EPISODE 15:MAPENZI YA JINI LA MAJI Mwandishi: Dominick chuwa Whatsapp: 0787325447 ILIPOISHIA...... nyumba tena zaidi nikuwa ngazi zilionekana na ndani ya miamba ile mikubwa ilionekana kumechongwa madirisha mwanga wa taaa ukionekana...SASA ENDELEA.... Na taa zile hazikua za tochi useme labda haziwezi loana bali ilikua ni mienge ya moto yenye kumulika vizuri kitendo ambacho kilizidusha mshangao wa Ashura kwa sababu hakuwahi kufikiria haya siku moja kwamba moto unawaka chinj ya maji. Ingelikuwa dunia kuna moto wa aina ile, ungelikuta watu wanachoma samami chini ya bahari japo ule moto ulionesha kama haunguzi. Waliendelea kuogelea mpaka kufika eneo lenye ngazi au lango kuu sehemu ile maji yakawa mepesi akawa anaweza kushuka kwa chini na kutembea kwenye ngazi ila yule samaki bado aliendelea kuongoza kwa kuogelewa Walifika katika eneo walikojipanga samaki wagu wengi kupitiliza mfano wako kwenye maandamano wote wakimuangalia yeye, huwezi amini mpaka kufika mda ule hakujua nini kinamtokea kaletwa aliwe au kufanyiwa ukatili kwa sababu kama ni samaki watu pale ndio lilikua chimbuko lao Kila alipotembea wale samaki watu walimuangalia kwa furaha huku wengine wakipiga vigelegele vya chinichini wakifurahi uwepo wake. Walipita katika ule msururu wa samaki kisha wakafika sehemu ambayo ngazi zilipanda juu kamakwamba ni jukwaa la juu kwani kila mmoja aliangalia upande ule. Walisimama kwa mda wa sekunde chache ghafla alitokea mwanaume wa makamo, mwenye nywele za udhuhuri, kajaza kidogo, miaka alionesha kati ya hamsini mpaka sitini. Wale samaki watu walipomuona waliinamisha vichwa kuonesha ishara ya heshima kisha yule aliyeongozana na Ashura alifungua mdomo "Nimefanya kama ulivyoniagiza mfalme mtukufu" kikuweli bado yalikua ni mambo mapya kabisa kwa Ashura kumbe walikua wana uwezo wakuongea hadi chinu ya maji hakika yalikua ni maajabu zaidi kwake "Safi sana, ndio maana nilikutuma Kwa maana nilijua huwezi niangusha katika kazi yako, hakika leo itakua ni furaha kubwa" akimgeukia Ashura ambaye bado alikua anamshangaaa "Karibu katika Falme ya Samaki, binti ASHURA, wewe ndio utakayeweza kuifanya falme hii iwe na furaha ya milele" kwa Ashura bado ilikua ni fubgate kuona mzee kama yule anamjua jina, tena yeye hakufanana na wengine kwamba wana mkia wa samaki bali, alikua na miguu kama ya binadamu. Yule mzee au kiongozi wa ile falme alimuarisha yule aliyemleta Ashura aende akamvalishe nguo nzuri za harusi. Kiukweli aliona bado yuko kwenye ndoto, hado kufikia kuvishwa nguo za Harusi wakati baba harusi hajamuona ilianza kumtisha kiasi. Alifika kwenye chumba cha mapambio, au saluni ya majini ya maji, akakalishwa chini nakuanza kuvalishwa na kupambwa "Mbona, mnanipamba kama bibi harusi kuna nini humu mbona sielewi" alishindwa kuzuia nafsi yake ilibidi aulize. Lakini wale nguva walitoa tabasamu wakimwabia ataona kinachotokea ila kapata bahati kubwa sana. Dakika chache kupita, Ashura alikua ashakamilika kwa kuvalishwa kasketi cheupe, ju alivalia sidiria nyeupe yenye rangi ya dhahabu, nywele zilpambwa na maua ya rangi za madini, kiuno chake kilirembbwa na shanga ya rangi ya dhahabu kuifanya azidi kupendeza zaidi Alivyotoka ndani ya chumba kile alikuta nderemo za vinananda na matarumbeta vinapigwa. Yule mfalme alipomuona alicheka kisha akapiga makofi na katika hali ya kushangza asiyotarajia Ashura hakuamini macho yake baaada ya kumuona SHIKOROBO akitokeza kwa pembeni juu ya lile jukwaa. Mikono ilimtetemeka, machozi yakimlenga, asiamini kama ipo siku damh za shikorobo kiasi kile atakuja kumkuta siku moja yuko Hai, tena