageukia wazazi wake ambao walikua washa panic. Kwa hasira na jazba Baba Ashura alitaka kunyanyuka pale aliko akachuku panga la rafiki yake Juma ili atokeze kwenda kumkata Shikirobo mbele ya mtoto wake. Ilibidi Juma na rafiki yake wachukue Jukumu la kumzuia kwa sababu walijua vema yule Jini hawezi kufa kirahisi na silaha. Na ni bora wangeenda pale pale alipo na Ashura kwa sababu alikua ashakuwa binadamu ila uzembe walioufanya ndio ule kutokwenda "Baba kumbuka yule ni Jini huwezi kwenda kimpiga, bali ni kwenda kupitia kwa mganga NDUMBA atupe dawa ya kulilegeza, niulize mimi niliyetoka kukimbizwa kwa hiyo punguza hasira tufikirie namna ya kufanya" Alizidi kusisitiza Juma akimshiklia chini mzee wake aliyefura kwa hasira. Yale maneno ya Juma yalimuingia Mama yake ndipo alipopata nguvu ya kunyanyuka huku akisema. "Twendeni tukachukue dawa haraka tuje kupambana hii vita ya majini sasa leo nataka nimalize mizizi yote ya majini kwa sababu huyu jini hanifahamu kwamba mimi ni NAMIKELE binti wa MBULISITA" wakatia anasema maneno hayo kwa ujasiri kuonesha kwamba yeye ni mtaalamu wa kupambana na Majini alikua ashanyanyuka nakuanza kuongoza kurudi nyumbani kuchukua dawa na kwa jinsi walivyokuwa wajinga wakaondoka wote kurudi nyumbani hakuachwa ata mtu mmoja kuangalia sinema ya bure dhidi ya ASHURA na SHIKOROBO.. **** Shikorobo alipotanua mikono, Ashura alijikuta anakimbia mbio na kumrukia mpaka kifuani kwake. Hata siku moja hakuwahi hata kukumbatiana kwa hiyo kile kitendo cha kugusana hasi na chanya machungwa ya Ashura yakipogusa kifua cha Shikorboo wakijikuta wote wanasisimka mwili mzima kwa mapenzi ata kabla mtu hajamuongelesha mwenzake walirukiana midomoninakuanza kuena mate huku wakipapasana kwa mahaba mazito..............ITENDELEA... IPATE FULL WHATSAPP IKIWA NA PICHA ZAKE KWA SHILINGI 1000 nitafute kupitia 0787325447 upate utaratibu wa kulipia

at 1:23 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top