EPISODE 14:MAPENZI YA JINI LA MAJI Mwandishi: Dominick chuwa Whatsapp: 0787325447 ILIPOISHIA...... Wakiwa wanashangaa midomo yote wazi mara yale maji yakaanza kunyanyuka juu kwenda hewani halafu yakawa yanakuja Pole pole ule upande waliokua wakina Juma na wazazi wake kwa muundo wa mviringo.......SASA ENDELEA.... Yalikua ni maajabu ya kwanza kuona Juma na baba yake ijapokuwa kike kitendo cha maji kuwafata hakikumtingisha nywele waka ugoko Mama ASHURA. Vuguvugu la maji yale yalianza kuleta fukuto la joto sehemu ile, majasho yakaanza kutoka kwenye vinyweleo mfano wa bomba iloyong'olewa koki Kwa taratibu wakaanza kurudi nyuma kila mviringo wa maji uliposogea.Hatua zao za kurudi nyuma alifanya Baba na mtoto ila mama hakutaka kurudi nyuma matokeo yake alisimama nakuanza kunyoosha mikoni juu kama anajisalimisha, maneno ya kutisha na yasioleweka yalimtoka kinywani mwake mfululizo "Mama, tukimbieeee " juma alimuita wakiwa wao wamefika mbali mama yao maji yalimkarbia, "Mama Ashura huwezi pambana nayo" alihimiza baba Ashurra ijapokuwa kelel zile hazikumfanya hata mama ashura kurudi nyuma zaidi ya kupambana na nguvu zile za maji Mama yule aliita majini na kutumia ushirikina wake wote jiasi kwamba mbingu zikaanza kuvurumisha mawingu mazito na yenye dalili ya kunyesha mvua kali. Maji yalimfikia hatua moja toka aliposimama joto likampanda nafikri, angepimwa na kipima joto ata ule mshale ungepitiliza namba zote. Alifanya kwa mbele mfano anasukuma ukuta uliokua tayari kwa kudondoshwa, maji yalitulia pale pale zikawa baina ya nguvu mbili moja ya jini nyingine ya kichawi zikipambana, Ilifka wakati mama Ashura alitaka kudondoka ikamfanya Juma kutaka kwenda kumkimbilia lakini aliona karudi katika hali yake ya kawaida. Zilipita sekunde mia moja maji yakifukuta karibu na mwili wa mama Ashura huku maneno ya kichawi yakiendekea kusemwa, gauni lililoa chapa chapa kwa jasho. Majani yaliyokua eneo lile yalianza kunyanyuliwa na makali ya upepo uliotokea upande wa nyuma kuelekea kule kwenye maji kama unaenda kupambana na maji. Vurumai la eneo lile lilibadilisha hali ikachafuka kukawa vumbi tupu hata wakina juma hawakuona tena mbele kunafanyika nini kwa ajili ya gkza la matakataka na vumbi mpaka pale upepo ulipotulia baada ya dakika nne, hali ikawa kawaida walipokuja kutazama mbele tena walikuta mtu aliyevalia gauni la bluu, kalala chini yale maji ya moto yasionekane tena kukawa wazi na kumekauka kama hakikuwa na maji, ijapokuwa hali ilikua shwari lakini kibanda cha mganga ndumba hakikuonekana Walikimbia kwa pamoja wote baada ya kukna Mama Ashura kalala chini, walifika pale aliko wakapiga magoti na kumgeuza kwa sababu alikua kalala kwa tumbo, la hasha walikuta mama yule kawa mweupee wa papai bovu au kuku aliyechemshwa, Hali ya Mama Ashura ilikua mbaya alikua ni mtu akichemshwa kwa mbele, juma alimshika mkono mmoja ulikua wamoto kidoho auachie kwa kuunguzwa, baba yake alimshika kichwani Bado alikua anaangalia na kuhema kwa shida kidogo damu zikimtoka puani, "Mama,!! Mke wanngu" waliita kwa pamoja wote. Wakimtingisha. Mama Ashura alinyanyua mdomo wake kwa ujasiri kama hakuea katika ugonjwa akacheka akisema "Nimewashinda nguvu" "Wakina nani hao? Aliuliza juma akizidi kumuangalia mamae "Majini ya maji yalitaka kututeketeza kama walivyomteketeza bwana NDUMBA, wamechukua kibanda chake na yeye pia kaenda kugeuzwa supu huko UJININI," alikohoa kidogo akaendelea " Tu.....tu..likosea Masharti, mganga alituambia tumwagie dawa kabla ya kumpiga ila tulijisahau tukampig kabla ya kufanya vile, ila...ila ila..." maneno yake yalikata kidogo kuonesha anapungukiwa na pumzi. Hawakuw na muda wa kumsikilixa tena kwa sababu hali yake ilizidi kuwa mbaya juma kwa Uchungu wa Mama yake alichuchumaa kisha alimuamuru baba yake ampandishe Mgongoni wamkimbize nyumbani kama watawahi kumpa dawa kwa sababu hakukuwa na zahanati wala hospitali ya karibu, kulikua ushirinikana na kijiji, kijiji na ushirikina zaidi ni miti ndio iigunduliwa kila kukicha hii ni dawa inatibu gonjwa fulani au inaua kitu fulani. Baada ya kuekewa mgongoni alismama kama punda aliekea gunia ka mchele huku mwenye mzigo alimchapa fimbo akimbie kwa zile mbio alizotoka nazo Juma hakuhisi kama yuki na mtu mgongoni kichwa chake kilivurugwa kuhusu kumponesha mama yake kabla hajafa * * * * Kitendo cha Ashura kurudi katika hali ya kawaida akiwa ndani ya maji Msichana Samaki aligeuka na kumpa ishara Ashura kuwa amfate. Hakusita kumfata kwa sababu yule ndio aliyemvuta na hajui anapelekwa wapi licha ya kugundua kwamba ni mtu mwema sio kama alivyofikiria. Hakuelewa mara moja kama kweli anakopelekwa kutakua Falme za shikorobo mawazo yake mda ule yalikua kumshangaa yule samaki anavyoegelea kwa umbo la kibinadamu. Kwenye njia ile ya maji walisindikizwa na samaki wadogo wadogo wa kawaida wakiwa katika kila rangi zaidi ya maua, Ashura alitamani kuwashika ila kila alipojaribu walikimbia huku aliyemtangulia akizidisha kasi ya kuogelea. Nyongo ya kilio cha Ashura ilidondokewa na robk ya furaha kuogolea chini ya maji na kuona viumbe vilivyojificha chini ya maji Tabasamau la likikuja kuachishwa kwa mshangao pale safari yao ya kuogelea kufika mbele ya mawe au miamba mikhbwa yalichongwa kama vichuguu vikubwa au ghorofa ndogo, ilichongwa kwa uhodari na ustadi mkubwa kuleta mandhari ya kuwa enel lile haliishi samaki bali ni viumbe wenye utashi kama bindamu kufanya mawe yaoneknae kama nyumba tena zaidi nikuwa ngazi zilionekana na ndani ya miamba ile mikubwa ilionekana kumechongwa madirisha mwanga wa taaa ukionekana..........ITAENDELEA....

at 1:23 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top