EPISODE 11 & 12: MAPENZI YA JINI LA MAJI Mwandishi: Dominick Chuwa Whatsapp: 0787325447 ........ILIPOISHIA......... Wakati wakiwa mbali kabisa na mto mara ghafla walisikia mchakacho karibu vichaka vya pale tena huo mchakacho sio wa kawaida kwa sababu ile miti iliyowazunguka ilianza kutikisika matawi huku ardhi ikitetemeka, ata ule mbalamwezi waliokua wanautegema ulianza kufifia mwanga ................SASA ENDELEA........... Breki ya miguu yao ilitoa taarifa kupitia kwenye mishipa ya fahamu mpaka kwenye ubongo kwamba kuna hali ya hatari inapaswa kusimama, wote walisimama kama walikua katika mafunzo ya jeshi kana kwamba wakifika eneo lile wasimame. Kila mmoja nywele zilimsisimka wakihisi labda ndio mzimu wa Shikorobo unawafata mapema vile "Mama, hiyo ni nini mbona kuna hali nisiyojua" aliuliza Juma kwa uwoga akijutia kumpiga shikorobo kwa sababu, kama ni mzimu utakua umerudi yeye ndio angekua wakwanza kuuliwa. "Subirien kaeni kimya" alijibu mama yule ambaye bado hakutishwa na chochote kuhusu uchawi au majini. Alitangulia mbele akiwapita wale wa nyuma. Alivyopiga hatua moja mbele ghafla nyayo za mtu anakimbia zilisikika zikija upande ule lakini kama njia ya pembeni yake kwa sababu wao hawakufata njia walipia "shortcut" ili wawahi kufika. Kile kishindo kiawa kinazdii kusogea halafu ni kwa kasi sana na pia huyo mtu alionesha ana nguvu kwa sababu majani makavu ya ule msitu yalipiga kelele kila ilipokanyagwa na nyayo ya kiumbe anayekimbia Kwa kuwa Juma alianza kusikia uwoga mpaka kuaanza kutoa hewa kwa njia ya nyuma, mama yake ata kabla hajamgundua huyo mtu ghafla Juma alitoka mbele kwa mbio baada ya popo kutoka kwenye jiwe kubwa lillokia pale. Kile kitendo cha Juma kukimbia kwa uwoga na wale wengine walifuata kama unavyoelewa usiku muwe katika kundi na sehemu ya kutisha mmoja atoke mbio kama kaona kitu hakika kama ushawahi nahisi unajua nini kinatokea hapo. Ilikua ni mwendo Wa kukanyagana na kupigana vikumbo vya uwoga kama wako kweny mechi ya mpira. Hakuna aliyemkumbuka mwenzake kwamba kabaki nyuma wasijue kwamba anayekimbia upande ule wa pili alikua ni Ashura yeye akija mtoni **** Kilio cha Ashura kikisindikizwa na vigelegele vya majani makavu kila unyayo wake ulipokanyaga chini bado viliendelea kutawala katika njia ile ya kuelekea mtoni. Akili yake alihisi kama imechanganyikiwa asiamini kama kweli SHIKOROBO wake kauwawa.Hakusikia ata zile keleke za mparangano wa kina juma walivyokimbia upande wa pili masikio Yake yalikua mfano wa mtu kiziwi kwa sabsabu kuna mda popo na bundi walikua wanalia lakini yeye hakusikia na ni muoga kupindukia akisikia kelele za Bundi. Mwendo ulianza kupungua taratibu baada ya kuona anakaribia kufika mtoni. Aliyasogeza majani yaliyomzuia kupita mpaka alipofika mtoni macho yake yalikaza sehemu moja kama mtafunani wa mirungi. Kwenye kiwanja kadogo au fukwe ya mto ule, miguu yake ilianza kukosa nguvu za kutembea akawa anatembea matege na kama mtu anayesukumwa alipokuta maji yote yana uwekundu wa damu. Alipofika kabisa kwenye mto hapo ndipk ata yale matege ya miguu yake iliisha akajikuta anadkndoka chini kwa kupiga magoti mfano wa ndama aliyetoka kuzaliwa mda mfupi "Shii.....shi.....shi......shi......ko." alitaka kutaja jina la Mpenzi wake shikorobo lakini kwikwi na machozi kuingia ndani ya mdomo ndio ilikatisha neno lile akajikuta ana kigugumizi asichotegemea. Kiukweli kama ni mapenzi binti yule alikua kaoza akafa kabisa kwa penzi alilopewa. Alipeleka mkono wake kwenye mto akashika yale maji yenye damu zilizotapakaa kote. Alivyoshika mwili ulimsisimka kama vile