EPISODE 9: MAPENZI YA JINI LA MAJI Mwandishi: Dominick Chuwa Whatsapp: 0787325447 ........ILIPOISHIA......... Shikorobo alishtuka kusikia sauti ile aliibuka tena kwa mara nyingine akageuka ile sauti inapotoke ndipo alipokutana na sura tatu za kazi kama wanajeshi na silaha za kutisba wakimfata yeye yani inaitwa tatu kwenye moja........SASA ENDELEA........ Mbio za kina juma zilikua zinatwamishwa na wingi ule wa maji walijikuta miguu inakua mizito. Alijiaandaa vizuri kwa mapambano Shikorobi nguvu azikivuta maana pale aliona bila kutoa kipondo watamzoe vibaya na kwa jinsi walivyoku wajinga wakajileta wanaume tupu, alimjua mmoja kwenye kyndi lile ambaye ni juma Hasira zake zikaongezeka maradufu Mbio zao zilikuja kukwama pale walipokuwa karibu karibu, jicho kwa jicho, wakinyoosha mapanga kama wacheza kareti wa kichina. "Wewe ndio unataka kumpkteza mwanangu" alisema mzee yule ambaye ni baba yake juma. "Leo lazima tukuonyeshe kazi,, twendeeeeeeniiii" alidakia Juma akiamrisha wenzake waende. Mzee wake ndio alikua wakwanza kupeleka mti aliobeba kumpiga nao shikorobo. Lakini ghafla shikorobo aliinama na kuzama kwenye maji. Wakiwa wameshika silaha walibaki kuduwaa kwa mtu kama yule azame ndani ya maji fasta kiasi kile ni kitendo cha ajabu sana. Wakiwa wanashauriana juma akiwa nyuma kabisa yeye ndio alionekana muoga, katika hali wasiyotarajia maji yalinyanyuliwa kwa kasi ya ajabu sehemu ile waliko pala pale akaibuka shikorobo tena kwa mara nyingine akiwa katika umbo la mkia wa samaki. Walishtuka sana kumuona vile kwa sabaabu mara ya kwanza walimuona na miguu, kitendo cha wae kushangaa kikampa nafasi shikorobo alipiga mkia wake ndani ya maji kama Dolphin, aliponyanyuka alitumia ubapa wa samaki kumpiga nao yule mzee baba yake juma uliofanya mzee yule adondokee kwenye maji kama kifurushi cha mihogo. Yule rafiki yake juma nae alijitokeza na panga lake lenye makali kwenye kumchoma shikorobo lakini la hasha walichokoza nyuki ambaye alikua analinda mzinga, kwani hata lile panga Kabla hajalifkisha karibu na mwili wa Shikorobo alishtukia chini ya miguu yake ndani ya maji ikipigwa mtama na kitu chenye kama miba na mitelezo ikionesha kwamba mkia wa shikorobl ulikua mrefu sana. Juma ndio akibakia akitetemeka kwa sababu alibaki yeye tu ambaye hajapokea yale mangumi ya fasta fasta kwa kutumia mkia. Kwa kua bado wale walikua chini ya maji na mama yake mda ule alikua ashasogea karibu kwenye tukio kibuyu chake kikiwa mkono wa kushoto akivizia. Juma alitoka kwa nia ya kwenda kuwaokoa baba na rafiki yake wasiendelee kipigwa au kuzama maji. Wakati anaenda kwa mashaka nae aklpigwa ngumi ya uso iliyomfanya aanze kuona nyota na maruerue ya kila rangi mbele yake. Kiukweli Shikorobo alikua hashikiki ata kidogo kwa hali ile, wale watu wa watatu walijikuta chini wakitoka kavu hata kurusha ngumi, wakiwa wanagala gala chini ya maji, Mama ashura akachukua nafasi ile kwa ajili afanye mambo yake. Juma ndio alikua wakwanza kuamka tena mama yake akisonga mbele. Juma Alimshika baba yake tena kumtoa pale kwa tahadhali zaidi mda huu. Alimsogeza pembeni ya fukwe kabisa akarudi tena kumchukua yule rafiki yake. Mama yake kibuyu kikiwa nyuma baada ya kuona njia ya kawaida imeshindikana alisonga mbele aliposimama shikorobo akiwa na nia yake ni kumpulizia ile dawa aliyopewa na mganga. Kwa imani ya kishirikina alijua vema lazima watashinda vita e hata kama walikosea masharti. Shikrobo alipomuona mama yule anamfata alituliza makali yake ya hasira moyo wake ukazizima kumuona mwanamke, sio kwamba alimpenda la hasha. Sifa ya Shikorobo huwa aana huruma sana na wanawake na pia hapendwi wapigwe ndio maana akatulia kuona amekuja kufanya nini wakati kaona wanaume walivyopigwa. Ila hakujali sana alimtazama tu aaangalie anafanya nini. "Kijana, umekosea kuwa na mahusiano na binti yangu sasa leo nataka nikuoneshe mimi ni nani" ni maneno ya mama Ashura akimimina dawa ya unga katika kiganja chake kwa nyuma nyuma ambapo