hana ata kovu "Shikorobooooo" aliita kwa nguvu Ashura machozi ya furaha yakimtoka "Ndio mimi mpenzi wangu," aliitikia Shikorobo akiwa anashuka kwenye ngazi, na Ashura nae akawa anapanda wakipokutana kati wote walikumbatiania kwa mapenzi mazito, vigelegele na Na nderemo zilivurumishwa katika himaya ile. "Kumbe uko Hai, nililia sana kwa ajili yako. Shikorobo imekuaje mpaka uko hapa?" Ashura alisema kwa masikitjko akiwa anamshika shika baadhi ya viungo vya mwili wa Shikorobo "Nisingeliweza kufa kirahisi vile, kwanza sisi huwa tuna nafsi zaidi ya tatu ukiua moja inabaki mbili, wao waliua moja kwa hiyo iliyofata ndio ikanifanya niwe hivi, na pia mapanga ya duniani yanaweza kutukata na sio kutuua tena makovu yake hayawezi kukaa ata kwa masaa yanapotea. sisi tuna silaa zetu maalumu za kuliwa, ukiendelea kukaa huku utajua yote" alimulelezea jinsi alivyopigwa mpaka kuja kuchukuliwa, na wenzake. ASHURA alizidi kufurahi kuona tena anakumbatiana na SHIKOROBO Walimgeukia mfalme ambaye alikua bado anawaangalia wamalize yao kisha shikorobo alisema "Baba huyu ndio msichana niliyewaambia kutoka duniani" "Ndio, nimetimiza Furaha yako Mwanangu nahisi sintoumizwa tena kama nilivyoumizwa na mdogo wako ASHA" kumbe yule mfalme ni baba yake na ASHA aliyechukuliwa na KOKU Duniani, baada ya kusema vile walipanda mpaka kwa mfalme alipo kisha alichukua kamba fulani akashika mikonk ya ASHURA na SHIKOROBI kwa kuikutanisha, akaanza kuifunga huku akisema "KATIKA NDOA HII HAKUNA KIUMBE CHOCHOTE KITAKACHOTENGANISHA, NIMEMTEUA MWANANGU KAMA MFALME WA HIMAYA HII NA MKE WAKE ATAKAYEMUOA LEO HAPA ATAHESHIMIKA KAMA MALKIA," alimalizia kufunga kamba radi za ajabu na mingurumo ilipiga Samaki watu wengine waliiinamisha vichwa vyao chini kutoa heshima ya ndoa ile "SASA MSHAKUA MKE NA MUME WA KIHALALI" alisena baba yake SHIKOROBO na bila kupoteza mda walirukiana midomoni kwa furaha nakuanza kupata mate *** **** Mpaka walipokuja kufika nyumbani, Bado MAMA ASHURA alikua katika hali mbaya sana.walimlaza juu ya kitanda jitihada za kutafuta mitishamba ya kumtibu zikaanza. Sio juma Wala baba yake wote walichanganyikiwa kwa hali ile. Kwa utashi wa kujua mimea na dawa waliweza kumponya yule mama asife lakini hakuweza kuamka kitandani alikua ni mtu aliyeparalaizi. Wa kulishwa kuogesha ata kwenye haja hujisaidia hapo hapo hali iliyofanya familia ile waishi kwa shida sana. ******* ASHURA aliishi na Shikoribo asiwe anajua Mama yake mzazi anaishi Duniani kwa matatizo, hatoki kitandani kwa ajili yake. Waliisha kwa furaha wakapata mtoto wa kike nae ASHURA alivyozidi kukaa nae akawa na mkia wa samaki akafanana na samaki walioishi chini ya maji. Lakini siku zote mkataa kwao ni mtumwa, aka ahidi ipo siku atarudi Duniani kumsalimia MAMA yake na familia kwa ujumla *****MWISHO****** FUNZO: Katika maisha mtegemee sana mungu wako kwa maana yeye ndio kila kitu kwako. ila ukimtegemea mwanadamu atakuzidishia matatizo tu kama waliyoyapata wazazi wa Ashura kwa kumtegemea mganga NDUMBA wakizani ndio atakua suluhisho ya matatizo yao PILI: Ukipenda mtu mpende kwa upendo wote ambaye ata ikitokea misukosuko ya aina yoyote huwezi mwacha yani uwe na uvumilivu kama ASHURA. TATU: Ukimpenda mtu jaribu kumwambia ukweli na kisha pambana kutetea Penzi lako kama SHIKOROBO NNE: usiwe kichochezi cha kuvunja mapenzi ya watu kisa vitu vidogo na pia usiwe mtu mtaka sifa na vyeo kama JUMA.(JAPO HATUFUNDISHI KUPENDA MAJINI) SHUKRANI: Ziende kwa watu wote waliokua na mimi toka mwanzo mpaka mwishi wa story hii.

at 1:23 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top