kashika mwili wa mtu huyo. Kitu kilichomthibitishia kwamba yale maji ni damu za Shikorbo aliona rasta moja iliyokatika ikielea juu ya maji. Aliendelea kufanya doria ya macho kwenye mto ule huwenda akauona mwili wa SHIKOROBO lakini cha kushangaza hakukuwa na hata Ule nwili waliouacha wakina juma unaelea haukuwepi tena maeneo yale na haiwezekanu kuzama kwenye kina kirefu kama kile wakati mtu kafariki. Ashura hakujua keamba mwili uliachwa ndani ys mto fikimra zzake alikumbuka ike ndoto akaona kichaka alichoota ikabidi anyanyuke ili akatazame kwenye hicho kichaka kama atamuona kweli. ***** Ilichukua sekunde kama hamsini sehemu ya kuchuku dakika zaidi ya kumi wakina juma wali fika nyumbani wakiwa wanahema kama mbwa mwitu akiyotoka mawindoni. Yule rafiki yake juma hakuwa na haja ya kukaa tena pale kwa sababu, ni usiku na kuna karibia asubuhi ngoja aende kwake akiacha familia ile ikiwa ina mazungumzo yao. Sasa mbinde ikawa kwa wazazi wa juma namna ya kuingia ndani watamwanbiaje Ashura wakizani Ashura yuko ndani ya nyumba. Kibatari kilikua kinawaka bado lakini ule mlango wa nyumba hata haukufungwa.... .......ITAENDELEA...... EPISODE 12:MAPENZI YA JINI LA MAJI Mwandishi: Dominick Chuwa ............ILIPOISHIA.....Kibatari kilikua kinawaka bado lakini ule mlango wa nyumba hata haukufungwa.........SASA ENDELEA.... "Tumekimbiaaaa nikajua ni yule tu....." aliripoka juma kwa nguvu mama yake akamziba mdomo akimwambia. "Shiiipu Ashura atasikia" alinong'ona mama yake. Waliangia ndani kwa kunyata panga na kisu wakaenda kuweka kwenye karai moja wapo lilolokua ndani. Mama yake ndio alikua wa kwanza kwenda kuchungulia kama Ashura kalala lakini hali aliyokuta kitandani kwa Ashura ilimstisha kidogo, mashuka yako chini. Alirudi sebuleni akitumbua macho kama kapigwa na butwaa.Kibatari cha sebuleni kikiwa kimewashwa juma na baba yake walisubiri jibu. "Baba Ashura mtoto hayuko" alitamka mama yake kwa huruma "Unasemaje wewe?" Aliuliza mzee yule akiamka haraka kwenye kiti akamsukuama mama ashura nae akaenda kutazana kwenye chumba cha Ashura. "Haa huyu mtoto atakuwa kaenda wapi sasa, mbona anataka kutupa presha" aliuliza baba Ashura wasiijue kwamba wao ndio wamesababisha kuondoka kwake. "Baba, nishajua aliko ndio atakua yule aliyekua anakimbia kule njia ya mtoni tukazani ni jini, mimi ndio nahisi hivyo lazima atakua yeye" alitoa wazo juma wazo amablo lilikua ni la ukweli. "Anhaaa! Itakua kweli, huyu mtoto mpuuzi kweli sasa tunafanyaje na kajuaje kwamba tuko mtoni?' Aliuliza mama Ashura "Muache aende akakute maiti ya Laaana yake huko mtoni pumbavu, tusihangaike kurudi kumfuata, embu niletee chakula nile kwanza asubuhi inafika ata cjala" maneno ya mzee yule aliyaongea akirudi kwenye kiti akionesha hajatetereshwa na kitendo cha Ashura kwenda mtoni usiku wa manane. ****** Ashura alifika kwenye kile kichaka hakukuta hata tone la damu zikiwa pale. Alikata tamaa akijua fika ndio mwisho wake wa penzi lake na Shikorobo. Kwakweli usiku ule ulikua ni wa majonzi kwa binyi yule, huwezi amini mpaka jogoo wakwanza anawika Ashura alikua bado yuko mtoni. Baada ya kuona kwamba kunakaribia kukucha akajigundua yuko uchi hakuwa na budi kurudi nyumbani haraka kabla jua halijachomoza halafu akutwe uchi njiani. Alifika nyumbani kwa kujificha ficha kwenyee vichaka mbinde ikawa kuingia ndani ambapk mpaka mda ule alijua fika wazazi wake watakua ndani atapitaje akiwa uchi. Kwa bahati nzuri kwenye kamba ya kuanikia nguo kuliku na gagulo lake la kufanyia kazi za shamba alililifua akaona hilo hilo ndio litamsitiri aingie ndani kwanza. Aliliendea