EPISODE 13:MAPENZI YA JINI LA MAJI Mwandishi: Dominick chuwa Whatsapp: 0787325447 ILIPOISHIA...... Ashura alizidi kupiga kele maana hakujua ni nini kinamvuta chini ya ardhi kwa kasi namna ile..........SASA ENDELEA...... Mpaka Juma na wazazi wake kufika katika dibwi lile, walikua washachelewa kwani mda ule Ashura alikua ashafika kimo cha maji kwenye kifua chake.ingelikuwa ni mfupi sana angelisha zama kwenye maji nakupotelea kabisa Alijihisi kuna mtu anamshika kwenye nyayo zake, mtu mwenyewe mikono ilikua milaini kupindukia kanakwamba hakuwahi kupata hata mionzi ya jua, lakini jambo lilomshangaza ni pale wazazi wake walipofika, Juma alimshkka kichwa, baba na mama yake walishika mikono ya pande zote mbili ambayo nayo ilifika kwenye kiungo cha msuli na pingili ya chini ya mkono, walipojaribu kumvuta juu huyo mtu aliyemvuta Ashura chini ilionesha ana nguvu kubwa kiliko zile za watu watatu. Juma alitumia maubavu yake yote, mzee yule nae alikumbuka ujana wake alipokua akipambana na ngedere kwa shambani kwake, na nguvu za nyongeza zilikua kwa yule mama lakini haikufanya Tembo kushituka kisa kuguswa na sisimizi. "Jamanii mwanangu anazama, uwiiiiii, majirani eeee" alilpiga kelele Mama Ashura moyo wake usiweze kuvumilia kuona binti yake ana zama maji "Mamaaaa niokoeni" alisaidiwa na kelele za ashura mda huu akianza kunywa maji ya kidimbwi kile. Kiukweli maji ni maji tu na yananguvu khliko lakini nguvu zake nahisi zinaonhezewa na baadhi ya viumbe. Mikono ya Ashura kwa bahati mbaya iliwaponyoka wazazi wake ilisababisha juma kubaki peke yake akiwa kashikilia fundo la nywele za Ashura kama katani zilizotoka kufuliwa. Kama tatu ilishindwa ikibaki moja isingeweza kamwe, zile nywele za ashura zilikatika juma akabaki kashikilia baadhi ya nywele za mwisho za Ashura kama kinyozi wa mkasi. Hakuwamini viini vya macho yao kuona Binti waliyempigania anaondoka kilaini wakiwa wanamuangalia. Kila mtu alihisi Kuchanganyikiwa. Mama Ashura alijikuta anatumbukiza mguu ndani ya kidimbwi kile cha maji amfate mtoto wake aliko, kama si ushapu wa Baba Ashura na juma kumuwahi angeenda kushuhudia kile kinachoenda kufanyika kwa mtoto yake chini ya maji. Akiwa ndani ya maji mazito yaliyosheheni usafi na samaki wa aina yake Ashura alishangaa ni mto gani au ziwa gani lililopita chini zaidi ya usawa wa bahari. Hakuwa mvuvi wala baharia useme anaweza kumiliki kuogelea chini ya kina kama kile, alijitahidi kutumia uwezo wake wa kuzaliwa nao kuzuia pumzi lakini alijikuta anameza robo lita kila alipofungua mdomo. Katika hali ya bumbuwazi alishangaa kuona samaki mkubwa samaki ambaye ni wa maaajabu kwani juu alifanana na kiwiliwili cha binadamu mwenye sura iliyochkngoka, macho rembu rembu mfano wa mlevi aliyelewa gongo pua na midomo yake kuumbe kjle hakika alifaa kuitwa nusu binadamu tena wa jinsia ya kike ambaye juu hakuvaa kitu Ashura alijikjjta anataka kuzimia baada ya kushtukia kumbe mtu yule kwa chini ana mkia wa samaki kama kibua. Ukichanganya kunywa maji na kuona msichana wa ajabu kama yule alijihisi kizunguzungu mbele akiona giza lakini kabla hajafika katika hatua ya kuzimia yule, binti niseme samaki mtu alimfata na kumshika kwenye midomo akampulizia pumzi ambayo ni kama uzima wa chini ya maji kwa sababu zile pumzi zilimfanya Ashura arudi katika hali ya kawaida, kwa kupumua kama yuko nchi kavu. * * * * Kupotea kwa Ashura chini ya maji ilianzisha kilio kipya kwa famili yake. Mama yake hakuwa anashikika hata kidogo kwa kelele za vilio. Baba yake mikono yake ilikua kama mzigo juu ya kichwa chake kila mara aliiweka na kuitoa. Juma peke yake ndio alikua na moyo wa ujasiri japo alikua anajukumu la kushika mama yake kila alipotaka kwenda kujirusha kwenye kile kimto "Mama wewe ndio umesababisha, unalia nini sasa dawa yako haijafanya kazi yoyote" alilaumu juma kilara chake kikitoka kijasho chembamba. "Kweli kabisa, mimi nilijua tu dawa ile haitafanya Lawama nyingi zilimdondokea Mama Ashura ambaye hakujibu lolote akijiona kweli yeye ndio ana makosa. "Haiwezekani NDUMBA anigee dawa feki, kwanini auliwe halafu arudi, lazima nikamlipizie kwa hkchi" ni maneno yenye jazna kubwa na hasira ndani yake akatoka pale njee kwa nia ya kurudi kwa mganga Ndumba ambaye ndio aliwapa dawa ya jini. Maneno yale alisikia Juma, pia na Baba yake wote kwa kuwa ni kitu kimona lawama zikaangukia kwa mganga aliyewapa dawa. Walimfata mama Ashura ambaye mida ile alikua ashafika kwenye njia ya kuelekea kwa mganga.Ama kweli mganga hajigangi licha ya Mama Ashura kutumia ushirikina wake lakini haikusaidia chochote. Mizozo ilindelea katikati ya safari kila mmoja akipewa lawama yake, lakini Wakati wanabishana hili na lile mara kwenye njia waliyokua wanatembea alitokea paka mweusi tii zaidi ya Oil chafu kiasi kwamba ni macho tu yalionekana. Walisimama kidogo yule paka alianza kulia kama mtoto mchanga, waliogopa sana walitaka kurudi ila Mama yake juma alisema msiogope mimi hawa nawaweza,kish alichukua udongo akamrushia yule paka huku akisema maneno flani yasiyoeleweka. Haikueleweka yule paka ni wa nani wa kutumwa au jini ila yale manenk yalimfanya akimbie kama yuko mbio za marathoni "Mhh! Hii ni dalili mbaya kwa mganga NDUMBA huyu paka ni wake imekuaje katoka?" Alisema mama Ashura wakiendela na safari, japo iliwashtua wote ila hawakua na jinisi Baada ya mwendo mfupi walifika karibu na maneo ya kibanda cha yule mganga . Katika hali ya kushangaza walipofika kwenye usawa wa kuona Kibanda hakukua tena kibanda wala majani. Kilikua ni kitendo cha kutisha sana, lile eneo la mganga kulitapakaa maji kama mto wa siku nyingi tena maji yake yalifuka mvuke mfano yanachemshwa, hawakuamini macho yao kama kumbe wamechokoza majini ya maji. Wakiwa wanashangaa midomo yote wazi mara yale maji yakaanza kunyanyuka juu kwenda hewani halafu yakawa yanakuja Pole pole ule upande waliokua wakina Juma na wazazi wake kwa muundo wa mviringo.........ITAENDELEA......

at 1:23 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top