Shikorobo maskini hakutambua lile akabaki njia landa yule mama anaongeaje maneno ya kijasiri namna e wakati hajabeba hata silaha. Baada ya Mama yule kumimina kiasi cha unga kwenye kiganja cha kulia, aliuleta mkono ule wenye dawa Mbele ya mdomo wake akiwa kaufunua unga wenye rangi ya manjani na kijiivu ukiwa umetanda. Shikorobo bila kuelewa kile ni nini maana hakuwahi kuona ushirikina yule mama aliupuliza ule unga kuelekea katika uso wa Shikorobo akiambatanisha na maneno ambayo hayakueleweka mara moja "NIPU SHUGARASI BAHIMU" alipotamka maneno hayo ule nga ukiwa hewani uligeuka moshi mzito na kufika katika uso wa shikorobo fasta. Shikorobo alipoona vile ndio akagundua kwamba ile ni dawa lakini alikua ashachelewa kwani ule moshi japo alikazana kuzuia na mikono lakini uliingia machoni, puani,na sehemu zote za matundu kwenye uso wake haikupita hata sekunde hali yake ikaanza kubadlika akijihisi joto lingi, kizunguzungu huku nguvu alizokua nazo zikaana kumuisha. Alijitahidi kushindana na hali ile lakini kwakweli Mama Ashura alikua ana uwezo mkubwa katika ushirikina kwa sababu pale pale Kidume cha majini, mwaamba wa majini ya maji alianza kwenda chini taratibu ndani ya maji. "Njoeeeeeni, ashalegeaaaaaaaa, harakaaaa" alipiga kelele mama Ashura akiwaita wakina Juma waliokua nje ya mto wanapeana huduma ya kwanza. Ile sauti iliwapenyeza ndani ya masikio yao hata yale maumivu hawakusikia tena baada ya kuangalia kule ndani ya mto kuona shikorobo anayumba yumba kama mlevi. Juma alichukua lile panga mda huu ndio akawa wa kwanza kunyanyuka sehemu ile akaingua ndani ya mto mpaka alipomfikia Shikorobo bado alikua kalegea sasa ikawa ni kama mpira wa mazoezi kwa juma Alimpiga panga la kwanza Shikorobo hakujbu shambulizi zaidi ya kutoa mngurumo mkubwa na upepo mkali ukavuma kiasi kwamba mto ukachafuka. ****** Ashura alipofika nyumbani alikuta nyumba imetulia hakuna hata kuku aliyekua njee kwani giza lilikua lishaingia. Alienda kumimina maji Akijihami sana kwa jinsi wazazi wake watakavyomsema. Alipomaliza kumimina akaingia ndani ambapo hakuamini kama hatokuta mtu ata wazazi wake waliozoea kulala mapema. Lakini kwa kuaa alikua kachoka hakujiuliza mara mbili kwamba wameenda wapi kweli siku ya kufa nyani miti yote humteleza. Kutokana na uchovu aliokua nao kwa kupewa penzi zito na shikorobo alienda chumbani kwake moja kwa moja akawasha koroboi lake lillokua na utambi mkubwa kama muuza samaki usiku kisha baada ya mwanga kuenea ndani ya chumba chake alivua nguo zake zote akijutupa kitandani na kujifunika na shuka. Akiwa anawaza hili na like ulivuma upepo mkali mule ndani ambao aliufananisha na ule wa shikorbo wa mtoni maskini bila ata kufikri kwamba mpenzi wake atakua kwenye matatizo ule upepo ndio ukamfanya apitiwe na usingizi mzito uliomfanya aanze kuota ndoto ya ajabu ya kutisha.. ****** Ule upepo na mngurumo wa shikorobo haukumtishi juma kusitisha zoezi lile tena Juma kwa hasira alizidi kumkata shikorobo kwenye mwili wake kama samaki anayetolewa utumbo, na wale wa nje hasa baba yake nae alikuja amebdba jiwe kubwa mfano wa tofali kwa hasira ya shikorobi alimtupia jiwe la kichwa kilichofanya kichwa cha shikorobo kipasuke kama tikitiki na damu zikaanza kuenea ndani ya mto ule. Wote watatu wakawa wanapiga na kukakata kila sehemu waliyoiona inafaa kukata, ubapa wake ndio ulifanywa cheke cheke, kile kisu cha juma cha pande mbili kikawa kina zamishwa mpaka ndani ya mwili na kutolewa kama mtwangio ndani ya kinu. Ujanja wote Shikorobo na kuwa na mahusiano na binti wa kibinadamu kukamponza.m. Hakujua binadamu wabaya. Zilipita dakika tano tu mto ulichakufa kwa damu za shikorobo hakuna ata sehemu ambayo kulikua na maji masafi zaidi ya damu za shikorobo. Mwili wa shikorobo ulielea juu kuonesha kwamba amekufa lakini juma hakuamini alichuku tena kile kisu akitaka kwenda kuchinja kabisa shingo yake..........I TAENDELEA.........

at 1:23 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top