gagulo hilo akalivaa kwa maana lilikua ni mfumo wa dela kisha akafuta machozi nakuanza kuingia ndani. Alifika mpaka ndani ya nyumba kwenye sebule akakuta wote watatu wamepitiwa na usingizi wakalala katika mikao ya kila aina kwebye viti. Aliwataza kwa hasira walivuochafuka damu akajikuta machozi yanaanz tena upya ilibidi akimbili chumbani kwake akatulize maumivu ****** Ilikua asubuhi nyingine tena Ashura baada ya kuamka alichukua kitana chake na kwenda kenye kuka chini ajaribu kupotea mawazo ya kilio chake. Lakini Walipoamka tena wazazi pamona na juma walifufu tena lile jambo wakiaanza kuelezana jinsi walivyomuua Shikorobo. Pongezi nyingi zilimuendea juma baba yake akiwa kamshika mkono alizidi kumsifia. "Kijana wangu umenifurahisha sana kwa jinisi ulivyogundua tukio hili, hakika hakuna atayekushinda kwa ugunduzi, Na ili kuonesha furaha yangu mashamba yote nitakumilikisha wewe," alisema mzee yule akipiga piga bega la juma hata chai walikua hawajanywa kwao ilikua kama sikukuuu. "Baba mimi sikulenda kuona mdogo wangu anapotea ndio maana nikamfatilia sasa nisingewaambia si ungekuta kapotea katika mazingira ya kutatanisha" alisapoti Juma "Sawa kabisa mwanangu na yule Ashura lazima nitamuozesha kwa yule rafiki yako atake asitake" waliendelea kumsimanga na kumzoza Ashura. Mama yake alipomuona Ashura kakaa mbali na wao kwa jinisi alivyokua na sifa aliingia ndani na kuchukua lile karai lenye silaa zilizotapakaa damu za Shikorobo akaanza kumfata pale alipokaa. Ashura alijaribu kuchana nywele lakini nafsi yake haikumsahau kabisa Shikorobo yeye akawa ni wa kulia tu mkono mmoja akiuegemezea kwenye kiti. Alishtuka anaguswa kwenye bega alipogeuka akakuta ni mama yake kisha yule mama akalibwaga lile Karai chini akaanza kumpa madongo Ashura. "Hee yani unalia kisa yule rasta wako, ndio hivyo mama tushaamuulia mbali ulishindwa kumwambia kwamba mama yako ni mkuu wa kupambana na majini, ila wewe mwanagua huna akili mpaka ukaenda kupenda jini una wazimu eee, onaa sasa......" aliendea kuongea akachukua panga lile kubwa Kisha akaendela "Hili ndio lilimgawanisha vipande yule mpuuzi wako tulisahau kuleta nyama ya mchuzi nyumbani, we lia ata mwaka mzima lakini ndio hvyo tushamuaa,haloo oooooooo" alimaliza mama yule akageuka kurudi akakitonessha kidonda cha ASHURA upya. Alitazama lile panga kwa jinsi lilivyo kweli Shikorobo asingeweza kupona hata kidogo. Aliweka mkono wake kwenye kichwa kilio kikaendelea lakini wakati analia ile miguu yake aliiweka katika kidimbwi kamoja kilichotokana na Maji ya mvua iliyonyesha siku za karibuni. Ashura akiwa haelewi hili wala lile mama yake ata hajafika mbali alivyokuwa analia machozi yake yalidondokea kwenye kile kidimbwi ambacho hakikua kikubwa kwenda chini ni ata robo ya miguu yake haikuzana. Ghafla katoka hali isiyitarajiwa alishtukia anavutwa ndani ya kile kidmbwi na kitu kama sumaku kueleke chini. Alipiga kelele ya msaada maana hakutegema kidimbwi kana kile kumzamisha kama yuko kwenye mto. Zile kelele walizisikia mma yake ambaye alikua hajafika mbali, juma na baba yake walipogeuka kuangalia ule upande wa kelele la hasha mambo yalikua yashakua mambo kwani Ashura mda ule alikua ashafika kwenye kiuono kwenye kale kadimbwa akizama chini. Wote walimkimbialia ili wakamuokoe asizame wakishangaa ni aina gani ya kidimbwi kilichoyokua pale kama kisima wakati kilikua kidogo kama urefu wa beseni. Ashura alizidi kupiga kelele maana hakujua ni nini kinamvuta chini ya ardhi kwa kasi namna ile .........ITAENDELEA......

at 1:23 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top